RC Kunenge: Kariakoo ilikuwa kama Dubai, tujitahidi kuirejesha tuwavutie Wacongo na Wamalawi

RC Kunenge: Kariakoo ilikuwa kama Dubai, tujitahidi kuirejesha tuwavutie Wacongo na Wamalawi

Mazingira yamevurugwa sana!! Kumekuwa kama gulio!! Hata hakupitiki
 
Ndiyo chama kikuu cha upinzanini, ilianza kulizungumzia hili swala tangu 2016 lakini hao CCM waliwaita ni wasaliti wasiopenda kodi ikusanyiwe, sasa CHADEMA wametulia wao CCM wameanza kuongea yaliyoongelewa 2016 na CHADEMA mfano Nape na Msukuma na leo Kunenge.
Kongole mkuu chadema waliona mbali sana haya mambo
 
Wanasiasa wanapopenda kufananisha nchi au miji yao eti ilikuwa kama Dubai, huwa najiuliza wanakusudia Dubai ipi? Ile ilivyokuwa Jangwa ama hii ya sasa? Maana sikumbuki hata siku moja kama kuna Mji hapa TZ uliwahi kuwa kama Dubai
 
Swala la kodi na mtindo wa ukusanyaji ni tatizo. Yes, kodi ilipwe lakini kuna mambo hayapo sawa.
 
Kuna sehemu Dubai inaitwa Deira wengi waliofika wanapajuwa. Hii sehemu ndio utawakuta waafrica, wahindi na wengi tu ndio kama kariakoo yetu. Utakuta askari wako lakini hukuti wanamuuliza mtu kitu sio kwamba hawaoni wanawake wanaojiuza hapo wanaona kila kitu na ile nchi unajuwa sheria zake. Ila wanafunga macho muhimu usivunje sheria na wanalinda usalama ila waanacha movement zote free kabisa hawagusi mtu wanalinda mazingira ya biashara. Sasa jiulize kwanini wanafanya vile? wanajuwa hawa wanakuja kununua wanatoka sehemu tofauti bila hawa hakuna Deira ila ukikutwa unafanya ujinga huo sehemu zingine unakamatwa. Kariakoo ilitakiwa tuifanye kama Deira.
Biashara yoyote haitaki usumbufu,vitisho nk

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kuvunja ni rahisi, kujenga ni taabu. Sasa watu wamejenga maisha yao miaka hamsini. watu wamejenga biashara zao miaka hamsini . wamapata nafasi kufungua biashara zaokwa dhiki sana. Na wakati wa Mwalimu, ilikuwa hamna kodi, kodi zimeanza baada ya Mh. Mkapa tena kidogo dogo na kwa Kikwete, mdogo mdogo. Ghafula ameingia Jiwe kwa kishindo. ameanza kuwa dhalilisha wafanya biashara na kuwanyang'anya mali zao. Ameweka mkuu wa mkoa wa daresslaam mwizi na jambazi. Kila biashara inatozwa kodi miaka kadhaa iliopita venginevo biashara inachukuliwa. Sasa hiyo Dubai itarudi wapi wakati mumekwisha kuwadhulumu wafanya biashara. wamachinga pia hamukuwawacha kwa kisingizio cha kodi. Pesa mumechukuwa kufanya siasa. Nchi hii haina pesa. watu hawana pesa, biashara haina pesa. matajiri hawana pesa. masikini pia hawana pa kuzitafuta. Tutegemee nini?. Dubai itakuja tu?. wawekezaji hawaji tena. wa tanzania tumeshindwa kusimama na nchi yetu tutegemee nini?.
 
Act
Kaka sisi wafugaji wa kuku wa mayai tunajua principal; kuku lazima ale kwa siku gram 125 ya chakula ili na wee upate yai moja!
Sasa mlishe pumba tupu uone kama utapata hilo yai.

Sasa kuna watu hawampi kuku hata hiyo pumba afu eti wanategemea aendelee kutaga...thubutu!Actually hakupi yai moja kwa siku ila wastani wa mayai 5 kwa siku saba. Halafu anakuja mtu anakudai mayai 3 kama kodi!
 
Inaumiza Sana.. basi tuu. Mi nafikiri Ingependeza mtu unachuma chochote huko nje unaleta nyumbani bila kubugudhiwa Watu wasingekuwa wanaficha mahela huko nje
Usitegemee lolote toka kwa watu wanaowaza kinyumenyume. Mtanzania anaishi Malawi miaka 3 anakusanya mtaji mil.100 anaamua kurudi nyumbani, akifika mpakani anapewa kesi ya uhujumu Uchumi na fedha yote inataifishwa, sasa sijui kaujumu uchumi wa nchi gani?
 
Kumbuka mji mkuu umehamia dodoma. So iyo lazima ilete ifect katika masoko.
 
Wakati watu wanalalamika mlisema hao ni wapiga dili
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh Kunenge amesema Dar es salaam ilikuwa kama Dubai ikizihudumia nchi za Afrika mashariki lakini haijulikani kitu gani kimeirudisha nyuma.

Kunenge amewataka watendaji wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha Kariakoo inarejea kuwa Dubai ya Afrika mashariki kama ilivyokuwa enzi zile.

Chanzo: ITV

Maendeleo hayana vyama!
Watendaji wa JiJi ndiyo wameliharibu JiJi kwa kua kero sana kwa Wafanyabiashara,hadi wakakimbia na wengine wameacha kufanya biashara wanawasoma Watendaji Sasa watakula wapi!?
 
Back
Top Bottom