RC Makalla: Nitaongea na Wadau ili daladala zinazoishia Kariakoo ziwe zinaishia Machinga Complex kesho ni mwisho wa kuhama!

RC Makalla: Nitaongea na Wadau ili daladala zinazoishia Kariakoo ziwe zinaishia Machinga Complex kesho ni mwisho wa kuhama!

Hii ni dalili ya zoezi kukwama.
Machinga complex sio soko na haliwezi kuwa solution ya tatizo.
Huwezi kutatua problem kwa kuihamisha hamisha au kwa kubuni uozo mwingine. Hapa namaanisha kupeleka daladala 'machcomp' ni kuongeza traffic jams eneo hilo.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Safi sana Makalla ,Kuanzia tar 31 na 01 ni kukamata wabishi wote na kuwapiga faini laki3 na kifungo cha miaka mi3 ili iwe fundisho kwa wasiotaka kutii sheria bila shuruti.
Eenhee! Mnataka kila mtu awe shoeshiner mjini!? Au ndio yale ya kupunguza msongamano magerezani kwa kuondoa wezi wa kuku na kujaza machinga!? Huyo anayejiita makala hata mbeya alitusumbua sana sisi machinga. Machinga wa dsm tafuteni namna ya kupambana naye, kwa kuwa akili hana huyo jamaa.
 
Yaani Nia yangu ninkwenda Kariakoo, wewe unipeleke Machinga complex. Huyu ni Makala au Sakala?

Ajifunze kuheshimu haki za raia, sio kutupelekesha kiboya atakavyo
Machinga complex hakuna bus terminal ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa.

Labda machinga complex iwe ni via lazima daladala zipite hapo.

Tuna tatizo la kuwa na viongozi licha ya kuwa na exposure sijui akili zao huwa zinakuwa wapi?

Kwa mtu aliyefika Cape town South Africa ile Tax terminal yao ni ya ghorofa, kwakuwa mji wetu umejengwa bila plan hapo kariakoo bado palikuwa na uwezo wa kujenga daladala terminal ya ghorofani paleale gerezani mwendokasi, chini wabaki BRT na juu wapewe daladala.
 
Comment bila shaka unaiandika ukiwa Mogadishu wewe si bure
Vile actually sio vituo ni barabara za kupitisha magari ya mizigo kuingia sokoni. Vingekuwa vituo vingekuwa na nafasi sasa zile ni njia za barabara tu. Kitendo cha kupaki magari pale kinasababisha foleni ya magari barabara nyingine hasa road ya polisi pale. Napo kusingekuwa na kituo wangekuwa wanapaki hapo
 
Mkumbushe kuhusu mabasi yote ya mikoa kuishia Magufuli Bus Terminal, aliishia wapi?
 
Machinga complex hakuna bus terminal ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa.

Labda machinga complex iwe ni via lazima daladala zipite hapo.

Tuna tatizo la kuwa na viongozi licha ya kuwa na exposure sijui akili zao huwa zinakuwa wapi?

Kwa mtu aliyefika Cape town South Africa ile Tax terminal yao ni ya ghorofa, kwakuwa mji wetu umejengwa bila plan hapo kariakoo bado palikuwa na uwezo wa kujenga daladala terminal ya ghorofani paleale gerezani mwendokasi, chini wabaki BRT na juu wapewe daladala.
Sasa exposure ya Cape Town itamsaidia nini Makala hapa. Kwamba ajenge kituo cha daladala cha ghorofa, yeye hana bajeti hiyo na wala sio kazi yake. Anachokifanya ni kutumia miundombinu iliyopo kwa kila kinachowezekana. Kwanza hii nchi kila mtu lawama, ufanye lawama na usifanye lawama.

Huwezi kuwa kamanda jeshini ukapewa AK-47 ukalalamika unataka AR-15 kama NATO. Kwanza mji huu una miundombinu mibovu na haujapangwa, kila mabadiliko yataleta effects
 
Wahamisheni jumla sio mnasubiria wakati wa uchaguzi

Mbezi Beach huku bado kwenye residential plots bado wamejaa!! Makalla usipowaondoa hao utakuwa umelikoroga na hapo lazima awajibike diwani wa Kawe na wenyeviti wa mitaa husika kwani wao ni wadau wa hizi biashara ndio maana wana hujumu zoezi!.

Sasa Makalla usikae ofisini na kuitisha press conference tu, njo mtaani uone live!
 
Hivi anaijua vizuri machinga complex kiasi cha kutoa amri ya daladala ziende pale? lile eneo daladala zikirundika ataiweza hiyo foleni kuanzia msimbazi huku mpaka chango'mbe kule.... Viongozi wetu wajifunze kutumia numbers kufanya maamuzi yao..
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema wamachinga waliogoma kuhama wataondolewa kwa lazima na vibanda vyao kuhamishwa. Kesho 30/10/2021 ndio siku ya mwisho kwa wamachinga wite kuhamia maeneo rasmi.

Kadhalika Makalla amesema ataongea na wadau wa Usafiri ili daladala zote zinazoishia Kariakoo ziwe zinaishia Machinga Complex ili kuchangamsha biashara katika eneo hilo.

Source: ITV habari
Watu waumie ili kuchangamsha machinga? Kweli çcm wote ni akili ndogo
 
Kuna daladala inayoishia Kariakoo?
Makala analeta siasa

Kuna miundo mbinu gani pale Machinga complex ya kutosheleza daladala zinazoishia gerezani au Sokoni kariakoo?

Yote hii anajaribu kuonyesha kuwa wamewatengea wamachinga maeneo. Hili siyo kweli!

Lakini pia vipi kuhusu wamachinga wa Kigamboni, Mwenge etc hao mmewatengea maeneo gani?
 
Kama wanahitaji machinga eneo lile basi waanze kuliboresha kwa maana ya space na kila kitu..

Uwanja wa mpira Karume uhame na pale wajengewe flats kadhaa ndefu wakae hapo.
Yale makaburi ya waislam upande wa pili, yahame iwekwe stand ya daladala ya kisasa..na eneo lile litanuliwe kidogo mpaka pale kqenye flyover inayojengwa chang'ombe..

Pale soko la mchikichini karibu na Tbl napo lihame na wale warudi machinga complex kwa wenzao baada ya maboresho...lile eneo la soko itengenezwe parking kuuubwa ya gari ndogo kwa ajili ya wateja wa machinga na wanaoingia kariakoo.. ( parking iwe ya ghorofa kadhaa)....

Jiji la Dar es salaam linahitaji akili sasa kulipanga upya na kuacha mipango ya zimamoto na siasa zisizo na maana otherwise jiji litakuwa kila siku muda wote limesimama tu..
 
Viongozi wajifunze sasa kutumia numbers kwenye maamuzi yao sio kusimama tu na kutoa maamuzi kutoka vichwani...

Maana yake ni nini: kila jambo kabla ya kuamua lazima ukusanye taarifa, data, takwimu na uresearch jambo lenyewe, utengeneze solution based on data collected..

Issue ya wamachinga: mlipaswa kwanza mfanye sensa ya machinga wote kwa mkoa wa Dar es salaam na maeneo yao waliyokaa, muandae centers za kuwahamishia kulingana na maeneo waliyopo, muweke miundombinu ya hizo centers, muanze kuwapanga kwa kuwakabidhi maeneo yao kila mmoja baada ya hapo muwape siku za kuhama....hayo yote yanakwenda sambamba na routes za daladala kufika maeneo hayo, matangazo redioni juu ya biashara kuhamia maeneo hayo na kuyapa promo hata kwa miezi mitatu..
 
Back
Top Bottom