Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, Julai 28, 2025 amewasimamisha viongozi wa chama cha wafanyabiashara wa nyama mkoani Katavi kwa tuhuma za ukiukwaji wa sheria, taratibu na miongozo ya uendeshaji wa biashara, ikiwa ni pamoja na kupandisha bei ya nyama bila kushirikisha mamlaka husika
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya viongozi hao kupandisha bei ya nyama bila kufuata utaratibu unaotakiwa, jambo lililosababisha usumbufu kwa wananchi na kuibua sintofahamu juu ya mwenendo wa biashara hiyo
Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa ametangaza kuivunja rasmi kamati ya uongozi wa wafanyabiashara hao na ameagiza mchakato wa kuandaa katiba, kusajili chama hicho rasmi, na kufanyika kwa uchaguzi halali wa viongozi usimamiwe mara moja na viongozi wa mkoa
Sambamba na hilo, ameagiza bei ya nyama kurejea katika kiwango cha awali cha shilingi 10,000 kwa kilo kutoka 12,000 ili kuepusha kuwaumiza walaji, huku mashauriano yakiendelea kufanyika kwa lengo la kubaini sababu za kupandishwa kwa bei hiyo
Amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpanda kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote aliyetoa amri ya kusimamisha uchinjaji katika machinjio, akimtaka kumtambua, kubaini sababu za kutoa maagizo hayo, na kuhakikisha anachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria