RC Makalla: Kuanzia usiku wa leo hakuna Panya Road atasalimika, operesheni inayoanza si salama kwao

Hawa watoto sio wa kuwapeleka polisi...solution nzuri ni kumalizana kabisa ili tuheshimiane.....

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Mawazo ya kipuuzi kbs na mawazo km haya ndy wanakuwa Nayo polisi baadhi wakishapewa kazi ya kuingia mtaani kutafuta wahalifu..

Enzi hizo za wahuni wa Temeke Mimi nimewahi kusombwa polisi kisa tupo kitaani tunacheza draft na polisi wanatafuta vikundi vya kihalifu

Wangekuwa na mawazo km yako wengi tungekufa bila hatia

Km umezaliwa uswahilini wanakotokea hawa panya road,mburahati,kigogo,manzese,tandika nk haiwezi kuepuka kukutwa na majanga ya kihalifu ktk safari ya maisha yako..

Hao watoto wamejikuta Tu wamezaliwa uswahilini,hawakujichagulia wao wenyewe ingawa uhalifu ni Jambo walilolichagua..Polisi wakiingia mtaani wanachojua wanaenda kukamata panya road uswahilini,sasa mara kadhaa inatokea wanakamatwa na wasiohusika..Je,kuua ni solution?? Fikiria tena mkuu!!

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Hivi Wale Machinga Waliovunjiwa Vibanda Vyao Walienda Wapi?

Au ndo hawa Wametafuta alternatives...!
 
Unahangaika kupata kipato siku nzima yote. Ukirudi nyumbani vibaka aichukue yote na kukuua kisa unafanya kazi.

Mbadala ni kuwaachia nchi vibaka.
 
Sasa sielewi unaweza vipi kuthibitisha huyu ndiye huyu siye? hebu tuambie. Hawa vijana ni washenzi na hwana huruma na mtu serikali ni lazima tena wamechelewa sana mpaka jana Raisi kaamua kuliongelea hadharani IGP Sirro ajitafakari kama anastahili kuwepo hapo. Police wana mapungufu yao lakini kwa hili nawaunga mkono 100% mkijuwa ndio hawa nawaomba msijaze jela zetu piga wacha wakawazike hakuna huruma katika hili kama wewe mzazi hujui mwanao yuko wapi na makundi gani usije kujilaumu. Mtoto akikaa na wavuta bangi na yeye kama mvuta bangi kama yuko na makundi haya ni hao hao hakuna cha haki ya binadamu wala nini tembeza kipigo sawasawa. tutajuwa mchele ni upi na mchanga upi mbele ya safari.
 
Unatetea upuuzi kabisa. Unasema vijana wote maskini wawe wahalifu?
 
Afadhali wamefanya yao kabla ya sikukuu...

wadhibitiwe mapema...

Mazalia ya omba omba hayo..watoto hawana kwao!
 
Ngoja wakugundue watakutembelea mtaani kwako soon.....huwa wanatumia nusu saa tu ..polisi wanafika baada ya lisaa limoja
 
Kitendo Cha kuongezeka kwa matukio ya uhalifu ni dhahiri kwamba maisha ni magumu Sana na tutashudia mengi Sana haya ya Panya Barabara ni mwanzo tu
 
View attachment 2208639

Yaani mbinu nzuri ingekuwa ile ya kipindi cha Augustino, mzazi au ndugu unapewa taarifa kachukue maiti sehemu fulani au mochuari.

Hiyo ya nenda kituo cha polisi imekaa kama ina upendo fulani hivi!.

hiyo geresha tu nenda kituo cha polisi ukiangalia kwa JICHO LA TATU utagundua ni nenda WODI NAMBA 26
ukifika POLISI utaambiwa nenda WODI NAMBA 26 MUHIMBIRI
sasa ukifika MUHIMBIRI ukiuliza WODI na 26 ipo wapi unashangaa unaelekwezwa JENGO LA WODI NAMBA 26 linatazamana na TAASISI YA MOYO
 
We umeshashasikia kuna msako wa kuwakamata wahalifu halafu unaenda kukesha vijiweni unacheza draft..hapo ukikamatwa unamlaumu nani sasa
 
We umeshashasikia kuna msako wa kuwakamata wahalifu halafu unaenda kukesha vijiweni unacheza draft..hapo ukikamatwa unamlaumu nani sasa
Haha, kuna watu wapuuzi sana. Watadai haki za kibinadamu zinavunjwa. Za wengine wanaofata sheria, wanaoibiwa,kupigwa, kuuawawa, kutoweza kutembea kwa uhuru hazivunji.

Tunajali haki za wahalifu tu.
 

Msako wa Nyani, Ngedere haponi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…