Hekima ya viongozi Kama Hawa ndio inaweza kuiponya Nchi, Rais angekuwa na washauri wenye hekima Kama huyu nadhani angekuwa Rais Bora.
Senegal wametengeneza vifaa vyao vya kupima raia Nchi nzima sisi kwetu tunasubiri mpk mtu ajipeleke? Haya Mama huyu asingeongozwa na hekima ya mungu angeambukiza wangapi/ameshaambukiza wangapi??.
Inasikitisha Sana Kama tumepata uwezo wakununua ndege by cash money tunakuja kukosa pesa ya kununua vifaa vya kupimia walipa Kodi😭😭😭, pesa zinazochangwa na watu na taasisi binafsi zinafanya kazi gani??, Serikali Haina pesa za majanga??.
Kiukweli inasikitisha na INAUMA sana, wale waliokuwa wanaukejeli na kuwakejeli watanzania kuwa Corona ni ugonjwa mdogo hawawezii kufunga mipaka, kuzuia watalii leo hawaonekani tena!! Wameenda wapi? Waje watuonyeshe huo upendo wao kwetu katika kipindi kigumu Kama hiki, Bashiru, polepole, makonda mko wapi nyie ndio wapambanaji wetu njooni.
Hongera waziri mkuu kassim majaliwa, 2025 Kama ntakuwa hai basi ntakuchukulia fomu ya kugombea urais unafaa kuwa jemedali wa Vita huna chembe ya unafiki.
Hongera ummy mwalim tunajua unayoyapitia lkn umeonesha kujitoa ktk wakati mgumu.