RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

Kweli ukiwa mpinzani Tanganyika ni sawa na panya anae ishi ndani ya nyumba.

Kila siku unawaza jinsi ya kumuua atoke ndani nyumba yako.

Poleni sana wapinzani ndio viongozi wetu walivyo baadhi yao ila si wote
 
Watakamatwa kama wanavyokamatwa Machangudoa ila Makonda huu ujasiri ameurithi kwa nani? [emoji23][emoji23]

Na hao wabunge kwanini wasikae majimboni mwao wanakuja kukaa Dar kwenye Corona?
... ni wapi hakuna corona nchi hii?
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa Saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es salaam kuhakikisha wanarudi bungeni tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la Uzururaji. Mbunge anaepaswa kuwa Dar ni mwenye Kibali cha Spika tu.View attachment 1441377
Kawaida Alcohol huwa kwenye pombe, lakini SIFA INA ALCOHOL NYINGI KULIKO POMBE. Kijana huyusifa zimemlevywa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu dogo sasa, maamuzi na maazimio yake kuna wakati yanafanya serikali yangu tiifu ya CCM idharaulike!
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ametoa Saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es salaam kula bata kuhakikisha wanarudi Bungeni, tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku.



MAKONDA%20MEI%206.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Makonda amesema kuwa Mbunge anayepaswa kuwa Dar es salaam ni yule mwenye kibali au ruhusa ya Spika wa Bunge, tofauti na hapo ni vyema wakafunga virago vyao na kurudi Bungeni ili kuepuka kukamatwa.

"Mbunge anayepaswa kuwepo ni yule mwenye kibali cha Spika, kipindi hiki ni hatari na tunataka watu wanaotoka majumbani ni wale wanaoenda kufanya kazi, hatujaalika wazururaji kutoka mikoani, inawezekana wakahatarisha zaidi maisha ya wakazi wa Dar es Salaam kwa kuwaambukiza Corona, kipindi hiki ni muhimu katika Bunge la Bajeti dhidi ya mahitaji ya wananchi" amesema Makonda.

Hata hivyo Makonda amesema kinachomshangaza ni kuona Wabunge hao wamekimbilia Dar es salaam kufurahia maisha, badala ya kwenda majimboni mwao kutembelea wananchi wanaokabiliwa na mafuriko.
 
Mpuuzi sio "tusi", ni sifa kama ufupi na urefu. Ni neno litokanalo na kitendo "puuza ama puuzia". Ikiwa wewe stroke ni mpuuzi hata usipoitwa mpuuzi haibadilishi kuwa wewe ni mpuuzi
 
Back
Top Bottom