RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

Kila siku kampeni ya kuwafukuza mjengoni ilipamba moto. Na ilikuwa ni jukumu la Spika na Naibu kutafuta sababu zozote kuwafungia wabunge hasa wa Chadema.
Sasa ghafla wabunge hao wameamua kuji isolate ili wasiambukizwe au kuambukiza wabunge wengine kwa siku 14.
Badala ya kufurahia absence yao, CCM imechukizwa sana na kulaumu na hasa kumshambulia Mbowe utadhani ni maamuzi yake binafsi...
Unajitekenya na kucheka
Yaani viti vya chadema vipakwe corona bila ya wabunge wa ccm kuathirika
Yaani wabunge wa chadema wakikamatwa watapakwa virusi vya corona!
Chadema mmatia huruma sana kwa mawazo kama haya
Hebu mtuambie,hizo siku 14,za kurura zikiisha mtarudi bungeni au makwenu?ni wapi ambako mnahisi mkirudi hamtaambukizwa?
 
Tutasikia mapicha mengi kipindi hiki cha corona, Eh Mwenyezi Mungu tuvushe salama waja wako.
 
Bashite anatutoa kwenye wajibu wa MOH kutoa taarifa za covid19,watu wanataka kujua kwasasa sample wanapeleka wapi kupima covid19 baada ya ofisi ya maabara kushutumiwa kwa vipimo feki na kutumiwa na mabeberu? Ummy na Majaliwa mbona kimya sana kutoa taarifa?
baada ya ile press its like COVID amerestishwa in peace ......
 
Sijui lakini,kule China Kuna tetesi walitumwa Asymptomatic kwenda America kukohoa kohoa arround kwenye mikusanyiko then wakasepa na kuacha msala New York,,
Sidhani Kama hi consipiracy ilutokea kwa uhakika
Ahaaa. Yaani mmekosa hoja mpaka mnachekesha watu bure. Any way mfa maji...
 
Paul Makonda nikuulize pale GRAN MELIA Arusha huwa unafuata nn pale?? Au wewe una vibali vya kuzurura nchi nzima?? Naona umechanganyikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha awakamate kwani huko Dar ndio kwenye majimbo yao? Kama wangekuwa majasiri wangerudi majimboni mwao wasaidiane na wananchi kupambana na Corona. Inachekesha mtu wa Iringa anaenda kukaa Dar na kuwaacha wana jimbo lake.

Halafu mnalazimisha yupi yupo sahihi aliyepo bungeni na yule aliyekimbia bungeni na kwenda kula raha Dar na mke wake badala ya kurudi jimboni apambane na corona akiwa na wananchi wake, halafu hawa hawa wahuni ndio unawasikia oh Rais atoke Chato aje ikulu wenyewe makwao wanakimbia, Chadema acheni utoto bana.
 
Wacha awakamate kwani huko Dar ndio kwenye majimbo yao?kama wangekuwa majasiri wangerudi majimboni mwao wasaidiane na wananchi kupambana na Corona.Inachekesha mtu wa Iringa anaenda kukaa Dar na kuwaacha wana jimbo lake . Halafu mnalazimisha yupi yupo sahaihi aliyepo bungeni na yule aliyekimbia bungeni na kwenda kula raha Dar na mke wake badala ya kurudi jimboni apambane na corona akiwa na wananchi wake,halafu hawa hawa wahuni ndio unawasikia oh raisi atoke Chato aje ikulu wenyewe makwao wanakimbia,Chadema acheni utoto bana.
Unampangia mtu sehemu ya kuishi? Mwambieni basi Jiwe atoke huko Chato arudi ikulu kama imewauma sana! Mmepishwa bungeni, shida iko wapi? Ni mpuuzi anayefikiri anaweza kumpangia mtu aishi wapi na kwa wakati gani!
 
Maswali kumi (10) magumu kuyajibu kuhusu kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuhusu Wabunge wa Chadema waliojiweka karantini kwa majuma mawili.
Nimeumizwa na matamko ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ndugu Paul Makonda. Kauli yake inaibua maswali 10 ambayo kama ukiweza kujibu hata moja tu, utakuwa umesaidia wengi.

Nanukuu
“....Mbunge anayepaswa kuwepo Dar es salaam ni mwenye kibali cha Spika, natoa saa 24 kwa wabunge wote wasio na vibali warudi Dodoma tofauti na hapo tutawakamata kwa kosa la usururaji kama tutakavyowakamata machangudoa...” (Youtube Millard ayo, 6-5-2020)

Katika kauli hiyo inaibua maswali ambayo sidhani kama naweza kutoa majibu yake hapa; Yafuatayo ni maswali tata kuhusu kauli hii:-

1) Je nani amempa mamlaka Mkuu wa Mkoa kutamka maneno kama haya?
2) Je Wabunge wanaweza kuamuriwa na Mkuu wa Mkoa kurudi bungeni akiwa kama nani?
3) Je mtu akitaka kutoka nje ya bunge huwa anakuwa na kibali cha Spika katika muktadha upi?
4) Je kosa la uzururaji kwa sasa ni kwamba ukionekana hujaenda kazini kwako unafuatwa na kulazimishwa kwenda?
5) Je unawezaje kuwafananisha wabunge na machangudoa?
6) Je Mkuu wa Mkoa anatumika na Spika?
7) Je spika ni dhaifu kiasi kwamba hawezi kuwaambia warudi bungeni?
8) Je Mkuu wa Mkoa ana mamlaka yoyote ya kumlazimisha mtu kufanya kazi?
9) Je hoja za mkuu wa mkoa zina mashiko yoyote kikatiba na kisheria?
10) Je kwa nini inapotokea matamko ya hovyo kama haya mamlaka ya uteuzi haisemi chochote? Je inawezekana kwamba inahusika?

Je unaweza kuongeza maswali?

Kama una majibu yake, nisaidie; usisahau kutaja namba ya swali ulilojibu.
Asante!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngumu Kumeza...Katibu Mkuu wa CCM wa Sasa aliwahi Kushauri Mkubwa Huyu Arudi shule akajifunze Uongozi. Possibly Hajui Mipaka na majukumu yake Kiutendaji---Swali Number..... 8
 
Mliopo Dar hebu tuambieni, korona imeisha na hali ni shwari kabisa huko, maana tunaona wachunguji sasa wanawaambia waumini wasivae barakoa, leo kuna uzinduzi wa msikiti wa mtoro, daladala watu wameanza kugombania, vp kwani, kakorona kameshasepa? au mzigo wa madagascar ushatua ndio maana jeuri inapanda?
Samahani mkuu hivi kwani huu msikiti ulifungwa kwasababu ya Covid-19 ama kulikua na ukarabati?
 
Back
Top Bottom