RC Chalamila: Wafugaji waliovamia hifadhi waondoke ndani ya siku 6. Mkirusha mikuki tutarusha risasi za moto

RC Chalamila: Wafugaji waliovamia hifadhi waondoke ndani ya siku 6. Mkirusha mikuki tutarusha risasi za moto

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ametoa siku 6 kwa Wafugaji Wilayani Mbarali kuondoa Mifugo katika Hifadhi ya Bonde la Ihefu na Ruaha kabla hawajachukuliwa hatua kali

Amesisitiza "Nimetoa siku sita na nawaonya kwa Mfugaji yeyote atakayekaidi agizo hilo na kuleta mapigano katika uondoaji wa wafugaji hao kwa kurusha mkuki basi vikosi vya Majeshi vitatumia mabomu na silaha za moto"
 
Huyu Rc hana busara katika kutatua mambo, anafikiri kila jambo linahitaji mabomu na risasi za moto.

Hata mkewe wakikosana pengine anamtisha kwa bastola.. ridiculous!
Hao wapuuzi wafugaji ndiyo dawa yao. Hakuna busara wanayoijua zaidi ya hiyo. Waharibifu sana hao, walidhibitiwa kwa muda mrefu lakini naona sasa wamerudi tena.
 
Wafugaji ni watata sana, wakitoka kwenye hifadhi wanakuja kulisha kwenye mashamba ya wakulima, hata watengewe maeneo, wao siyo watu wakuzalisha nyasi za mifugo watulie.
RC na jeshi walinde wakulima watakaoenda kuvamiwa na hao waswagaji.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Wafugaji wanasumbua sana RC yupo sawa. Ila tukisema wafuge kisasa au wapunguze ng'ombe tutaweza bei ya nyama?
 
Aina hii ya ufugaji ni kirusi aisee, Tanzania tuna misitu na mapori yenye ukubwa wa karibia hekta 48 milioni, hawataki kwenda huko....
 
Back
Top Bottom