Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata kuandika huwezi lumumbaRoho ya kimasikini inamwandama mwandishi wa grobu na grobu yake.
Kama naona vile watanzania wanaogopa kumiliki vitu kisa tu mawazo ya kimasikini.
Baku yangu kule kijijini ana mifugo yake na anamiliki Zaidi ya ekari 2,000 sasa huyo mwenye ekari 20 sijui mnamtaja wa nini.
Mkuu rejea kwenye bandiko langu, nimezungumzia kama taratibu zilifuatwa.maadili yanaruhusu?
ukijibu hili ntajua kama umepona au bado ki....a kinasumbua
Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Katoto kamoja kanaonekana kasele sana, mpaka kamenyoa kiduku!Kuna mtu atatandikwa Fimbo. View attachment 851747
Wewe utakufa mapema baada ya bwana wako Bashite kufukuzwa kibarua na hatimaye kuozea rupangoMmawia kafie mbele.
Wew mbona unaweweseka ka kuku aliyechinjwa ghafla, kwa nini lakini?Wewe utakufa mapema baada ya bwana wako Bashite kufukuzwa kibarua na hatimaye kuozea rupango
Sent using Jamii Forums mobile app
Tangu jana kijakazi naona mna mihasira ya hatariWew mbona unaweweseka ka kuku aliyechinjwa ghafla, kwa nini lakini?
Mwenye nchi kashasema wewe nani kijakazi tu?Wew mbona unaweweseka ka kuku aliyechinjwa ghafla, kwa nini lakini?
Sasa wasiswasi wako ni nini haswa?
Sasa wasiswasi wako ni nini haswa?
Mwenye nchi keshatoa tamko lake wewe kubali tu ndugu yetuSasa wasiswasi wako ni nini haswa?
Nakuuliza tena, wasiwasi wa nini?
Nakuonea huruma kwani ulikuwa unatetea kitendo cha Bashite sasa naona kimyaaaaa[emoji16][emoji41]Nakuuliza tena, wasiwasi wa nini?
Uko sawa kabisa, na pili kama hiyo hela aliyonunulia ni hela ya kipato halali!Swala hapa liwe kama alifuata taratibu katika kupata hiyo ardhi;
Sheria inaruhusu mtanzania yeyote kumiliki ardhi.
Mmmmmh nchi yangu Tanzania wenye madaraka wanakukula taratibu hata hawawazi kuna vizazi vijavyo, kama hawatakufa,kama wanajenga chuki kubwa baina yao na wananchi wanaoishi maisha magumu kutokana na vitendo vyao? eeeh Mungu tunusuru ma mabaya yanayoweza kutokea, ile amani izidi kutamalaki ndani ya nchi yangu pendwa Tanzania.PAUL Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, amemvua nguo RaisJohn Magufuli katika vita ya ufisadi.
Siri zake zimeanza kuvuja na imeanza kudhihirika kuwa hasira zote na bidii ya kunyamazisha bunge, wapinzani, wakosoaji, na vyombo vya habari ni mbinu ya kuwezesha wajanja kuvuna wasikopanda na kujilimbikizia mali kwa kutumia ofisi ya umma.
Shaka ya wananchi juu ya sababu za rais kudekeza na kumpendelea Makonda, ambaye kwa kutambua kuwa ni kipenzi cha Rais Magufuli amekuwa anatumia cheo chake na ukaribu wake na rais kupora mali na kujimbilikizia mali zisizo na maelezo ya kutosha, imeanza kupata majibu.
Mali nyingi alizonazo hazijulikani kwa tume ya maadili ya viongozi, na haziendani na kipato chake.
SAUTI KUBWA inaanza na viwanja vya ardhi sita vikubwa vinavyomilikiwa na Makonda katika mkoa wa Dodoma pekee.
Viwanja hivi sita anavyomiliki Dodoma vipo katika eneo linalojulikana kama Iyumbu New Town Centre, katika block R na S, vikiwa na ukubwa wa mita za mraba kati ya 5,000 na 40,000 kwa kila kiwanja.
SAUTI KUBWA inasema pasipo shaka kuwa katika ujumla wake, viwanja vyote sita vya Makonda vinachukua eneo la mita za mraba 92,341.
Mchambuzi mmoja anasema: “Kwa ukubwa huo wa viwanja, kama mita ya mraba moja iliuzwa kwa Sh. 3,500, Makonda alilipa Sh. 323,193,500 kununua viwanja hivyo.
“Kama mita moja ya mraba iliuzwa kwa Sh. 5,000, Makonda alilipa Sh. 461,705,000 kununua viwanja vyote. Na kama mita ya mraba iliuzwa kwa Sh.15,000, alilipa Sh. 1,385,115,000 kumiliki viwanja vyote. Waliofungua mahakama ya mafisadi, kama wanataka waaminike, waanzie hapa.”
Eneo hilo ni sawa na hekta 9.23 au ekari 22.3 za ardhi, ambazo ni sawa na ukubwa wa viwanja 15 vya mpira wa miguu (soka). Ni sawa na kijiji kidogo.
Viwanja hivyo, ambavyo vielelezo vyake vimeambatanishwa hapa, havijulikani kwa tume ya maadili ya viongozi.
View attachment 851704
Katika block R kuna viwanja vinne namba 1, 28, 32 na 33. Kiwanja namba 1 kina mita za mraba 40,973, na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 2,581,300.
View attachment 851705
Kiwanja namba 28 kina ukubwa wa mita za mraba 18,210 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 1,147,250.
View attachment 851708
Kiwanja namba 32 kina ukubwa wa mita za mraba 13,080 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 824,050.
View attachment 851709
Kiwanja namba 33 kina ukubwa wa mita za mraba 9,932 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 625,750.
View attachment 851711
Katika block S, Makonda anamiliki viwanja viwili, namba 17 na 18.
View attachment 851712
Kiwanja namba 17 kina ukubwa wa mita za mraba 5051, na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 318,250. Kiwanja namba 18 kina ukubwa wa mita za mraba 5,095, na kinalipiwa Sh. 321,000.
Kwa mujibu wa vielelezo ambavyo SAUTI KUBWA inavyo, hadi tarehe 21 Mei 2018, viwanja hivyo vilikuwa vimehakikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma. Ingawa mmiliki ni Makonda, vyote vinaonekana vimesajiliwa kwa ajili ya taasisi.
Suala la viwanja vya Makonda linaibuka wakati kuna sintofahamu juu ya makontena 20 bandarini ambayo Makonda anagoma kuyalipia kodi, huku Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiamuru yapigwe mnada kuokoa kodi ya serikali.
Makontena hayo, ambayo awali Makonda aliyakana, yameandikwa jina lake, naye anadai kwamba vifaa vilivyomo ni kwa ajili ya shule ambazo hata hivyo hazijulikani.
Hata huko Marekani anakodai vilichangwa, kuna utata juu ya watu wanaodaiwa walivichanga. Hapo hapo kumezuka hoja kwamba ndani ya makontena ya makonda kuna vifaa vingi zaidi ya samani za shule, na kwamba samani hizo zimetumika kufunika “mzigo” halisi.
Tayari kuna maelezo kuwa Makonda aliingiza makontena hayo kwa ajili ya miradi yake binafsi kwa kutumia ofisi ya serikali. Ubabe aliotumia kushambulia wanaohoji kuhusu makontena hayo, huku akitumia jina la rais ni baadhi ya mambo yanayoleta hisia kwamba kati ya Makonda na rais kuna biashara ambayo wananchi hawajaijua.
Baadhi ya wachambuzi wa siasa wameiambia SAUTI KUBWA kuwa uswahiba uliopitiliza kati ya Makonda na Rais Magufuli una harufu ya ufisadi.
Wanasema hata mabavu ya rais na Makonda kutumia vyombo vya dola dhidi ya raia wanaokosoa utawala wake ni mazalia ya ufisadi mkubwa utakaoibuka taratibu, hasa baada ya muda wa Rais Magufuli kuondoka madarakani.
Chanzo kimoja kimeiambia SAUTI KUBWA: “Usidhani Magufuli hajui uchafu wa Makonda. Anamlinda kwa sababu wana mradi wao. Makonda ni mtoto wa baba, ni mmoja wa viongozi wapendwa wanaojua dili chafu za baba; ndiyo sababu ya ushirika wao kunyamazisha wakosoaji.”
“Kama Watanzania walidhani Magufuli ni mwadilifu kama anavyojitapa mbele yao, walikosea sana; huyu anajulikana kwani katika wizara zote alikopitia, kulikuwa na kelele na mbwembwe nyingi za takwimu, lakini ufisadi ulitamalaki. Ataacha leo kwa vile yupo Ikulu?,” kimehoji chanzo kingine, na kuongeza:
“Hawa jamaa wana majengo na viwanja nchi nzima. Wanajimilikisha nchi utadhani dunia inaisha kesho au wanamkomoa mtu. Si uliona hata majuzi rais akiwa Mwanza, baada ya kumtembelea dada yake hospitalini, alisimama pale Nyerere Road kuzindua kwa siri jengo lake linaloitwa Nyerere Plaza, akajidai anazungumza na wananchi. Ni mali yake ile.
“Tutajua mengi sana kadiri muda unavyokwenda, na watu watashangaa. Hili la Makonda limeshamchafua rais, nasikia anajipanga kujifanya anamtumbua kwa lawama za juu juu kama njia ya kuficha uchafu wao. Hata akitumbuliwa leo ni geresha tu. Utasikia Makonda ametokea mlango mwingine.
“Hata huyu mhuni (Cyprian) Musiba ameagizwa kurusha mashabulizi dhidi ya Makonda kwa malengo maalumu maana wote ni kambi moja. Ni sanaa inachezwa kuzuga wananchi, kumsafisha rais.