Maswali kumi (10) magumu kuyajibu kuhusu kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuhusu Wabunge wa Chadema waliojiweka karantini kwa majuma mawili.
Nimeumizwa na matamko ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ndugu Paul Makonda. Kauli yake inaibua maswali 10 ambayo kama ukiweza kujibu hata moja tu, utakuwa umesaidia wengi.
Nanukuu
“....Mbunge anayepaswa kuwepo Dar es salaam ni mwenye kibali cha Spika, natoa saa 24 kwa wabunge wote wasio na vibali warudi Dodoma tofauti na hapo tutawakamata kwa kosa la usururaji kama tutakavyowakamata machangudoa...” (Youtube Millard ayo, 6-5-2020)
Katika kauli hiyo inaibua maswali ambayo sidhani kama naweza kutoa majibu yake hapa; Yafuatayo ni maswali tata kuhusu kauli hii:-
1) Je nani amempa mamlaka Mkuu wa Mkoa kutamka maneno kama haya?
2) Je Wabunge wanaweza kuamuriwa na Mkuu wa Mkoa kurudi bungeni akiwa kama nani?
3) Je mtu akitaka kutoka nje ya bunge huwa anakuwa na kibali cha Spika katika muktadha upi?
4) Je kosa la uzururaji kwa sasa ni kwamba ukionekana hujaenda kazini kwako unafuatwa na kulazimishwa kwenda?
5) Je unawezaje kuwafananisha wabunge na machangudoa?
6) Je Mkuu wa Mkoa anatumika na Spika?
7) Je spika ni dhaifu kiasi kwamba hawezi kuwaambia warudi bungeni?
8) Je Mkuu wa Mkoa ana mamlaka yoyote ya kumlazimisha mtu kufanya kazi?
9) Je hoja za mkuu wa mkoa zina mashiko yoyote kikatiba na kisheria?
10) Je kwa nini inapotokea matamko ya hovyo kama haya mamlaka ya uteuzi haisemi chochote? Je inawezekana kwamba inahusika?
Je unaweza kuongeza maswali?
Kama una majibu yake, nisaidie; usisahau kutaja namba ya swali ulilojibu.
Asante!
Sent using
Jamii Forums mobile app