RC Makalla: Nitaongea na Wadau ili daladala zinazoishia Kariakoo ziwe zinaishia Machinga Complex kesho ni mwisho wa kuhama!

RC Makalla: Nitaongea na Wadau ili daladala zinazoishia Kariakoo ziwe zinaishia Machinga Complex kesho ni mwisho wa kuhama!

Hapo ni kusababisha vurugu na usumbufu usio na sababu kwa raia.. fikiria foleni ya kutoka hapo gerezani mpaka machinga complex.. hizo daladala ziachwe ziendelee kupaki hapo zilipo ili kusaidia raia.

Kumbuka kuna kipindi daladala za mbagala zilikuwa zinafika machinga complex, baada ya kituo kufungwa ili mwendokasi wakarabati, ikawa ni.mateso na kero kubwa kwa raia sababu ya umbali na foleni ya magari mpaka kufika hapo kituoni..
 
Kabla hajazipeleka atanue kwanza barabara na ajenge kituo.

Hizo za kigambonj tu zishajaza eneo na kusababisha msongamano. Tatizo la machinga komplex hakuna nafasi ya kufanyia biashara. Mitaa yote inayozunguka yale majengo kuna vituo vya daladala na kutoka maeneo karibu yote ya Dar
Kwani hajui kama wafanyabiashara walishindwa kupanga kwenye yale majengo sababu baada ya kukamilika vigogo wenzie walikodi kutoka nssf wakaanza kuwachaji wapangaji kwa pesa nyingi?

Ndio kama inavyoenda kutokea kwenye masoko na stendi alizoacha magufuli. Ilianzia soko la morogoro lakini uzuri Jiwe alikuwepo akawaambia wazitapike hela walizochukua kwa wafanyabiashara tena aliwataja kwa majina.
 
Hivi hao Machinga wana lipi la maana hadi wawe kama wanabembelezwa wakati raia walipa kodi hawana upendeleo wowote kama hao wakepa kodi
 
Unalijua joto la Dar na msongamano wa watu kuanzia Machinga Complex Hadi Kariakoo?
Mbona wa kigamboni, chanika , machimbo , kisarawe ,viwandani na kitunda wanashukia machinga complex , sema kile kituo ni kidogo tu , ila sio mbali kama unavyoongea ww
 
Kuna daladala inayoishia Kariakoo?
Ndio

Daladala za

Tegeta-Kariakoo (shimon)
Mabibo-kariakoo (jiran na shimon)
Makumbusho-kariakoo zinazopitia manseze , zinaishia msimbazi
Kawe-k/koo
 
Mbona wa kigamboni, chanika , machimbo , kisarawe ,viwandani na kitunda wanashukia machinga complex , sema kile kituo ni kidogo tu , ila sio mbali kama unavyoongea ww
Hao watu hua wanalazimika kuja karume kupanda gari zinazoenda Muhimbili kwa wanao elekea msimbazi au Mnazi mmoja kwa wanao elekea congo ,ndio zinazo waingiza k/koo
 
Safi sana Makalla ,Kuanzia tar 31 na 01 ni kukamata wabishi wote na kuwapiga faini laki3 na kifungo cha miaka mi3 ili iwe fundisho kwa wasiotaka kutii sheria bila shuruti.
 
Chapa kazi RC, lazima miji yetu iwe na utaratibu, wanaokupinga katika hili ni wanafiki
 
Huyu jamaa nimetokea kumuelewa sana. Wengi watambeza ila anachokifanya makonda na wengine walishindwa.
 
Kwann
Yanapaki barabarani vile siyo vituo bwashee.
Miaka yote daladala mnaziangaliaga tu kupaki vituo visivyo rasmi? Na hata la makala lengo sio kutoa vituo vya daladala kwasaab hakuna vituo rasmi, lengo ni kusogeza daladala kwaajil ya machinga 😂😂😂😂.
 
Back
Top Bottom