Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Godfrey Chongolo akiongoza Mkutano wa Nane wa Baraza la Biashara la Mkoa huo amesema malipo ya Wakulima wanaoidai Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) watalipwa malipo yao hivi karibuni na kukiri malipo yalichelewa kidogo.