Uchaguzi 2020 RC Gambo adaiwa kusuka mpango wa kuandaa wazee wa mila ili wamwombe agombee ubunge Arusha

Uchaguzi 2020 RC Gambo adaiwa kusuka mpango wa kuandaa wazee wa mila ili wamwombe agombee ubunge Arusha

Lema mwenyewe yuko mbioni kumuacha Mbowe chama chake,anastaafu siasa anarudi kwenye biashara ya magari
Biashara ya Magari au Wizi wa Magari???nitakuwa wa Kwanza kumpiga Risasi huyu jambazi
 
Kikubwa ni kufutwa kwa Chadema Arusha mjini

Chadema imechelewesha maendeleo Arusha

Wamechelewesha vipi wakati kodi inachukuliwa na serikali. Ubunge hauna uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo. Mbunge ni mpiga debe tu. Kama anataka kuleta maendeleo abakie kama mkuu wa mkoa. Mbunge hana maamuzi yeyote zaidi ya uwakilishi. Vilevile walisema Meya kafanya kazi nzuri sasa atafanyaje kazi nzuri halafu alaumiwe mbunge ambaye ni mwakilishi tu. Cha kujiuliza je mbunge kaongelea bungeni matatizo ya Arusha mjini au hajaongea. Wabunge Tanzania haina faida hivyo kwasababu bugeti ya bunge hata wakipanga inatekelezwa kwa asilimia 30% tu. Yaani hata ukipiga kelele wakaweka budget inaweza hata isije! hiyo ndiyo Tanzania sasa kubadilisha mbunge itasaidia nini
 
CCM watapoteza Jimbo la Arusha Mjini tena wakimpendekeza RC Gambo kugombea.
 
Katika hali isiyo ya kawaida mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo anadaiwa kuandaa wazee wa mila ya kimasai maarufu kama Laigwanan ili waweze kumwomba agombee ubunge katika jimbo la Arusha Mjini.

Wazee hao wa mila wanaodaiwa kukusanywa kutoka maeneo mbambali jijini Arusha ambayo ni Terat,Muriet,Mkonoo,Mateves,Oljoro,Sakina na kata ya kati ambapo wametengewa zaidi ya sh,20 milioni ili kukamilisha zoezi hilo.

Mkakati huo unasukwa kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa Ccm akiwemo mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Arusha, Stephen Zelothe sanjari na mwenyekiti wa Ccm wilaya Joseph Masawe.

Taaarifa za uhakika zimeeleza kwamba wazee hao wa kimila wamepanga Mara baada ya bunge la jamhuri kuvunjwa rasmi watafika nyumbani kwake na kumwangukia ili agombee ubunge wa jimbo la Arusha Mjini.

Mmoja wa wazee wa kimila anayetoka kata ya Terat,Baraka Kivuyo ameelezea kwamba wameambiwa wafike nyumbani kwa kiongozi huyo eneo la Muriet huku wakiwa na mbuzi na kondoo kama ishara ya kumwomba kwa heshima ombi lao.

Hatahivyo,kiongozi Hugo ameelezea kwamba kumekuwa na nguvu kubwa inayoyumika kuwasukuma baadhi ya kiongozi wa kimila ili waende nyumbani kwa Gambo jambo ambalo limeibua sintofahamu katika mkakati huo.

"Kila wiki wanafika viongozi wa Ccm hapa ili kujua tunaendeleaje na mpango wetu wa kujikusanya na kwenda kumwomba Mkuu wa mkoa agombee ubunge" alieleza Kivuyo

Hatahivyo,alienda mbali zaidi na kudai kwamba pia kuna mkakati unaosukwa ili wazee hao wafike mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk John Magufuli ili wamwombe amruhusu Gambo agombee ubunge.

"Ikitokea kwamba Rais Magufuli anafanya ziara hapa Arusha basi sisi wazee tumeombwa na Gambo kwamba atatengeneza mazingira tufike mbele yake na kumwomba amruhusu kijana agombee ubunge" alisisitiza kiongozi Hugo

Mbio za ubunge katika jimbo la Arusha Mjini zinazidi kushika kasi ambapo mbali na Gambo baadhi ya makada wanaotajwa kulimezea mate jimbo hilo ni pamoja na mfanyabiashara maarufu,Philemon Mollel maarufu kama Monaban,wakili wa kujitegemea Albert Msando,wakili wa kujitegemea Edmund Mgemela,meya aliyejiuzulu Calist Lazaro,Dkt Batilda Buriani na wengine mbalimbali.

Mwisho

.View attachment 1453897
Ivi kat ya ubunge na ukuu wa mkoa kipi kina maslahi??? Msaada

Its not over until its over...[emoji769]
 
Ubunge na Ukuu wa Mkoa upi una thamani zaidi kwa madaraka na kipato?
Hataki kuteuliwa ili awe waziri wa misafara ya rais hivyo akiwa mbunge tiyari hiyo nafasi anaipewa kabla ya jioni
 
Back
Top Bottom