RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

Huyu mkongwe sana sio mwanafunzi mkuu.
Ila sikubaliani na logic yake,Mkuu wa mkoa hawezi kuropoka statements kama zile kimasihara kama anavyotuaminisha mtoa mada.Anataka kumsafisha Makonda mana anajua amekwisha feli kwenye kusudio lake.CHEZEA BITI LA ZITTO KABWE wewe!!!
Hivi nyie wanafunzi mnafungua lini shule?kwanini msisome hata online atleast muwe bze?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo zangu dar napata mchuzi wa pweza,
Bashite is just a CLOW -Sugu Moto chini a.k.a Deiwaka.

Ila huyu jamaa si mzima kichwani ienda ikawa dish limecheza,Yaani CCM kulikuwa na watu wa kupiga propaganda bwana lakini si huyu ch..ko, ccm imejifia kwa sasa hawana weledi wa kufanya Siasa na sasa kimekuwa kikundi cha kigaidi tu.hawana tofauti na Janjaweed.






Sent using Jamii Forums mobile app
 
Work From Home (WFH) kwa sasa ni kitu cha kawaida..... Sasa kama Mkuu kaamua kuWFM why not others.....!?
 
Hayo ni moja ya maamuzi ya kijinga sana kutaka kutumia sheria za RC kuweka ndani watu.

Nadhani Chadema sasa watumie CIVIL DISOBEDIENCE endapo kuna mbunge yeyote atakamatwa.

Sitashangaa kama ofisi za umma zitavamiwa na kuchomwa maana RAIA wamekasirika. Vituo vya mafuta jee? Nadhani jiji likichafuka dunia nzima itajiuliza kunani huko Tanzania? Maana hawa wanataka kuficha habari zao za kushindwa kudhibiti corona kwa kuwaharass wabunge wa Chadema.

Sheria gani inayo mlazimisha mbunge aingie bungeni? Ipi inamkataza kuwa Dar kama huko sio kwao.
Nitashangaa sana hili likipita, pengine vita itakayo anzia hapo ndio itabadili uongozi wa nchi. Sehemu nyingi zilizo ongozwa na wajinga, sababu za kijinga ndizo zimewaondoa



Sent using Jamii Forums mobile app

Na tusipotafuta Katiba mpya haraka, tutaangamia na watoto wetu, ndio maana hata Jiwe ana kiburi cha Herode tena hataki kuckia swala la katiba mpya.
 
Huyu mkongwe sana sio mwanafunzi mkuu.
Ila sikubaliani na logic yake,Mkuu wa mkoa hawezi kuropoka statements kama zile kimasihara kama anavyotuaminisha mtoa mada.Anataka kumsafisha Makonda mana anajua amekwisha feli kwenye kusudio lake.CHEZEA BITI LA ZITTO KABWE wewe!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Angalia maudhui. Makonda hata akisema kama ni kweli hawana cha kumfanya. Na Makonda hajawahi kutafuta kusafishwa.

Labda we mgeni nchini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siamini Makonda kama kweli alikuwa na nia yoyote ya kuwasaka hawa viumbe.
Alichotaka ni tujue kwa sasa wako wapi.

Kwa Zitto Kabwe tulikuwa tunajiuliza alipo maana tulikuwa tunamuona fb na twitter. Wengine wakasema yupo Dodoma, wengine wakasema hapana yupo Kigoma hasa kipindi kile alichotaka Magufuli aje ikulu ya Dar. Kumbe nae hayupo ofisini(jimboni) wala bungeni hayupo.
Tulidhani anasaidia wapiga kura wake kuwapa elimu ya kujikinga na covid 19 kwa kuwakumbusha kufuata miongozo ya wataalam huko jimboni. Kumbe kelele zote ni sababu kakaa tu dar hana kazi ya kufanya. Kweli huyu wa kumpuuza.

Haya hao kina Mdee waliondoka bungeni wakatuambia watakaa dodoma kwa ajili ya kujikarantini. Kumbe wapo Dar. Asingesema Makonda tusingejua. Ndio maana kina Silinde wakaona ni upuuzi. Unakimbia bungeni uje kula bata Dar. Bulaya alisema wabunge wajiudhuru nyadhifa zao kwa sababu wamekiuka maafikiano. Maafikiano ilikuwa kuwepo Dodoma, mbona wao wapo Dar. Nao wajiudhuru sasa. Kweli Chadema hii ya kina bulaya inachungulia shimo.

Hawa nao ni wa kuwapuuza tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kitu cha kwanza kabisa unachotakiwa kujua ni kwamba, kwa wakati huu, wabunge walitakiwa kukutana kimtandao kutoka popote nchini.

Kujazana bungeni wakati Covid-19 ishaingia bungeni ni ujuha mkubwa sana.
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda ametoa saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es Salaam kula bata, kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo, watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku.

RC Makonda amesema kwa hawajaalika wazururaji jijini Dar es Salaam maana wanaweza kuhatarisha zaidi maisha ya wanaDSM kwa kuwaambukiza ugonjwa wa Corona. Amesema wabunge wanaopaswa kuwa Dar ni wale tu wenye kibali Maalum cha Spika wa Bunge.

Ikumbukwe kwamba Wabunge wa CHADEMA kwa pamoja walikubaliana kutoingia Bungeni kwa kile walichodai kwamba wanajiepusha dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona baada ya vifo vya ghafla vya wabunge watatu na watakaa karantini jijini Dodoma ili kuangalia mwenendo wa afya zao.


BAADHI YA WABUNGE WALENGWA BAADA YA KUSIKIA KAULI YA MAKONDA

Mbunge wa Kigoma Mjini na MwanaJF Zitto amjibu RC, asema
Mimi ni Mbunge wa Kigoma Mjini. Nipo Dar es Salaam. Sijakwenda Dodoma Bungeni Kwa sababu ninaamini kuwa Bunge lilipaswa kuahirishwa ili kupambana na Korona. Sitakwenda Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hana Mamlaka yeyote ya kuniamulia niwe wapi katika Jamhuri ya Muungano

Sitakwenda Dodoma. Nitakaa Dar es Salaam kwa Uhuru kabisa. Najilinda dhidi ya Korona Mimi Binafsi na Familia yangu. Ninakaa nyumbani. Ninawalinda wapiga kura wangu wa Kigoma Mjini pia. Haya masaa 24 aliyotoa Mkuu wa Mkoa yaishe kwa Wabunge ni UPUUZI. ANIGUSE.


Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa naye amshukia RC Makonda
Nipo Dar Makonda jaribu kunikamata, mpuuzi wewe

Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya naye hakutaka kubaki nyuma
Wewe Bashite akili ndogo haitawali akili Kubwa usitafute kiki kupitia sisi ,sisi tupo Carantini tunajitambua, utaishia kukamata wabunge wa Chama chako na Mawaziri wenu ambao hawatulii Dodoma .Anza na Waziri wa Afya si Anakuwaga Dar ,kamata kama mzurulaji ..Acha kujitutumua .

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche naye akaamua kuibuka na Mistari ya Biblia
Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu,
ukimtwanga kama nafaka kwa mchi,
hutauondoa upumbavu wake.
Mithali 27:22


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akaamua kukumbushia kisa cha Mwamwindi kumuua Dkt. Kleruu
Kuna wakati nilisema hawa watoto wakiachwa waendelee hivi kuna siku wata chukua wake za watu kwa nguvu.Ujinga,kiburi utaingiza Nchi kwenye machafuko.Leo nime ikumbuka kesi hii,Republic vs Said Mwamwindi ya mwaka 1972.Said Mwamwindi alimuua RC Wilbert Kleruu

Kwamba imefika mahali RC Paulo anaweza kuwapangia watu tena Wabunge wapi wana stahili kuwa?Nani anawapa huu ujasiri?tunako elekea ni kubaya sana?Kwamba Wabunge wana fananishwa na Changudoa na wazururaji halafu Bunge litakaa kimya kwa sababu wanao fananishwa ni CHADEMA? HATARI SANA


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amejibu
Niko zangu DAR napata supu ya PWEZA ... Bashite is just a CLOWN


====

WABUNGE WAZURURAJI KUONDOSHWA DAR BAADA YA SAA 24.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo May 06 ametoa Saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es salaam "kula bata" kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la Uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura Usiku.

RC Makonda amesema Mbunge anaepaswa kuwa Dar es salaam ni yule mwenye Kibali au Ruhusa ya Spika wa Bunge tofauti na hapo ni vyema wakafunga virago vyao na kurudi Bungeni ili kuepuka kukamatwa.

"Hakuna asiefahamu kuwa sasahivi tuko katika Mapambano dhidi ya Virusi vya Corona na sio uzururaji, ifahamike huu sio Mji wa wazururaji hivyo natoa Masaa 24 kwa Wabunge wote kurudi Dodoma tofauti na hapo tutawakamata kwa kosa la Uzururaji kama tunavyowakamata Machangudoa" alisema RC Makonda

Aidha RC Makonda amesema kwa Sasa ni kipindi muhimu cha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali na wananchi waliwachagua kwenda kuwawakilisha Bungeni na kupigania maslahi yao hivyo kitendo cha kukimbia Vikao vya Bunge ni kutowatendea haki wananchi waliowachagua.

Hata hivyo RC Makonda amesema kinachomshangaza ni kuona Wabunge hao wamekimbilia Dar es salaam kufurahia Maisha badala ya kwenda Majimboni mwao kutembelea wananchi wanaokabiliwa na Mafuriko.

Pia soma > Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2

Kima ktk ubora wake. Ukiona paya anacheza cheza sebuleni jua kuna shimo karibu.
 
Back
Top Bottom