Tetesi: RC Makonda ajimilikisha ekari 22.3 mkoani Dodoma, sawa na ukubwa wa viwanja 15 vya Soka

Tetesi: RC Makonda ajimilikisha ekari 22.3 mkoani Dodoma, sawa na ukubwa wa viwanja 15 vya Soka

PAUL Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, amemvua nguo RaisJohn Magufuli katika vita ya ufisadi.

Siri zake zimeanza kuvuja na imeanza kudhihirika kuwa hasira zote na bidii ya kunyamazisha bunge, wapinzani, wakosoaji, na vyombo vya habari ni mbinu ya kuwezesha wajanja kuvuna wasikopanda na kujilimbikizia mali kwa kutumia ofisi ya umma.

Shaka ya wananchi juu ya sababu za rais kudekeza na kumpendelea Makonda, ambaye kwa kutambua kuwa ni kipenzi cha Rais Magufuli amekuwa anatumia cheo chake na ukaribu wake na rais kupora mali na kujimbilikizia mali zisizo na maelezo ya kutosha, imeanza kupata majibu.

Mali nyingi alizonazo hazijulikani kwa tume ya maadili ya viongozi, na haziendani na kipato chake.

SAUTI KUBWA inaanza na viwanja vya ardhi sita vikubwa vinavyomilikiwa na Makonda katika mkoa wa Dodoma pekee.

Viwanja hivi sita anavyomiliki Dodoma vipo katika eneo linalojulikana kama Iyumbu New Town Centre, katika block R na S, vikiwa na ukubwa wa mita za mraba kati ya 5,000 na 40,000 kwa kila kiwanja.

SAUTI KUBWA inasema pasipo shaka kuwa katika ujumla wake, viwanja vyote sita vya Makonda vinachukua eneo la mita za mraba 92,341.

Mchambuzi mmoja anasema: “Kwa ukubwa huo wa viwanja, kama mita ya mraba moja iliuzwa kwa Sh. 3,500, Makonda alilipa Sh. 323,193,500 kununua viwanja hivyo.

“Kama mita moja ya mraba iliuzwa kwa Sh. 5,000, Makonda alilipa Sh. 461,705,000 kununua viwanja vyote. Na kama mita ya mraba iliuzwa kwa Sh.15,000, alilipa Sh. 1,385,115,000 kumiliki viwanja vyote. Waliofungua mahakama ya mafisadi, kama wanataka waaminike, waanzie hapa.”

Eneo hilo ni sawa na hekta 9.23 au ekari 22.3 za ardhi, ambazo ni sawa na ukubwa wa viwanja 15 vya mpira wa miguu (soka). Ni sawa na kijiji kidogo.

Viwanja hivyo, ambavyo vielelezo vyake vimeambatanishwa hapa, havijulikani kwa tume ya maadili ya viongozi.
View attachment 851704
Katika block R kuna viwanja vinne namba 1, 28, 32 na 33. Kiwanja namba 1 kina mita za mraba 40,973, na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 2,581,300.
View attachment 851705
Kiwanja namba 28 kina ukubwa wa mita za mraba 18,210 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 1,147,250.
View attachment 851708
Kiwanja namba 32 kina ukubwa wa mita za mraba 13,080 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 824,050.
View attachment 851709

Kiwanja namba 33 kina ukubwa wa mita za mraba 9,932 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 625,750.
View attachment 851711

Katika block S, Makonda anamiliki viwanja viwili, namba 17 na 18.
View attachment 851712
Kiwanja namba 17 kina ukubwa wa mita za mraba 5051, na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 318,250. Kiwanja namba 18 kina ukubwa wa mita za mraba 5,095, na kinalipiwa Sh. 321,000.

Kwa mujibu wa vielelezo ambavyo SAUTI KUBWA inavyo, hadi tarehe 21 Mei 2018, viwanja hivyo vilikuwa vimehakikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma. Ingawa mmiliki ni Makonda, vyote vinaonekana vimesajiliwa kwa ajili ya taasisi.

Suala la viwanja vya Makonda linaibuka wakati kuna sintofahamu juu ya makontena 20 bandarini ambayo Makonda anagoma kuyalipia kodi, huku Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiamuru yapigwe mnada kuokoa kodi ya serikali.

Makontena hayo, ambayo awali Makonda aliyakana, yameandikwa jina lake, naye anadai kwamba vifaa vilivyomo ni kwa ajili ya shule ambazo hata hivyo hazijulikani.

Hata huko Marekani anakodai vilichangwa, kuna utata juu ya watu wanaodaiwa walivichanga. Hapo hapo kumezuka hoja kwamba ndani ya makontena ya makonda kuna vifaa vingi zaidi ya samani za shule, na kwamba samani hizo zimetumika kufunika “mzigo” halisi.

Tayari kuna maelezo kuwa Makonda aliingiza makontena hayo kwa ajili ya miradi yake binafsi kwa kutumia ofisi ya serikali. Ubabe aliotumia kushambulia wanaohoji kuhusu makontena hayo, huku akitumia jina la rais ni baadhi ya mambo yanayoleta hisia kwamba kati ya Makonda na rais kuna biashara ambayo wananchi hawajaijua.

Baadhi ya wachambuzi wa siasa wameiambia SAUTI KUBWA kuwa uswahiba uliopitiliza kati ya Makonda na Rais Magufuli una harufu ya ufisadi.

Wanasema hata mabavu ya rais na Makonda kutumia vyombo vya dola dhidi ya raia wanaokosoa utawala wake ni mazalia ya ufisadi mkubwa utakaoibuka taratibu, hasa baada ya muda wa Rais Magufuli kuondoka madarakani.

Chanzo kimoja kimeiambia SAUTI KUBWA: “Usidhani Magufuli hajui uchafu wa Makonda. Anamlinda kwa sababu wana mradi wao. Makonda ni mtoto wa baba, ni mmoja wa viongozi wapendwa wanaojua dili chafu za baba; ndiyo sababu ya ushirika wao kunyamazisha wakosoaji.”

“Kama Watanzania walidhani Magufuli ni mwadilifu kama anavyojitapa mbele yao, walikosea sana; huyu anajulikana kwani katika wizara zote alikopitia, kulikuwa na kelele na mbwembwe nyingi za takwimu, lakini ufisadi ulitamalaki. Ataacha leo kwa vile yupo Ikulu?,” kimehoji chanzo kingine, na kuongeza:

“Hawa jamaa wana majengo na viwanja nchi nzima. Wanajimilikisha nchi utadhani dunia inaisha kesho au wanamkomoa mtu. Si uliona hata majuzi rais akiwa Mwanza, baada ya kumtembelea dada yake hospitalini, alisimama pale Nyerere Road kuzindua kwa siri jengo lake linaloitwa Nyerere Plaza, akajidai anazungumza na wananchi. Ni mali yake ile.

“Tutajua mengi sana kadiri muda unavyokwenda, na watu watashangaa. Hili la Makonda limeshamchafua rais, nasikia anajipanga kujifanya anamtumbua kwa lawama za juu juu kama njia ya kuficha uchafu wao. Hata akitumbuliwa leo ni geresha tu. Utasikia Makonda ametokea mlango mwingine.

“Hata huyu mhuni (Cyprian) Musiba ameagizwa kurusha mashabulizi dhidi ya Makonda kwa malengo maalumu maana wote ni kambi moja. Ni sanaa inachezwa kuzuga wananchi, kumsafisha rais.
Kwa mkuu wa mkoa kumiliki viwanja au ekari hizo 22 sio jambo la ajabu
Shida kama kavipata hisivyo halali
 
Sasa ukiangalia bei za hivyo viwanja mbona hata mfanyakazi mdogo tuu ananunua? Kwa kuna mtu alizuiliwa kununua? Mshahara wa RC ni shs Ngapi na ameanza kazi lini mpaka ashindwe vitu vidogo hivi? Tuache roho za kimasikini
Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo ni hulka ya ulafi, inakinzana na maadili ya utumishi
 
Na unaposema kipato cha MTU unamaanisha nini? MTU anaweza kumiliki Mali akiwa bado yuko tumboni mwa mama take kabisa!! Kama mzazi akiamua kumlilikisha motto wake Mali alizonazo hapo kuna shida gani!! Mwingine kamilika mpaka Mali za babu zake! Hii ni tabia za familia tajiri !! Wasukuma wanamiliki ng'ombe wengi!! Mfano kama makonda ni msukuma na wazazi walimpa urithi Wa ngombe wengi na Leo akaamua kuwaza na kununua ardhi ambayo ni asset isiyoharibika tofauti na ng'ombe hapo kuna shida gani? Na baada ya mkoa Wa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi MTU mwenye akili na mjanja lazima anaunua viwanja chap kwa ajili ya maendeleo yake!! Hata Mimi nina 15 keka!! Njooni na hoja nyengine!!
Sheria inataka aridhi uiendeleze ndani ya 36 month, ukishindwa unanyanganywa, je anaweza iendeleza??
 
Tulipoua Azimio la Arusha na misingi yake na kulipokea Azimio la Zanzibar, sisi wenye akili tulijua kuwa mwanzo wa utajiri kufuru unaingia Tanzania.
Kiongozi wa Umma hakujilimbikizia mali ( iwe amenunua,amerithi au amepora)
Tukamuona Julius Nyerere ni mhafidhina. Mzee aliona mbali.
Mwifwa! Paulo makonda alijaza fomu kuomba viwanja( vilitangazwa na mamlaka halali), akatafuta fedha ( kukopa kwenye taasisi za fedha) akalipia viwanja na kukabidhiwa viwanja vyake kihalali.
Analipa kodi ya ardhi na riba zake.
Kumsema huku itaonekana tuna wivu wa kimaskini.
Itaonekana chuki binafsi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
yale yaliyo semwa ....kuwa Yajayo yanafurahisa nadhani yameanza kuwadiaa kidogo kidogo na yanafurahisa kwel kwel.....nausubir tena muda wa watu kupata tabu kwel kwel naona unawadia after 2020
 
ushahamisha goli
maskini bana
Wapi nimehamisha goli wewe mtumwa wa Bashite? Tatizo lenu vichwa mnavyo ila matumizi ndio tatizo, hakuna mtu anashida na Bashite kununua viwanja au kumiliki mali ila tatizo lipo kwenye uwazi katika umiliki kama sheria inavyomtaka kutamka kama kiongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ukiangalia bei za hivyo viwanja mbona hata mfanyakazi mdogo tuu ananunua? Kwa kuna mtu alizuiliwa kununua? Mshahara wa RC ni shs Ngapi na ameanza kazi lini mpaka ashindwe vitu vidogo hivi? Tuache roho za kimasikini

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha wehu, hiyo ni bei ya kulipia land rent sio kununua kiwanja. Ili ujue bei ya viwanja chukua hizo sqm zidisha na bei ya kawaida ya kiwanja i.e price per sqm katika eneo husika. Mfano kama bei ya kiwanja ni Tzs 5,000 per sqm basi zidisha hiyo na hizo total sqm. Hivi shule mnasomea ujinga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thread kama hizi ni za kichochezi na hazina nia njema na Rais pamoja na nchi kwa ujumla.

Kitendo cha kudai kuwa Rais alizindua jengo lake liitwalo Nyerere Plaza alipokwenda kumuona mgonjwa, ni uongo wa first glade nadhani unafaa kwenye magroup yenu ya Kikabila ambako kuna kundi kubwa la Wajinga wanaodanganyika ovyo sio kuleta kwa GT.

Pia hata hizo Invoice ni disputable kwa sababu Invoice sio Hati ya kiwanja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Keshokutwa uje tena kutetea. Final glade wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapi nimehamisha goli wewe mtumwa wa Bashite? Tatizo lenu vichwa mnavyo ila matumizi ndio tatizo, hakuna mtu anashida na Bashite kununua viwanja au kumiliki mali ila tatizo lipo kwenye uwazi katika umiliki kama sheria inavyomtaka kutamka kama kiongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app

kanunua lini?

wapi hajadeclare?..weka uthibitisho

lini inapaswa mtu atoe taarifa baada ya kununua?

mengine yako

kama huna any evidence, sheria, kanuni....unabwabwaja
 
kanunua lini?

wapi hajadeclare?..weka uthibitisho

lini inapaswa mtu atoe taarifa baada ya kununua?

mengine yako

kama huna any evidence, sheria, kanuni....unabwabwaja
Sasa kumbe hujui either ame declare au hajafanya hivyo unabwabwaja nini hapa?
Na ni jukumu langu kukuonyesha kama haja declare au ni lako wewe unayetaka uthibitisho?
Mimi nimeamini hivyo sasa wewe usiyeamini hivyo kwanini usiende kutafuta uthibitisho wako ukauweka hapa kama unona hiyo ndio njia nzuri?
Ujifunze siku nyingine kupinga kama umeamua kupinga kwa kumuwekea ushahidi aliyesema tofauti na unachojua wewe.
Simply ni jukumu lako wewe mfuasi wa Bashite kutuambia viwanja hivyo amevitaja kwenye orodha ya mali anazomiliki, sisi tunasema hajavitaja kama unaona tunamuonea kashtaki kwake sisi tunaojua tutakuja kumthibitishia yeye mwenyewe Bashite sio wewe mtumishi wake wa ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja niwaambie kitu kimoja, kuwa na mali ya udhalim ni dhambi kubwa sanaa, lakini ktk siku za leo kuna watu wanaofikilia kuwa kila kiongozi mwenye mali amepata kwa udhalimu, hii hapana, ukiwa mwaminifu ktk Mungu, Mungu huwa anabariki, mfano, humpa mtu mawazo mema ya kutambua fulsa na akisha itambua fulsa pia hulinda kipato cha mtu, hii ninamaanakuwa utashangaa mtu anakipato kidogo lakini anafanya mambo ya maendeleo kuliko yule mwenye kipato kikubwa, kuna watu wengine au wenye mamlaka wanatumia pesa hovyo , lakini wengine huwa wanajinyima sana na wanakitunza kile wanachokipata, sasa kwanini hawa wanaojinyima wasiwe na mafanikio?hata ktk maofisi watu kama hawa wapo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu dogo anaangaika hata anunue wilaya nzima ya Chamwino sawa.
Ila ninachoamini mimi baada ya kipara kuondoka magogoni dogo hatokua na haki hata ya kupalilia kitalu cha hayo maeneo hayo ...zaidi ya kuozea jela au kuliwa kichwa.
Unless ni heri awekeze hivo viwanja ughaibuni / uhamishoni maana ndo itakua sehemu salama kwake kuishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom