Tetesi: RC Makonda ajimilikisha ekari 22.3 mkoani Dodoma, sawa na ukubwa wa viwanja 15 vya Soka

Tetesi: RC Makonda ajimilikisha ekari 22.3 mkoani Dodoma, sawa na ukubwa wa viwanja 15 vya Soka

Swala hapa liwe kama alifuata taratibu katika kupata hiyo ardhi;

Sheria inaruhusu mtanzania yeyote kumiliki ardhi.
Ishu siyo taratibu ya kupata viwanja hivyo, embu kapitie vizuri sheria ya maadili ya viongozi wa umma ndio uje ukomenti.
Maana naona umekomenti utumbo tu, huwezi kumfananisha kiongozi wa umma na mtanzania yeyote tu wa kawaida. Pumbafu mkubwa we.
 
"Tunafungua mahakama za mafisadi"! Kumbe mafisadi yanalelewa ndani ya nyumba kabisa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni pesa nyingi kwa mfanyakazi wa serikali, yatubidi kwanza tupate maelezo ya kina jinsi ya upatikaji wa pesa ya viwanja.Je hivi ni kweli ni Makonda mkuu wa mkoa au mwingine?Kama ni yule Mh.Makonda atakuwa na swala la kujibu.
Je miiko ya uongozi ilizingatiwa?
Kumbe kazi ya madaraka kwa kupitia mkono wa siasa ni mtaji wa kula bila kunawa.
 
Nittakuwa wa mwisho kukubaliana na wewe kuhusu Makonda na Rais JPM kushirikiana kwenye biashara/ufisadi, maana kama ingelikuwa hivyo basi JPM angempa Makonda pesa ya kukombolea container zake, sakata lisingefika hapo lilipofika.

Ila watanzania wengi wanasubiri kuona kiwango cha uwadilifu wa Rais JPM na Mh. Makonda kwenye sakata hili la wazi la makontena, kwakuwa msimamo wa Rais kwa viongozi waliotenda makosa kama aliyotenda Makonda unafahamika. Watanzania wanasubiri movie itaishiaje.
Kabisa rais wa nchi atoe billion 20 kukombolea container wakati akisema tu Mpango anatekeleza
 
Halipii au analipia?
Alienda kanisani la cheti fake, akaenda la "makontena ya ofisi za walimu" sasa atakwenda kwa hili la viwanja ila bado haijulikani atakwenda kanisa gani labda kanisa la Ufufuo na Uzima maana la cheti cha 0 alikwenda Lutherani na la makontena akaenda Anglikani
 
Kweli bashite ni mtoto wa damu wa mfalme.
Screenshot_2018-08-31-15-43-25.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alienda kanisani la cheti fake, akaenda la "makontena ya ofisi za walimu" sasa atakwenda kwa hili la viwanja ila bado haijulikani atakwenda kanisa gani labda kanisa la Ufufuo na Uzima maana la cheti cha 0 alikwenda Lutherani na la makontena akaenda Anglikani
Halipii au analipia?
 
Sasa ukiangalia bei za hivyo viwanja mbona hata mfanyakazi mdogo tuu ananunua? Kwa kuna mtu alizuiliwa kununua? Mshahara wa RC ni shs Ngapi na ameanza kazi lini mpaka ashindwe vitu vidogo hivi? Tuache roho za kimasikini

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu acha utani million 400 uzipate kwenye mshahar tu haiwezekani mshahar hata hauzidi 20 mill

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni pesa nyingi kwa mfanyakazi wa serikali, yatubidi kwanza tupate maelezo ya kina jinsi ya upatikaji wa pesa ya viwanja.Je hivi ni kweli ni Makonda mkuu wa mkoa au mwingine?Kama ni yule Mh.Makonda atakuwa na swala la kujibu.
Je miiko ya uongozi ilizingatiwa?
Kumbe kazi ya madaraka kwa kupitia mkono wa siasa ni mtaji wa kula bila kunawa.
Sasa unashangaaje kua na kiwanja ukubwa huo kama makontena tu kodi yae ni billions je hayo makontena thamani yake sh ngp

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The only honourable advice to Paul Makonda, assuming what has been exposed here is true and correct, and that the evidence so tendered hereat is not a doctored document, just seek a ceremonious exit. Resign!
Good advice, though you could have used swahili for others to understand specifically Bashite and his Co
 
Ishu siyo taratibu ya kupata viwanja hivyo, embu kapitie vizuri sheria ya maadili ya viongozi wa umma ndio uje ukomenti.
Maana naona umekomenti utumbo tu, huwezi kumfananisha kiongozi wa umma na mtanzania yeyote tu wa kawaida. Pumbafu mkubwa we.
Haya ndio matatizo ya kurukia comment na kutoa majibu bila kuzielewa.
 
Dhambi tuzifanyazo kwa siri hutuumbua baadaye. Hakuna namna watubu tu.
 


Ansbert Ngurumo30th August 20180 Comments



PAUL Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, amemvua nguo Rais John Magufuli katika vita ya ufisadi.

Siri zake zimeanza kuvuja na imeanza kudhihirika kuwa hasira zote na bidii ya kunyamazisha bunge, wapinzani, wakosoaji, na vyombo vya habari ni mbinu ya kuwezesha wajanja kuvuna wasikopanda na kujilimbikizia mali kwa kutumia ofisi ya umma.

Shaka ya wananchi juu ya sababu za rais kudekeza na kumpendelea Makonda, ambaye kwa kutambua kuwa ni kipenzi cha Rais Magufuli amekuwa anatumia cheo chake na ukaribu wake na rais kupora mali na kujimbilikizia mali zisizo na maelezo ya kutosha, imeanza kupata majibu.

Mali nyingi alizonazo hazijulikani kwa tume ya maadili ya viongozi, na haziendani na kipato chake.

SAUTI KUBWA inaanza na viwanja vya ardhi sita vikubwa vinavyomilikiwa na Makonda katika mkoa wa Dodoma pekee.

Viwanja hivi sita anavyomiliki Dodoma vipo katika eneo linalojulikana kama Iyumbu New Town Centre, katika block R na S, vikiwa na ukubwa kuanzia mita za mraba kati ya 5,000 na 40,000 kwa kila kiwanja.

SAUTI KUBWA inasema pasipo shaka kuwa katika ujumla wake, viwanja vyote sita vya Makonda vinachukua eneo la mita za mraba 92,341.

Eneo hilo ni sawa na hekta 9.23 au ekari 22.3 za ardhi, ambazo ni sawa na ukubwa wa viwanja 15 vya mpira wa miguu (soka). Ni sawa na kijiji kidogo.

Viwanja hivyo, ambavyo vielelezo vyake vimeambatanishwa hapa, havijulikani kwa tume ya maadili ya viongozi.

Katika block R kuna viwanja vinne namba 1, 28, 32 na 33. Kiwanja namba 1 kina mita za mraba 40,973, na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 2,581,300.



Kiwanja namba 28 kina ukubwa wa mita za mraba 18,210 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 1,147,250.



Kiwanja namba 32 kina ukubwa wa mita za mraba 13,080 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 824,050.



Kiwanja namba 33 kina ukubwa wa mita za mraba 9,932 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 625,750.



Katika block S, Makonda anamiliki viwanja viwili, namba 17 na 18.



Kiwanja namba 17 kina ukubwa wa mita za mraba 5051, na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 318,250. Kiwanja namba 18 kina ukubwa wa mita za mraba 5,095, na kinalipiwa Sh. 321,000.



Kwa mujibu wa vielelezo ambavyo SAUTI KUBWA inavyo, hadi tarehe 21 Mei 2018, viwanja hivyo vilikuwa vimehakikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma. Ingawa mmiliki ni Makonda, vyote vinaonekana vimesajiliwa kwa ajili ya taasisi.

Suala la viwanja vya Makonda linaibuka wakati kuna sintofahamu juu ya makontena 20 bandarini ambayo Makonda anagoma kuyalipia kodi, huku Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiamuru yapigwe mnada kuokoa kodi ya serikali.

Makontena hayo, ambayo awali Makonda aliyakana, yameandikwa jina lake, naye anadai kwamba vifaa vilivyomo ni kwa ajili ya shule ambazo hata hivyo hazijulikani.

Hata huko Marekani anakodai vilichangwa, kuna utata juu ya watu wanaodaiwa walivichanga. Hapo hapo kumezuka hoja kwamba ndani ya makontena ya makonda kuna vifaa vingi zaidi ya samani za shule, na kwamba samani hizo zimetumika kufunika “mzigo” halisi.

Tayari kuna maelezo kuwa Makonda aliingiza makontena hayo kwa ajili ya miradi yake binafsi kwa kutumia ofisi ya serikali. Ubabe aliotumia kushambulia wanaohoji kuhusu makontena hayo, huku akitumia jina la rais ni baadhi ya mambo yanayoleta hisia kwamba kati ya Makonda na rais kuna biashara ambayo wananchi hawajaijua.

Baadhi ya wachabuzi wa siasa wameiambia SAUTI KUBWA kuwa uswahiba uliopitiliza kati ya Makonda na Rais Magufuli una harufu ya ufisadi.

Wanasema hata mabavu ya rais na Makonda kutumia vyombo vya dola dhidi ya raia wanaokosoa utawala wake ni mazalia ya ufisadi mkubwa utakaoibuka taratibu, hasa baada ya muda wa Rais Magufuli kuondoka madarakani.

Chanzo kimoja kimeiambia SAUTI KUBWA: “Usidhani Magufuli hajui uchafu wa Makonda. Anamlinda kwa sababu wana mradi wao. Makonda ni mtoto wa baba, ni mmoja wa viongozi wapendwa wanaojua dili chafu za baba; ndiyo sababu ya ushirika wao kunyamazisha wakosoaji.”

“Kama Watanzania walidhani Magufuli ni mwadilifu kama anavyojitapa mbele yao, walikosea sana; huyu anajulikana kwani katika wizara zote alikopitia, kulikuwa na kelele na mbwembwe nyingi za takwimu, lakini ufisadi ulitamalaki. Ataacha leo kwa vile yupo Ikulu?,” kimehoji chanzo kingine, na kuongeza:

“Hawa jamaa wana majengo na viwanja nchi nzima. Wanajimilikisha nchi utadhani dunia inaisha kesho au wanamkomoa mtu. Si uliona hata majuzi rais akiwa Mwanza, baada ya kumtembelea dada yake hospitalini, alisimama pale Nyerere Road kuzindua kwa siri jengo lake linaloitwa Nyerere Plaza, akajidai anazungumza na wananchi. Ni Mali yake ile.

“Tutajua mengi sana kadiri muda unavyokwenda, na watu watashangaa. Hili la Makonda limeshamchafua rais, nasikia anajipanga kujifanya anamtumbua kwa lawama za juu juu kama njia ya kuficha uchafu wao. Hata akitumbuliwa leo ni geresha tu. Utasikia Makonda ametokea mlango mwingine.

“Hata huyu mhuni (Cyprian) Musiba ameagizwa kurusha mashabulizi dhidi ya Makonda kwa malengo maalumu maana wote ni kambi moja. Ni sanaa inachezwa kuzuga wananchi, kumsafisha rais.
 
Kwani kumiliki mashamba au viwanja kihalali ni dhambi?? Cha mhimu ni kuuliza au kufuatlia kwa waziri Wa ardhi kama anavimiliki kihalali!! Umbea hausaidii kitu!! Mwishoe mtaanza kusema kuwa siyo RAIA
 
Na unaposema kipato cha MTU unamaanisha nini? MTU anaweza kumiliki Mali akiwa bado yuko tumboni mwa mama take kabisa!! Kama mzazi akiamua kumlilikisha motto wake Mali alizonazo hapo kuna shida gani!! Mwingine kamilika mpaka Mali za babu zake! Hii ni tabia za familia tajiri !! Wasukuma wanamiliki ng'ombe wengi!! Mfano kama makonda ni msukuma na wazazi walimpa urithi Wa ngombe wengi na Leo akaamua kuwaza na kununua ardhi ambayo ni asset isiyoharibika tofauti na ng'ombe hapo kuna shida gani? Na baada ya mkoa Wa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi MTU mwenye akili na mjanja lazima anaunua viwanja chap kwa ajili ya maendeleo yake!! Hata Mimi nina 15 keka!! Njooni na hoja nyengine!!
 
Back
Top Bottom