RC Hapi aswalisha suala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa Musoma Mara

RC Hapi aswalisha suala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa Musoma Mara

Si ndiye alikuwa amejawa na kiburi dhidi ya Wazee enzi za Mfalme Juha huyu?

Awaombe kwanza radhi wazee.
Wazee gani hao!??? Wale wa Dasalama au Mchikichini kule Kidentutwa B!??? Wazee tuliowajua nchi hii hata before JKN hajazaliwa ni Dkt. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya na Stephen Hilary Ngonyani eikeiei Profesa Majimarefu; hata kwa urefu wa majina yao utajua tu kwamba wana hakimiliki zote za kuwa wazee kwa umri wao. Period!!!
 
Musoma hawatakagi dharau wale..tunakukumbusha tu..nenda nao kwa busara

Naona Musoma ameingia kiunyenyekevu, maana Tabora alienda na wacheza ngoma na waganga wa kienyeji, usiku usiku akawa anatoka tabora anaenda kwa mama yake nzega anarudi tabora alfajiri
 
Wadau wa JF

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally Hapi ameshiriki Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa uliopo Musoma Mkoani Mara

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mara Msabaha Kassimu alimpa nafasi ya Kuswalisha Mheshimiwa Hapi

Mheshimiwa Hapi baada ya Swala alitoa hotuba na alihimiza Umoja, Mshikamano na Ushieikiano ili kuujenga Mkoa wa Mara

Mheshimiwa Hapi aliwaomba Wana Mara kuliombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassani

Hongera sana RC Hapi kwa kuwa mnyenyekevu mbele za Mungu

View attachment 1823390
Hawa wananajisi haya mavazi kwakweli,,,Huyu Naye sio type ya kina saa.nzuri wajameni leo anavaa vazi jeupe na angavu na barakashia juu,,,,daaah🤔🤔
 
Safi sana, ukipewa nafasi ya heshima ya kuswalisha ni jambo la kheri sana kuikimbilia.

Hii mada haina kitu zaidi ya kuibua hisia za udini
Sijawahi kuona Ukianzisha mada enzi za jiwe kukemea kuendesha nchi kutoka madhabahuni
 
Yaani dini nyingine bana ziajidhalilisha hivihivi kwa kujichanganya na siasa kupita kiasi.Ni lazima kuwe na msitari usiovukwa na wanasiasa ktk kuingilia masuala ya Dini. Haiwezekani mtu ambaye hayumo kwenye mfumo wa uongozi wa kuwaswalisha waumini apewe nafasi ya kuswalisha kirahisi hivyo.
 
Hivi si ndo huyu aliesema wapinzani hawastahili kuishi? Hivi hapo anaswalisha kwa kumtumia Mungu yupi? Labda sio Allah!
 
Haka kahuni kahuni ndo kanapewa fursa ya kuongoza ibada? Ana moral authority ipi ya kusimama mbele ya madhabahu kuwaelekez waumini wenzie njia ya haki?
 
Dini ya kiislamu....mtu yeyote anayejua kuisoma qur an na nguzo za swala,masharti yake ruhsa kuongoza ibada.
Sasa watu wanaumia kuona jamaa kaswalisha wanasahau kila mmoja ana haki ya kuabudu kwa mujibu wa katiba awe kiongozi wa nchi au mlala hoi wa kawaida,hongera sana kijana Ally Hapi kwa kuwa kiongozi aliyepitia madrasa na kuijua dini yako vema Allah karim akuongoze akukinge na husda za wabaya wako.
 
Haka kahuni kahuni ndo kanapewa fursa ya kuongoza ibada? Ana moral authority ipi ya kusimama mbele ya madhabahu kuwaelekez waumini wenzie njia ya haki?
Wewe umekamilika au ni msafi sana zaidi yake?
punguza chuki kijana au amevunja sheria kuswalisha?
 
Hawa mashehe ubwabwa wanatia aibu.
Ina maana Musoma Kuna uhaba wa maimamu kiasi hicho? Si mje Sumbawanga mvhukue hata watatu.....
Wewe huijui dini ya kiislamu bora kutulia kimya....imam ndio kiongozi mkuu wa ibada anamamlaka ya kumchagua mtu yeyote aswalishe hata mwanafunzi mdogo anayejua tu kusoma qur ani na kuifahamu swala, basi rukhsa kuswalisha usipagawe sana mkuu ni kawaida...hujawahi kumuona Erdogan anasoma Qur an kwa ahkam Tajweed kama sh. Abdulbasit abdusamad uislamu hauangalii cheo wala nyadhifa zako.
 
Back
Top Bottom