RC Hapi: Jumamosi ya pili ya kila Mwezi itakuwa ni siku ya kufanya mazoezi watumishi wa umma na Wananchi wote mkoa wa Iringa

Taifa linalojielewa zaidi hii ni elimu ambayo watoto wa primary na secondary wangekuwa wanafundishwa darasani
Taifa lenye utawala wa kidemokrasia lina elimisha kuhusu faida za kufanya mazoezi. RC angeandaa elimu na kutafuta air time kwenye TV na Radio.
 
kazi kweli kweli,...sijui wasioenda mazoezini watachapwa fimbo? 🤣 🤣 🤣
 
Nyie wasabato mtafanya jumapili
Jumamosi ni sabato ya bwana siku ya saba ya Juma,ambapo tunamuabudu Mungu ktk roho na kweli, This RC should respect faith and belief of others,God is bigger than our different careers,
 
Hivi yupo huyu?
.
Hajui mazoezi mtu mziima anapaswa kushauriwA na daktari kwamba afanye mazoezi kwa kiwango gani
 
Hivi lile tamko la kifanya usafi kila mwezi liliishia wapi?

Je ile amri ya makamu rais ya kufanya mazoezi nayo iliishia wapi?
 
Hivi lile tamko la kifanya usafi kila mwezi liliishia wapi?

Je ile amri ya makamu rais ya kufanya mazoezi nayo iliishia wapi?
Dar es salaam bado linaendelea Jumamosi ya mwisho ya kila mwezi hasa pale Kariakoo maduka yanafunguliwa saa 4, inaboa sana!
 
Aangalie asiingilie uhuru wa watu kuabudu - Iringa kuna Waadventista Wasbato wengi wanaoabudu siku ya Jumamosi ya kila wiki - hapo kutatokea shida.

Pili, watumishi wa Umma mishahara yao ni midogo sana hivyo siku hiyo wengi wao huitumia kuhangaikia vyanzo vingine vya mapato ili familia zao zineemeke,

Tatu, RC aangalie njia nyingine ya kuhamasisha watu kufanya mazoezi "ili hata akihama, kuachishwa, kufa, nk wananchi waendelee voluntarily kufanya mazoezi hayo vinginevyo hatafanikiwa,

Nne, kipindi hiki mikoa mingi watoto wa darasa la saba wamefaulu mitihani yao na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza lkn madarasa ni pungufu - hivyo RC Happi angetumia nguvu ya wananchi siku hiyo kujitokeza kusaidia ujenzi wa miundombinu ya madarasa, vyoo, mabweni, ofisi za walimu nk nk

Kwa ufupi, "afanye maamuzi baada ya kufanya cost benefit analysis"

Msakila M Kabende
Kigoma
 
Muda si mrefu tutasikia mtumishi kala mboko za matako Iringa.
 
Watu waliosoma vyuo vya kati wanamatatizo
 
Huyu naye anatafuta sifa tu! Anaturudisha tulikotoka 2015, watu wanahitaji kuchapa kazi
 
Atawaendesha sana awamu hii si kaona Peter Msigwa hayupo mtetezi wa wana Iringa!
 
Hatua za kisheria.

Sheria gani bwana wewe???

Wapeni hamasa watu wenu wafanye mazoezi ila msiwalazimishe.

Najua mtaanza kuwalazimisha walimu maana ndio guinea pig wenu wa kujaribu kila kitu.
 
Hatua za kisheria.

Sheria gani bwana wewe???

Wapeni hamasa watu wenu wafanye mazoezi ila msiwalazimishe.

Najua mtaanza kuwalazimisha walimu maana ndio guinea pig wenu wa kujaribu kila kitu.
Aisee!! hatari sana,walimu ndio guinea pig ya wanasiasa!!
 
Hivi hawa "uchwara" wanapata wapi jeuri hii"
Hakuna sheria inayowapa mamlaka hayo.
Uhuru binafsi ni haki ya msingi.
Afya ya mtu ni kitu binafsi na hakujawahi tokea kokote kulazimishwa kufanya mazoezi. Haya huhusu magonjwa ya mlipuko tu.

Kwa aina hii ya uongozi tutegemee ujinga mwingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…