RC Kigoma afanya ziara kukagua miradi ya maendeleo, asema barabara za vumbi zitasahaulika kuelekea Tabora

RC Kigoma afanya ziara kukagua miradi ya maendeleo, asema barabara za vumbi zitasahaulika kuelekea Tabora

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Serikali mkoani Kigoma imeahidi kuendelea kusimamia kwa ufanisi miradi yote ya Maendeleo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ubora kama ilivyopangwa sambamba na kutosita kuchukua hatua kwa mkandarasi yeyote atakayekiuka makubaliano ya mkataba na kukwamisha miradi hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mkoa wa Kigoma na kuwataka wananchi mkoani humo kuendekea kuiamini serikali katika usimamizi na utekelezaji wa miradi iliyoianzisha kwa lengo la kutatua kero zao.

Soma pia: Pre GE2025 Madiwani Kigoma ujiji walalama miradi ya maendeleo kukwama hivyo kuonekana hawajatimiza wajibu wao, waishutumu TAMISEMI wakitaka uchunguzi ufanyike

Amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia, mkoa umepokea Shilingi Tril. 11.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo huku baadhi ya miradi utekelezaji wake umekamilika na ambayo haijakamilika ipo katika hatua za utekelezaji na hakuna mradi uliokwama.

Amesisitiza kuwa masuala yote ya ujenzi yanasimamiwa na kanuni na Sheria zinazotokana na mikataba hivyo mkandarasi anapotakiwa kuongeza muda wa utekelezaji mradi, serikali itahakikisha nyongeza ya muda huo itakuwa ni ile inayokidhi matakwa ya kimkataba.

 
Back
Top Bottom