RC Makalla umeyamaliza ya wamachinga, lakini vipi kuhusu Mbuzi wazururaji wa Dar?

RC Makalla umeyamaliza ya wamachinga, lakini vipi kuhusu Mbuzi wazururaji wa Dar?

ngongoti2000

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2017
Posts
2,236
Reaction score
2,142
Wote tumeona kwamba mkuu wa mkoa RC Makalla na serikali kwa ujumla wamewakomalia wamachinga waondoke maeneo ambayo hawatakiwi kisheria.

Hiyo sawa; lakini kuna suala hili la mbuzi wa Dar ambao wanajichunga wenyewe Magomeni, Mbagala, Mbezi, Shekilango nk ambao nao wanaleta uchafuzi wa mazingira na sintofahamu ukizingatia wanajichunga wenyewe pamoja na kuwa na uwezo wa kufuata sheria za usalama barabarani kama trafic lights, zebra nk.

Lakini, hatujawahi sikia serikali ikitoa tamko juu ya hawa jamaa na sasa wanazidi kuongezeka mjini Dar. Labda RC Makalla angetuambia kwanini na hii mifugo isifukuzwe mitaani ili ikakae maeneo yanayowahusu kama walivyofanyiwa wamachinga?
 
Tatizo la mbuzi wengi wa Dar, sio mbuzi kama mbuzi.

Wale ni binadamu ndio maana wanavuka barabara kwenye zebra, wanajua kufuata mataa ya kuongozea magari, wanaenda makaburini kuwaombea marehemu, wanakula nyama na mikate nk nk nk

Kama huamini siku moja jifanye kama zuzu umkamate mmoja afu umcharaze bakora. Ila usije ukasema sijakuonya
 
Ni moja ya vivutio kwa huko Dar es Salaam . Maana Dar es Salaam simba[emoji881] wenu eti ni Diamond Platnumz, tembo[emoji208] ni Harmonize, chui[emoji249] ni Van boy, Mamba[emoji246] ni Dudubaya.[emoji1787][emoji1787][emoji848][emoji848]
 
Wimbi la ujambazi limerudi Tena

Kwetu uswazi Kawe,matukio ya nyumba,maduka kuvunjwa sasa yameongezeka

Jamaa wanakuja na gari,wanavunja,wanakusafisha kabisa kila kitu

Hapa namkumbuka Afande Zelote Stephen,aliisafisha Dodoma,majizi yote,yalimalizwa kwa mbinu takatifu

"Wameuwawa wakati wa kurushiana risasi na polisi"
 
Tatizo la mbuzi wengi wa Dar, sio mbuzi kama mbuzi.

Wale ni binadamu... ndio maana wanavuka barabara kwenye zebra, wanajua kufuata mataa ya kuongozea magari, wanaenda makaburini kuwaombea marehemu, wanakula nyama na mikate nk nk nk...

Kama huamini siku moja jifanye kama zuzu umkamate mmoja afu umcharaze bakora.... Ila usije ukasema sijakuonya
Halafu hao mbuzi Wana hisia ka binadamu kabisa Kuna moja niliona katoto kamegongwa na gari mama mbuzi akawa analia ka binadamu kabisa, huwa najiuliza Hawa mbuzi wanaishi wapi?
 
Back
Top Bottom