RC Kafulila awanyoosha wachina wa CHICCO, ni wale waliotaka kutupiga TZS 15BL kwenye ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa kilometa 57 kwa TZS 75BL

RC Kafulila awanyoosha wachina wa CHICCO, ni wale waliotaka kutupiga TZS 15BL kwenye ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa kilometa 57 kwa TZS 75BL

Endelea na moto ule ule wa kupandisha nyuzi za kafulila humu ndio tutajiridhisha kuwa wewe hukuwa chawa wake. Kwisha habari yenu kmmmk. Na bado!!!!!!
Kafulila hana pesa ya kunipa mimi,

Mimi ni mzalendo napenda viongozi wanaosimamia masilahi ya Watanzania haijalisha nini kitawapata kwa kusimamia kwao hayo masilahi,
 
Mkurugenzi wa TANROADS alikuwa wapi

Waziri wa ujenzi naye alikuwa wapi

Team ya ufundi ya TANROADS inafanya nini mpaka RC abaini makosa yote hayo tena ya kitaalamu
maajabu matupu aise
 
View attachment 2290873


Kampuni ya kichina ya CHICCO yatekeleza agizo la RC Kafulila, tayari imekamilisha marudio ya barabara yenye urefu wa kilometa 10 zenye thamani ya tzs15bl.

==
Kampuni ya Kichina ya CHICCO inayotekeleza ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi - Maswa yenye urefu wa kilomita57, ilianza ujenzi tangu mwaka 2018 kwa thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania billion 75. Wachina hawa walikwaa kisiki baada ya kutakiwa kurudia ujenzi wa vipande vya barabara vinavyofikia kilometa 10 kutokana na kujenga chini ya kiwango kilichowekwa.

Agizo hilo la kutakiwa kurudia ujenzi lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe David Kafulila Juni 5, 2021 ikiwa ni wiki moja tu baada ya kuripoti mkoani Simiyu kama Mkuu wa Mkoa mpya. Leo ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu agizo hilo, RC Kafulila akihojiwa na kituo cha EATV amekiri kuridhishwa na kazi iliyofanywa na kwamba ujenzi upo zaidi ya asilimia 96% kwa viwango vinavyokubalika.

"Nakumbuka ilikuwa ni wiki ya kwanza baada ya kuripoti kama RC, hii barabara niliona wakati nakuja kuripoti Simiyu. Nilifanya ziara na Bodi ya Barabara na kuelekeza marudio ya barabara na kumwelekeza mkandarasi kurudia. Nilimsisitiza barabara yake haitapokewa na Mhe. Rais ikiwa chini ya kiwango" alisema Kafulila na kuongeza kuwa, "mbali ya kurudia barabara, pia mshauri mwelekezi(consultant) alibadilishwa. Sasa watu wote wakipita wanafurahi kuona serikali sasa itapokea barabara imara sawa na thamani ya fedha zao wanazozitoa kupitia kodi na tozo mbalimbali."

"Huu ni ujumbe wangu kwa wakandarasi wote mkoani Simiyu, hakuna mradi utakaopokelewa ukiwa chini ya kiwango. Kwasasa nina amani hata Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan akipita kukagua nina amani kwamba fedha iliyoletwa ndani ya mkoa wetu kwajili ya barabara na hata miradi mingine, thamani ya pesa(value for money) inaonekana. Wakandarasi wababaishaji hawana nafasi, nimeshavunja na nitaendelea kuvunja mikataba na kila mbabaishaji aliyepata mradi kwa bahati mbaya Simiyu," alisisitiza zaidi.

"Serikali inalaza mabilioni ya fedha barabaran ndio maana lazma kuhakikisha tunabanana. Yaani gharama kilomita 1 ya lami ni takribani 1.5 bn., pesa ambazo zinatosha kukamilisha majengo ya kituo cha afya. Sasa upewe mabilioni yote hayo na bado ukabidhi barabara ambayo baada ya mwaka tu imeharibika na kuhitaji mabilioni mengine ya ukarabati? Huu ni ushenzi ambao hauwezi kupewa nafasi ndani ya awamu ya sita, na kwa upande wetu tutatimiza kipande chetu Simiyu, " alimalizia.

#SISITUKO TAYARI KUHESABIWA TAREHE 23/08/2022,WEWE JEE?!

Kazi nzuri sana Kafulila
 
Mheshimiwa kafulilt ni mzalendo kwelikweli.apewe tu nafasi ya kurejea Bungeni hapo mwakani maana sauti na mchango wake unahitajika sana.
 
machawa wa Ngedere ni wale wale na ID zao ni zile zile hapa JF;
Mwanahabari wa taifa
CM 1774858
Lucas Mwashamba
 
Back
Top Bottom