RC Kunenge: Kariakoo ilikuwa kama Dubai, tujitahidi kuirejesha tuwavutie Wacongo na Wamalawi

Mazingira yamevurugwa sana!! Kumekuwa kama gulio!! Hata hakupitiki
 
Kongole mkuu chadema waliona mbali sana haya mambo
 
Wanasiasa wanapopenda kufananisha nchi au miji yao eti ilikuwa kama Dubai, huwa najiuliza wanakusudia Dubai ipi? Ile ilivyokuwa Jangwa ama hii ya sasa? Maana sikumbuki hata siku moja kama kuna Mji hapa TZ uliwahi kuwa kama Dubai
 
Swala la kodi na mtindo wa ukusanyaji ni tatizo. Yes, kodi ilipwe lakini kuna mambo hayapo sawa.
 
Biashara yoyote haitaki usumbufu,vitisho nk

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kuvunja ni rahisi, kujenga ni taabu. Sasa watu wamejenga maisha yao miaka hamsini. watu wamejenga biashara zao miaka hamsini . wamapata nafasi kufungua biashara zaokwa dhiki sana. Na wakati wa Mwalimu, ilikuwa hamna kodi, kodi zimeanza baada ya Mh. Mkapa tena kidogo dogo na kwa Kikwete, mdogo mdogo. Ghafula ameingia Jiwe kwa kishindo. ameanza kuwa dhalilisha wafanya biashara na kuwanyang'anya mali zao. Ameweka mkuu wa mkoa wa daresslaam mwizi na jambazi. Kila biashara inatozwa kodi miaka kadhaa iliopita venginevo biashara inachukuliwa. Sasa hiyo Dubai itarudi wapi wakati mumekwisha kuwadhulumu wafanya biashara. wamachinga pia hamukuwawacha kwa kisingizio cha kodi. Pesa mumechukuwa kufanya siasa. Nchi hii haina pesa. watu hawana pesa, biashara haina pesa. matajiri hawana pesa. masikini pia hawana pa kuzitafuta. Tutegemee nini?. Dubai itakuja tu?. wawekezaji hawaji tena. wa tanzania tumeshindwa kusimama na nchi yetu tutegemee nini?.
 
Act
 
Inaumiza Sana.. basi tuu. Mi nafikiri Ingependeza mtu unachuma chochote huko nje unaleta nyumbani bila kubugudhiwa Watu wasingekuwa wanaficha mahela huko nje
 
Kumbuka mji mkuu umehamia dodoma. So iyo lazima ilete ifect katika masoko.
 
Wakati watu wanalalamika mlisema hao ni wapiga dili
 
Watendaji wa JiJi ndiyo wameliharibu JiJi kwa kua kero sana kwa Wafanyabiashara,hadi wakakimbia na wengine wameacha kufanya biashara wanawasoma Watendaji Sasa watakula wapi!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…