RC Makalla atoa Wiki moja kukomeshwa biashara ya ngono, awataka Polisi kuvaa kiraia na kujifanya wateja

RC Makalla atoa Wiki moja kukomeshwa biashara ya ngono, awataka Polisi kuvaa kiraia na kujifanya wateja

Hao polisi hawawezi kuwakamata hao wadada mana ishu utakuja hao wadada watakapowauliza polisi wataje ni kifungu kipi Cha PGO kinachowapa mamlaka hayo. Hapo ndo kila polisi atatawanyika kwa njia yake mana Kibatala shule yake imefika kwa kila mmoja na kila mtu anajua kuwa adui wa polisi kwa sasa ni PGO. RC Makala watumie mgambo.
Samahani mkuu kirefu cha "PGO" ni nini?
 
Kaka na dada waliozaliwa na baba mmoja na mama mmoja au? Kaka na dada wa bamdogo labda na wa bamkubwa
Tafuta humu. Mdada mmoja amejinyonga huko Singida. Kafumaniwa na mama mdogo akilala na baba mdogo. Tafuta, Mada hiyo imetoka Leo hii humu jf
 
Hawezi kuwatokomeza kamwe watawakamata ndio ila watatoka na pia wanambinu nyingi siku hizi, wanachotaka kufanya ni bei kupanda tu saiv buku tatu 1$ unachuja vizuri tu chumba chake ndom yake, sasa wakiwabuguth itabid guest kulipia elfu tano na wao elfu tano nafikir ubakaji utaongezeka
 
Polisi hawahawa wa night kali doria wakomeshe hii biashara
 
makalla-12-1080x570-1.jpeg

Picha: Mkuu wa Mkoa Amos Makalla

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa Wiki moja kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanadhibiti watu wote wanaofanya biashara ya Ngono kwenye eneo la Manzese Uwanja wa Fisi baada ya suala hilo kulalamikiwa na Wananchi.

Malalamiko hayo yametolewa wakati wa Mwendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua Migogoro ya Wananchi Jimbo la Kinondoni ambapo wamedai kuwa imefikia hatua biashara hiyo inahusha pia utumikishaji wa kingono kwa watoto wadogo Jambo ambalo ni kinyume na sheria na maadili.

Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Jeshi la Polisi kuwatuma askari watakaovaa nguo za Kiraia na kuwanasa watu wote wanaofanya biashara ya ngono.

Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa kata na Mtaa huo kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kumaliza suala hilo.

Bongo Five
Tafuta chanzo cha tatizo, ufumbuzi utakuwa rahisi. Hakuna mwanamke kwa kawaida anapenda kujiuza. Ni kudharilika kulikopitiliza. Japo sasa ni shughuli rasmi, ikiwa mbadala kwa ukosefu wa shughuli nyingine yenye heshima kwa jamii.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kwani makahaba wanakaa Road siku hizi
Makahaba wako kwenye maclub,majumbani nk
Na ukishawazuia makahaba kuingia kwwnye maclub,basi hapo ushaharibu biashara
Kuna biashara zingine zinaendana na anasa

Kwani siku hizi.ohio St,Tunisia Road kuna makahaba wanakaa

Ova
 
Dalili za kukosa ubunifu na kukosa kazi za kufanya.

Hii biashara imekuwapo hata kabla ya nabii Issa.

Hii biashara iko duniani kote na katika miji yote.

Wewe kama si mteja au mdau inakuhusu nini?

Hivi wa machinga kesha malizana nao?
Mtaka nyingi na saba hufikwa na mwingi msiba!

Muda upo, angeenda polepole na kwa uhakika kabisa!
 
makalla-12-1080x570-1.jpeg

Picha: Mkuu wa Mkoa Amos Makalla

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa Wiki moja kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanadhibiti watu wote wanaofanya biashara ya Ngono kwenye eneo la Manzese Uwanja wa Fisi baada ya suala hilo kulalamikiwa na Wananchi.

Malalamiko hayo yametolewa wakati wa Mwendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua Migogoro ya Wananchi Jimbo la Kinondoni ambapo wamedai kuwa imefikia hatua biashara hiyo inahusha pia utumikishaji wa kingono kwa watoto wadogo Jambo ambalo ni kinyume na sheria na maadili.

Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Jeshi la Polisi kuwatuma askari watakaovaa nguo za Kiraia na kuwanasa watu wote wanaofanya biashara ya ngono.

Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa kata na Mtaa huo kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kumaliza suala hilo.

Bongo Five
Suala la biashara ya ngono kwa wanawake ni ngumu sana kudhibitiwa kwa sheria zilizopo,maana wakikamatwa watashtakiwa kama wazururaji na si watu wanaojiuza.

Mwaka 2012 suala hilo la kukamata Chagudoa lilizua sintofahamu iliyofikia kurushiana maneno baina ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kinondoni Charles Kenyela na Wa Temeke Englibert Kiondo kwa namna kila mmoja alivyokuwa akiliendea.

Kiondo alitaka suala hilo lishughulikiwe kijamii zaidi kwa kuwa kuna sababu nyingi za kiwafanya wanaojiuza kujiuza na wanaonunua kununua.

Kenyela alitaka kukomesha kwa kuwakamata,lakini mwisho wa siku hakukuwa na kifungu kilichothibitisha kama yaliyokuwa yakifanyika ni biashara au makubaliano ya wapenzi na matokeo yake watuhumiwa walikuwa wanahamishiwa mahakama ya jiji
 
Back
Top Bottom