RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

Suala alilolianzisha siku chache zilizopita la kusaka walanguzi wa sukari Mkoani Dar es Salaam limeshindika , hii ni kwa sababu DSM hakuna sukari madukani , hivyo haiwezekani kukamata ulanguzi wa bidhaa ambayo haipo .

Baada ya hili kumshinda sasa ameamua kuhamisha mada na kuiburuzia kwenye kuwakamata wabunge wa Chadema kwa tuhuma zinaitwa uzurulaji , Makonda binafsi hana uwezo huo na wala Lazaro Mambosasa , ambaye imejulikana anatii kila analotumwa na Makonda pia hana uwezo huo .

Mamlaka ya Uteuzi inapaswa kutathmini kama Makonda bado anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa , vinginevyo ni kujitafutia kudhalilika pamoja naye .
 
Bunge ukishaliweka mfukoni waweza mfanya Mbunge chochote unachotaka na Spika akawa kimya.... akakosa la kufanya.!!

Bunge linapogeuka kuwa kama kikao cha chama cha CCM, ni hatari kwa taifa..RC anapokuwa na nguvu na kusema anakwenda kula sahani moja na wabunge wote waliopo dar ni hatari, maana wanagonga kwako wanakutoa kwa tanganyika jeki hadi kwa pirato....hatujalishi una Corona ama huna utajieleza huko huko...

Tanzania hapa ndipo ulipofikia...
 
Kila nikitaka kumsifia jiwe nakumbuka anamlea Bashite moyo unabadilika. Hili likilaza sijui alilichimbia wapi
 
Bashite Hajawai Kufanikisha Jambo

Atafeli pakubwa sana ana habari TISS ndio ilishauri Chadema watoke bungeni ili kumshinikiza jiwe achukue hatua Dhidi ya corona.
 
Kila siku kampeni ya kuwafukuza mjengoni ilipamba moto. Na ilikuwa ni jukumu la Spika na Naibu kutafuta sababu zozote kuwafungia wabunge hasa wa Chadema.

Sasa ghafla wabunge hao wameamua kuji isolate ili wasiambukizwe au kuambukiza wabunge wengine kwa siku 14...
Nani kawalazimisha hao Wabunge kurudi Bungeni? Kama hofu ni viti na meza zao hazitokuwa salama basi wasigombee tena Ubunge maana hiyo mission itakuwa bado ipo na haitokwisha leo
 
Mmetoroka bungeni eti mnajiweka Karantini, sasa mnakwenda DSM kufanya nini wakati kila siku mnataka DSM ifungwe eti kisa CORONA?
ala kumbe Dar ni mali ya mtu .... kwamba unapokuja uje na taarifa sahihi...la karantine yako utaimalizia Segerea.
 
Kila siku kampeni ya kuwafukuza mjengoni ilipamba moto. Na ilikuwa ni jukumu la Spika na Naibu kutafuta sababu zozote kuwafungia wabunge hasa wa Chadema.
Sasa ghafla wabunge hao wameamua kuji isolate ili wasiambukizwe au kuambukiza wabunge wengine kwa siku 14.
Badala ya kufurahia absence yao, CCM imechukizwa sana na kulaumu na hasa kumshambulia Mbowe utadhani ni maamuzi yake binafsi.
Sasa ghafla RC Makonda naye anakuja na kitisho kipya ambacho wadadisi wa mambo wanahisi sio wazo lake bali katumwa.
Tetesi ni kuwa, viti na meza zao Bungeni hazingekuwa salama tena kwenye maambukizi kama mpango kabambe wa "futa, delete kabisa" na kwamba hata hiyo amri ya Dar kijingajinga waweza kukuta akakamatwa/wakakamatwa wabunge na wakiwa chini ya ulinzi kupakazwa vimelea vya ugonjwa huo.
Chadema na wabunge wenu kuweni makini kwani tetesi hizo mtaani haijulikani nani kazivujisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo kali ya kukamatwa. Sasa wangekuwa wajanja wangekwenda tu katika majimbo yao najua wengi wana makazi au nyumba za kuishi labda tu waiachie Dar. Mbunge akiwa jimboni kwake hawezi kuitwa mzululaji.
 
Hii ya leo ya Makonda inaleta ukakasi na kumpa mtu divergent thinking.
Kama waliweza kuwa na ujasiri wa kummiminia mtu risasi 38, kwanini wasitumie coronavirus kuwapakazia wabunge wa upinzani kwenye meza zao? This is avery simple lethal technique!
Kwa chuki iliyopo inawezekana sana tena sana. Upinzani kuweni macho sana tena sana.
Wewe siasa hujui fanyakazi inayokuhusu mkuu!!
 
Endeleeni kufanya mizaha na kura za wananchi.
 
Huyo anaenda kusambaza na kubakaza kwenye viti usalama wake unakuwaje? Na anakitunza vipi hicho kirusi cha korona ambacho hakionekani? Na kama ni hivyo walishindwa nini kufanya mapema. Hoja ya kipuuzi.
Sijui lakini, kule China Kuna tetesi walitumwa Asymptomatic kwenda America kukohoa kohoa arround kwenye mikusanyiko then wakasepa na kuacha msala New York,

Sidhani Kama hii consipiracy ilitokea kwa uhakika
 
Sasa subiri kwanza wakamatwe halafu mamlaka ya uteuzi itatoa taarifa kama anafaa au la
 
Tukiamua kuacha kujazana ujinga tunaweza kama tukiamua.
Mwenye akili za kufikiri mbali atawaza hivyo. Pamoja na kumpiga Lisu risasi, bado wakamfanyia unyama wa kutomtibu, kumvua ubunge etc. kama wanapata mwanya huu "mzuri" kwanini wasifanye hivyo. Hakuna ujinga hapa, unaangalia possibilities za watu unao na mashaka nao kufanya jambo
 
Sasa wapakize kwenye meza za wapinzani, dah!!! Kwani wakifanya hivyo kuna atakayebaki salama bungeni?!! This is an abstract concept mkuu.
 
Suala alilolianzisha siku chache zilizopita la kusaka walanguzi wa sukari Mkoani Dar es Salaam limeshindika , hii ni kwa sababu DSM hakuna sukari madukani , hivyo haiwezekani kukamata ulanguzi wa bidhaa ambayo haipo.

Baada ya hili kumshinda sasa ameamua kuhamisha mada na kuiburuzia kwenye kuwakamata wabunge wa Chadema kwa tuhuma zinaitwa uzurulaji...
Bashite anatutoa kwenye wajibu wa MOH kutoa taarifa za covid19, watu wanataka kujua kwasasa sample wanapeleka wapi kupima covid19 baada ya ofisi ya maabara kushutumiwa kwa vipimo feki na kutumiwa na mabeberu? Ummy na Majaliwa mbona kimya sana kutoa taarifa?
 
Back
Top Bottom