RC Kafulila awanyoosha wachina wa CHICCO, ni wale waliotaka kutupiga TZS 15BL kwenye ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa kilometa 57 kwa TZS 75BL

Kawanyoosha vipi?kwa kuwaambia waludie kujenga?umejiuliza walipataje hiyo tenda?wao ndio wanatunyoosha,wanatoa Rushwa tenda inakuwa ya bei kubwa,Cha juu wanakula watendaji serikalini,mwishoni ni mwananch ndio ananyooshwa
Serikali yetu imejaa majizi na matapeli tupu
 
Yaani ile barabara serikali imepigwa vibaya mno.Barabara kabla ya kuzinduliwa ishaanza kupasuka na kuwa na mashimo.
 
Yaani Hii Nchi ina matatizo makubwa Sana ya watu waadilifu..

Yaani hapo kuna Meneja wa TanRoads Mkoa,kuna Project Supervisor ,kuna Consultant nk..

Wote hao wapo walikuwa wanaona na wakitaka wanyamazie Ili wagawame pesa na Wachina..

Nilishangaa hata ile barabara ya Kibaha Highway ilibidi Waziri wa Ujenzi Mbarawa aagize kufumuliwa na kujengwa upya kipande Cha km 2 Kwa sababu kama hizo..

Sasa hii ni Miradi Mikubwa pata picha miradi midogo ya huko Mawilayani..

Ni vyema linapokuja kwenye swala la kuleta mzaha kwenye pesa za umma sheria za kufilisi na kupigwa ndani ziimarishwe..
 
Tanzaania Mabarabara mengi yamejengwa chini ya kiwango, hivi sasa kila barabara inaviraka,

#Tunahitaji akinakafulila wengi Sana Tanzania
Ni uzembe wa Wakuu wa Mikoa/Wilaya na Takukuru kwenye masuala hayo..

Mkiwaachia Watendaji huwa Wana compromise na wakandarasi wanagawana pesa..

Hukuona yule Engineer aliyemdindishia Waziri wa Afya kwa mambo kama hayo harafu akapata na watetezi?

Mh.Rais viongozi wa kitaifa,mkibaini mambo ya hovyo kama haya muwe mnawawajibisha kuanzia RC na watendaji wengine wote waliohusika ila kuwachekea ni hatari..

Kuna mambo mengi Sana ya hovyo huwa yanafanyika harafu hatua hazichukuliwi tena wanaosimamia hufanya makusudi..

Mara nyingi sana utakuta wasimamizi kutetea hujuma za wakandarasi.
 
Kafulila chapa kazi rekodi yako inafahamika tangu ulipokuwa Mbunge baadaye Katibu Tawala wa Mkoa na sasa Mkuu wa Mkoa huna jambo usilolijua kuhusu utendaji kazi wa Serikali
 
Kafulila yuko vizuri Sana,
 
Hapa unatafuta ugomvi mkubwa na mataga
Tanzaania Mabarabara mengi yamejengwa chini ya kiwango, hivi sasa kila barabara inaviraka,

#Tunahitaji akinakafulila wengi Sana Tanzania
 
Mkurugenzi wa TANROADS alikuwa wapi

Waziri wa ujenzi naye alikuwa wapi

Team ya ufundi ya TANROADS inafanya nini mpaka RC abaini makosa yote hayo tena ya kitaalamu
Walipata 90% yao wakagawana na kusepa, wakamwachia mkandarasi 10% ya kufanyia kazi chini ya kiwango.
 
Mtaka alikuwa anawaweka wanafunzi kwenye Makambi tu hajui hata nini kinaendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…