RC Makalla: Machinga wote Dar walio katika hifadhi ya barabara, Wataondolewa na vibanda vyao kuanzia Septemba 13, 2021

Narudia tena wewe unalipwa hapo hujui maana ya machinga.... machinga hawawezi kaa mbali ya wateja... wanatakiwa kuwa mjini... hayo maeneo unayo yataja ni yapi? machinga complex? Tusubiri afanikiwe nikuletee zawadi...... uwezi kuwatoa machinga mjini
Nimekuelewa bwashee!
 
Duuh!,Hii ishu ya wamachinga kufunga barabara karibia zote za Dar kwa vibanda we unaona minor sana.Alafu kwenye major issues zako umeorodhesha na uchafu 😀
huyu mkuu wa mkoa anafanya cheap politics haya ni mambo minor sana, jiji hili lina changamoto kubwa na nyingi kuliko mambo ya wamachinga mfano miundo mbinu mibovu, wanafunzi kukaa chini, uchafu, hospitali hamna tiba ya uhak
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh Makalla amesema zoezi la kulirejesha jiji pamoja na mkoa mzima katika hadhi yake litaanza ambapo Wamachinga wanaofanya biashara zao barabarani na katika hifadhi za barabara wataondolewa.

Makalla amesema wamachinga wote wanapaswa kufanya biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa na siyo vinginevyo.

Chanzo: Clouds tv

cc: Mmawia
Naomba sana sana anza na mbagala, tegeta. Na hasa maeneo ya bunju B, maana sisi madereva wa mabasi ya kaskazini ikifika asubuhi na jioni tunapoteza mda mwingi pale
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh Makalla amesema zoezi la kulirejesha jiji pamoja na mkoa mzima katika hadhi yake litaanza ambapo Wamachinga wanaofanya biashara zao barabarani na katika hifadhi za barabara wataondolewa.

Makalla amesema wamachinga wote wanapaswa kufanya biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa na siyo vinginevyo.

Chanzo: Clouds tv

cc: Mmawia

======

RC MAKALLA: MARUFUKU MACHINGA KUFANYA BIASHARA KWENYE NJIA ZA WATEMBEA KWA MIGUU.

- Asema agizo hilo ni kwa Wafanyabiashara Mkoa mzima.

- Amtaka DC Ilala na Uongozi wa Machinga kuweka utaratibu mzuri kuwapanga Machinga Kariakoo.

- Awapo mbinu ya kufunga baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya Biashara.

- Wamachinga wakiri kuingilia maeneo ya watembea kwa miguu na kuahidi kuhama.

- Aeleza dhamira yake ya kuboresha mandhari ya Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepiga marufuku ufanyaji wa Biashara Kwenye maeneo hifadhi ya barabara zote za Mkoa huo baada ya utaratibu huo kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani na ongezeko la ajali.

RC Makalla
ametoa maelekezo hayo alipotembelea Soko la Kariakoo na kujionea Kero ya Ufanyaji biashara holela Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.

Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kufanya kikao na Wafanyabiashara hao Jumatatu ya *September 13 na kuainisha maeneo ya kuwapeleka wote waliovamia hifadhi ya Barabara.

Aidha RC Makalla amewaelekeza Kuangalia utaratibu mzuri wa kufunga na kufungua baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya biashara Kutokana na ufinyu wa maeneo ili Waweze kupata riziki.

Hata hivyo RC Makalla amesema kwa tathimini aliyofanya amebaini Hali ya Ufanyaji biashara holela Dar es salaam ipo kwa kiwango kikubwa na kuwanyima watembea miguu haki zao za msingi.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Manispaa zote za Mkoa huo kuweka Vibao vya kuzuia biashara Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.
Makalla shikilia hapo hapo usiyumbe
 
Kuna haja ya kubuni masoko ya Wamachinga kwa baadhi ya barabara kuliko kujenga masoko makubwa yanayoishia kukosa wajasiriamali.
Naunga mkono hoja kuwe na masoko yenye kukidhi biashara za namna hiyo mabanda ya kisasa lakini simple na miundombinu rafiki yenye kuweza kuvutia biashara na wateja lakini kariakoo yote mpaka huku posta au mwenge hizi biashara za hovyo hapana haya masoko ya wamachinga yanaweza kujengwa Temeke, Kindondoni na Ilala moja moja tu kukidhi matakwa ya maeneo hayo ila katikati miji ni biashara za kisasa na zenye kulipiwa kodi stahiki mji uwe wa kisasa na hili lisiwe Dar tu mikoa yote Tanzania. lazima tubadilike
 
Wamachinga kukaa katikati ya miji haileti picha kiustaarabu. Inaleta ugumu pia kuendeleza swala la usafi wa miji na kutoa nafasi kwa watumiaji wa barabara hasa watembea kwa miguu. Lakini serikali ilisahau kwamba hawa jamaa hawalipi kodi ndo maana tukarudishana kwenye miamala.
Swala la Chadema kuwatetea machinga ni kurukia hoja ila pia CCM iliwalea hadi kukusanya elfu 20 kila kichwa kwa hiyo wasitumie nguvu kupitiliza wakati wa zoezi.
 
Ngoja tuone utekelezaji. Ila kwa sisi wafanyabiashara tukio hili la kuondoa machinga likifanikiwa si linaweza kupandisha Kodi za frem kariakoo?
 
Ni Jambo jema ila angalizo tu, asije akawa anadhani anawaondoa wamachinga kumbe anajiondoa yeye ofcn!!

Kwa sabab kabla ya kuwaambia watu waliopo waondoke lazima afikirie wanaenda wap, ikiwa Hana plan wapi wanaenda maana yake anawaambia wajitafutie wenyewe, je yupo tayar na matokeo ya kujitafutia wenyewe??

Naona vibaka na wezi wanaongezeka zaidi, dar itakuja kuwa mji wa hatari kuishi kuliko eneo jingine tz...
Kupanga ni kuchagua, kama kweli ipo dhamira ya dhati inawezekana kabisa, shida ni siasa na kinyago alichotengeneza mtu kinamtisha mwenyewe
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh Makalla amesema zoezi la kulirejesha jiji pamoja na mkoa mzima katika hadhi yake litaanza ambapo Wamachinga wanaofanya biashara zao barabarani na katika hifadhi za barabara wataondolewa.
Kulirejesha? CCM mna fiksi sana aiseee. Wameshapigia kura sasa mnawapa wanachostahili
 
Wawaachie mitaa kadhaa Kama Congo etc..wasiwaondokoe kabisa kumbukeni Hawa vijana wanatafuta maisha na wengine wana familia jamani..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh Makalla amesema zoezi la kulirejesha jiji pamoja na mkoa mzima katika hadhi yake litaanza ambapo Wamachinga wanaofanya biashara zao barabarani na katika hifadhi za barabara wataondolewa.

Makalla amesema wamachinga wote wanapaswa kufanya biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa na siyo vinginevyo.

Chanzo: Clouds tv

cc: Mmawia

======

RC MAKALLA: MARUFUKU MACHINGA KUFANYA BIASHARA KWENYE NJIA ZA WATEMBEA KWA MIGUU.

- Asema agizo hilo ni kwa Wafanyabiashara Mkoa mzima.

- Amtaka DC Ilala na Uongozi wa Machinga kuweka utaratibu mzuri kuwapanga Machinga Kariakoo.

- Awapo mbinu ya kufunga baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya Biashara.

- Wamachinga wakiri kuingilia maeneo ya watembea kwa miguu na kuahidi kuhama.

- Aeleza dhamira yake ya kuboresha mandhari ya Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepiga marufuku ufanyaji wa Biashara Kwenye maeneo hifadhi ya barabara zote za Mkoa huo baada ya utaratibu huo kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani na ongezeko la ajali.

RC Makalla
ametoa maelekezo hayo alipotembelea Soko la Kariakoo na kujionea Kero ya Ufanyaji biashara holela Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.

Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kufanya kikao na Wafanyabiashara hao Jumatatu ya *September 13 na kuainisha maeneo ya kuwapeleka wote waliovamia hifadhi ya Barabara.

Aidha RC Makalla amewaelekeza Kuangalia utaratibu mzuri wa kufunga na kufungua baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya biashara Kutokana na ufinyu wa maeneo ili Waweze kupata riziki.

Hata hivyo RC Makalla amesema kwa tathimini aliyofanya amebaini Hali ya Ufanyaji biashara holela Dar es salaam ipo kwa kiwango kikubwa na kuwanyima watembea miguu haki zao za msingi.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Manispaa zote za Mkoa huo kuweka Vibao vya kuzuia biashara Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.
View attachment 1930496View attachment 1930497View attachment 1930498

View attachment 1930499

View attachment 1930500
Yuko sahihi.....

Awamu mpya....UKWELI MPYA....

Inapotokea ajali huwakumba WAFANYABIASHARA na WATEJA WAO....hapo tutalaumiana ?!!!!!

Road Reserves hazikuwekwa kwa ajili ya kufanya biashara......

UKWELI UTUWEKE HURU

#SiempreJMT
 
Back
Top Bottom