RC Makalla: Machinga wote Dar walio katika hifadhi ya barabara, Wataondolewa na vibanda vyao kuanzia Septemba 13, 2021

RC Makalla: Machinga wote Dar walio katika hifadhi ya barabara, Wataondolewa na vibanda vyao kuanzia Septemba 13, 2021

Watamwambia hawana maeneo mbadala ambako watapata wateja, hapo makalla atasemaje.....
 
Pale boma ilala pamemezwa kote na wamachinga wanasogelea ile stendi now,mbezi mwisho ile barabara ya kwendea kinyerezi kali sana lakini chinga wameichafua kuanzia pakuingilia upande wa moro rd mpaka kwenye round about ya malamba mawili,yale maeneo kiustaraabu yanabidi yawe masafi yote
 
Safi sana! jamaa wamegeuka kero kubwa katikati ya mji hata Mwenge pia!
Kama mbagala ndio kero kabisa hadi wachina wanaojenga barabara za BRT, wanatishiwa kupigwa kuwa wanawasumbua kila mala kuwahamisha mala hapa tunataja kujenga tokeni!!na zile sehemu zote walizoisha weka lami tayari ndio sasa zinatumiwa na wamachinga na sio magari tena!!na wanakuwa wakali kweli
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh Makalla amesema zoezi la kulirejesha jiji pamoja na mkoa mzima katika hadhi yake litaanza ambapo Wamachinga wanaofanya biashara zao barabarani na katika hifadhi za barabara wataondolewa.

Makalla amesema wamachinga wote wanapaswa kufanya biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa na siyo vinginevyo.

Source: Clouds tv

cc: Mmawia
Better
 
Waondolewe tu maana pamekuwa chaka la vibaka
Upo nje ila unashindwa hata kupumua
Nidhamu na mpangilio lazima uwepo hatuwezi kuwa hivyo kwa kuridhisha wachache

Hakuna sehemu duniani isiyokuwa na nidhamu na kufanya mambo hovyo hovyo kama sisi
 
safi sana.
kimsingi Karia koo kwa sasa inapaswa ihamie Maeneo ya MBEZI MWISHO, STENDI YA MAGUFULI.
JIJI la DSR ljnapaswa lipanuke.
tubadilike, wataalamu wa mipango miji wapo lkn hawataki kutumia taaluma zao vyema.
Huko Mbezi kwenyewe Machinga wamejaa huo mji mipango miji ishakua mibovu
 
Ni uamzi mzuri nami nauunga mkono maana hawa wamachinga wametapakaa kila pahali palipo na uwazi utakuta wamepanga bidhaa zao hadi imekuwa kero
 
Naona biashara ya tozo inaenda kuathirika kwani machinga na mama lishe ndo watumiaji wakubwa wa mitandao ya kutuma vijisenti.....au siyo?
 
Naona chadema washapata fursa nyingine ya kisiasa. Sasa watakuwa upande wa wamachinga kwa kujifanya wanawapigania na kusahau kumpigania mwenyekiti. Hapa ndio CCM inafanikiwaga kutawala akili za hawa jamaa.
 
Back
Top Bottom