RC Makalla umeyamaliza ya wamachinga, lakini vipi kuhusu Mbuzi wazururaji wa Dar?

Kuna mbuzi kawe wanavuka barabara kwenye zebra crossing [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Halafu hao mbuzi Wana hisia ka binadamu kabisa Kuna moja niliona katoto kamegongwa na gari mama mbuzi akawa analia ka binadamu kabisa, huwa najiuliza Hawa mbuzi wanaishi wapi?
Huyo dereva ana bahati, wengine ukiwagonga maiti inakuwa ya binadamu...
 
Bongo ukitaka kulinda mali yako ihusianishe na uchawi.
 
Namuonya awaguse Mbuzi wote ila siyo wa Yule Mpemba wa Mbezi Beach Makonde kwani anaweza akatangulia mapema Mochwari kujiandaa na Safari yake ya Milele Makaburini Kinondoni.
Wale wa mpemba ni majirani..kuna siku niko vyombo narudi home mida ya saa 9 usiku nikawakuta wamelala katikati ya barabara ile ya vumbi njia ya kwenda kwangu...nikasogea karibu na kuwapigia honi wananiangalia tu ..pombe zikanituma nipite juu yao ni katoka nduki na gari nikaenda kupaki...kesho yake nikarudi pale kwa miguu kinyemela hakuna hata damu wala aliyekufa
 
Nalikuwa kinondoni pale mtaa wa bwawani kule karbu na club moja ya sanaa.
Nikiwa na miaka nane naliona kitu cha ajabu sana kuhusu hao mbuzi tulikuwa watundu mpk tukafika kwa msikiti uliopo karbu na hapo tukafungua koki na kuacha maji na kuanza kuchezea kumbe kuna shekh anatuzoom mahala tukamaliza sasa kweye njia kuna mfereji na kama kadaraja cha mbao kama nne hivi me nikiwa mbele na wezangu nyuma tunakarbia kupita mferej tutoke eneo la msikit lakin cha ajabu alitokea mbuzi akakaa katikat ya kidaraja😂 na kama amedhamilia kutotoka pale mana tulirusha mawe wapi kugeuka nyuma nakutana na shekh kwa ishara anasema njoooni huku 😂

Ninachokumbuka nalifika home nmelowa matope ya mtaron kwa mbio zile changanya na yule mbuzi niliota ndoto mbaya sana usiku.
 
Kwahiyo huyo mbuzi alikuwa ndio shekh mwenyewe?
 
Acheze nao aone
 
Halafu hao mbuzi Wana hisia ka binadamu kabisa Kuna moja niliona katoto kamegongwa na gari mama mbuzi akawa analia ka binadamu kabisa, huwa najiuliza Hawa mbuzi wanaishi wapi?
Misukule hiyo bro shauri yako
 
Jifunzeni kujua tabia za wanyama na viumbe wengine ili muondokane na Imani potofu, mnakaa mjini hamjawahi kuwa wachungaji wala wafugaji wa mifugo ndiyo maana mnachangaikia kwa mawazo bila utambuzi.
 
Kuna Wahuni hapo hapo Makonde Kituoni baada ya Mbuzi wake Mmoja Kugongwa na Gari wakamkimbilia kumchukua na kwenda Kumchinja kilichowatokea Wote walikuwa Wakiharisha hovyo barabarani tena penye Watu wengi ila wakiwa peke yao Hawaharishi mpaka waliposhauriwa kwenda Kumuomba Radhi na Wakasamehewa.

Yule aliyegonga Mbuzi wake na Kumuua kisha akatomokea alienda kupata Ajali mbaya Kawe Bondeni na mpaka sasa ni Mwendawazimu.
 
Watu 8 waliomsumbua mpaka hivi sasa ni Marehemu na Vifo vyao ni vya ajabu ajabu tu. Huyo Mpemba hana Masihara Ndugu sitanii.
Hakuna uchawi, una hofu na umejengwa kwa Imani potofu kutokana na mazingira uliyo ishi na watu waliokuzunguka toka zamani
 
Watu 8 waliomsumbua mpaka hivi sasa ni Marehemu na Vifo vyao ni vya ajabu ajabu tu. Huyo Mpemba hana Masihara Ndugu sitanii.
Acha Imani potofu, hakuna cha mpemba wala nini, ni ujinga tu unawasumbua wengi kuamini uchawi wakati haupo, jifunze tabia za wanadamu na viumbe wengine, halafu jifunze jinsi mfumo wa dunia unavyo fanya kazi ili uondokane na Imani potofu
 
Jaribu kujifunza somo la saikolojia ili uwasaidie wengine kuondokana na Imani potofu
 
Ok hili kalisikia atalifanyia kazi

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ona wanadamu jinsi wallivyo wachoyo na wabaguzi. Wanataka waishi wenyewe sehemu nzuri tu kama vile dunia imeumbwa kwa sababu yao. Wakati binadamu ni mnyama kama wanyama wengine. Sisi wanadamu ndugu yetu wa karibu kabisa ni Sokwe mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…