RC Chalamila: Wanaume wengi wa Mkoani Mbeya wanapenda kulelewa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa mkoa wa Mbeya, wameachiwa jukumu la kuendesha familia zao huku wanaume wakiongoza kufanya vitendo vya dhuluma dhidi ya mali zinazotafutwa na wake zao.

Chalamila ameyasema hayo wakati akifunga kongamano la sita la jinsia ngazi ya wilaya, ambalo limefanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

RC Chalamila amesema kuwa wanawake wengi mkoani humo, ndiyo wanaobeba majukumu ya kutunza na kulea familia, ambapo hufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali ikiwemo kuuza mboga na matunda, wakati wanaume wakitumia mwanya huo kuwafanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kunyang'anya fedha wanazopata kwenye biashara na kwenda kuhonga michepuko.

"Idadi kubwa ya wanaume mkoani Mbeya, wanapenda kulelewa hawapendi kujishughulisha, wanawategemea wanawake kulisha familia na kufanya kila kitu, mbaya zaidi huwashinikiza wake zao kuomba mkopo kwa kutumia account zao ili wadhulumu hizo hela, nawaambia wanawake msikubali kutumika kama ndoa yako ina shida ondoka kaanzishe maisha mengine", amesema RC Chalamila.

EATV
 
Anaiongelea Mbeya ya wapi?
Kwa hiyo kwake yeye Mwanamke kujituma na kubeba majukumu tafsiri yake ni Mwanaume kulelewa.

Muda wote ambao amewekwa hapo kwa nafasi za uongozi maalum ameshindwa kuielewa Mbeya?

Mbeya Wanawake ni miamba wanaume ni miamba.
Halafu Wanawakee wa Mbeya hawana swaga za kulea na wanaume hawana mishe za kulelewa.

Tumuulize yeye aliyeogopa kwenda kugombea na kubaki kwenye nafasi ya kulelewa
 
RC Chalamila amesema kuwa wanawake wengi mkoani humo, ndiyo wanaobeba majukumu ya kutunza na kulea familia, ambapo hufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali ikiwemo kuuza mboga na matunda
Huyu mgeni hajui huu ni utamaduni wa kudumu wa wanawake wa kinyakyusa kwa mkoa wa Mbeya.

Chalamila aache mara moja kutudhalilisha Wanaume wa Mbeya.
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa mkoa wa Mbeya, wameachiwa jukumu la kuendesha familia zao huku wanaume wakiongoza kufanya vitendo vya dhuluma dhidi ya mali zinazotafutwa na wake zao.

Chalamila ameyasema hayo wakati akifunga kongamano la sita la jinsia ngazi ya wilaya, ambalo limefanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

RC Chalamila amesema kuwa wanawake wengi mkoani humo, ndiyo wanaobeba majukumu ya kutunza na kulea familia, ambapo hufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali ikiwemo kuuza mboga na matunda, wakati wanaume wakitumia mwanya huo kuwafanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kunyang'anya fedha wanazopata kwenye biashara na kwenda kuhonga michepuko.

"Idadi kubwa ya wanaume mkoani Mbeya, wanapenda kulelewa hawapendi kujishughulisha, wanawategemea wanawake kulisha familia na kufanya kila kitu, mbaya zaidi huwashinikiza wake zao kuomba mkopo kwa kutumia account zao ili wadhulumu hizo hela, nawaambia wanawake msikubali kutumika kama ndoa yako ina shida ondoka kaanzishe maisha mengine", amesema RC Chalamila.

EATV
Hii ni baada ya kulelewa yeye na mke wake au
 
Anaiongelea Mbeya ya wapi?
Lwa hiyo kwake yeye Mwanamke kujituma na kubeba majukumu tafsiri yake ni Mwanaume kulelewa.
Muda wote ambao amewekwa hapo kwa nafasi za uongozi maalum ameshindwa kuielewa Mbeya?
Mbeya Wanawake ni miamba wanaume ni miamba.
Halafu Wanawakee wa Mbeya hawana swaga za kulea na wanaume hawana mishe za kulelewa.
Tumuulize yeye aliyeogopa kwenda kugombea na kubaki kwenye nafasi ya kulelewa
Mi nimemsamehe bure maana ni shemeji yangu
 
Anaiongelea Mbeya ya wapi?
Lwa hiyo kwake yeye Mwanamke kujituma na kubeba majukumu tafsiri yake ni Mwanaume kulelewa.

Muda wote ambao amewekwa hapo kwa nafasi za uongozi maalum ameshindwa kuielewa Mbeya?

Mbeya Wanawake ni miamba wanaume ni miamba.
Halafu Wanawakee wa Mbeya hawana swaga za kulea na wanaume hawana mishe za kulelewa.

Tumuulize yeye aliyeogopa kwenda kugombea na kubaki kwenye nafasi ya kulelewa
Nafasi za uongozi za kuteuliwa (na sasa za ubunge,udiwani na urais) ni kulelewa kama kulelewa kwingine.
Yeye kwa kuwa ni "me" aliyepo Mbeya,basi naye ni wa kulelewa.
Huyu dogo asitake tutoe mambo yake ya kulelewa kule Moro enzi hizo,tena na mama muuza ndizi.
 
Hili jambo ni taboo kusemwa, ingawa halina shaka ndani yake. Tembelea shughuli nyingi za uzalishaji mali muda wa kazi ujionee ni wakina nani wapo busy na shughuli.

Halafu nenda kwenye vilabu na vikao vya mitaani ujione wazee wakazi wakifanya yao. Halafu time ya mlo, wao ndio wa kwanza mezani. Na wanadai ugali nyama, na sio mchicha wala mnafu.
 
Back
Top Bottom