RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

Makonda alikuwa ofisi za Clouds mapema kuliko kawaida yake, mpaka tukahoji jamaa ana kipindi Clouds nini maana si kwa kuja huko kila siku lakini tuitetea tukajua ni sawa kama viongozi wengine wanavyofikaga mjengoni kila siku maana nikawaida yao!

Cha ajabu siku hiyo alikaa mpaka usiku akawa anamtafuta soudy Brown na Qwisser wa SHILAWADU muda huo walikuwa bado hawajafika kazini basi akawa anazungukazunguka tu ofisi hii anatokea ile kama mfanyakazi wa Clouds.

Kwenye Mida ya Saa kumi hivi akakutana na kina Soudy pamoja na prodyuza wa kipindi wakawa wanaongea kwa uficho hivi na usiri tukajua tu ni mambo ya kawaida ya kuhitaji uprivate lakini siku ile ulikuwa unatia mashaka sana.

Kumbe Makonda alikuja na Story ya mwanamke mmoja ambaye yeye Makonda alisema huyo mwanamke amezaa na mchungaji Gwajima na ametelekeza akawa anataka arekodiwe na ubuyu uruke kwenye kipindi cha SHILAWADU.

Basi wakakubalia kwa kuwa ni habari itabidi huyo mwanamke arekodiwe na kipindi kiruke siku ya jana lakini kawaida ya Kipindi cha SHILAWADU ubuyu ukipatikana lazima kila mtu apewe Natural Justice ya kusikilizwa pande zote mbili sababu huwa ndiyo kawaida ya kipindi.

Makonda siku hiyo hiyo ya Alhamisi akamwambia Soudy ajiandae then huyo mwanamke mnayemuona kwenye video na mtoto aliletwa na wasaidizi wa Makonda ahojiwe na Soudy Brown tayari kwa kurushwa kwa kipindi.

Siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ni jana SHILAWADU wakamtafuta Gwajima kwa upande wake kama anaifahamu hiyo ishu na je mwanamke huyo aliyetajwa ni kweli kwasababu tunaelewa ugomvi uliopo kati ya Makonda na Gwajima isijekuwa SHILAWADU wanatumika kuwafitinisha watu vibaya!

kwa bahati mbaya Gwajima hakupatikana jana ijumaa kwa ajili ya kurekodiwa na kufanyiwa mahojiano.

SHILAWADU wakatumia busara mpaka apatikane Gwajima scene ya Dada mwenye mtoto ziende kwa pamoja na ya mchungaji Gwajima kama kawaida ya POVU inavyokuwaga.

Jana usiku sasa kumbe Makonda alikuwa anafuatilia kipindi cha SHILAWADU aone kama kile kipande kitaruka hewani wapi ndiyo akaamua kuja Clouds na magari mawili yeye mwenyewe Makonda na Watu kama nane hivi wakiwa na Bunduki aina ya SMG geti la kawaida mlinzi alifungua geti kwasababu amezoeleka Mh anakujaga mjengoni wakafunguliwa kisha wakaingia ndani.

Walipofika reception wakazuiwa kuingia ndani sababu hatuna utaratibu wa kuruhusu wageni baada ya saa Nne usiku kuingia ndani ya Ofisi kama siyo mfanyakazi wa CLOUDS.

Alipoona wanazuiwa wakatoa bunduki zao mlinzi akashurutishwa afungue mlango kwa nguvu sababu walimtishia na Silaha mlimzi akafungua mlango wakaenda naye hadi studio kipindi kilikuwa kinaendelea hewani.

Makonda akawatoa nje Soudy na Mwenzake Qwisser akawauliza kwanini video aliyowaletea haijachezwa wakaelezea utaratibu jinsi utaratibu ulivyokuwa Qwisser wakati anajielezea akapigwa mtama akaanguka chini wakavamia mitambo ya transmission kwenye traycaster wakitaka kile kipande kirushwe hewani prodyuza wa kipindi akamuambia Makonda kwanini anavunja utaratibu na kutumia nguvu na ameshapewa utaratibu akapigwa na kitako cha Bunduki mgongoni akaanguka chini bahati mbaya kipindi kilikuwa kimefika mwisho.

Wakamshurutisha Prodyuza wa SHILAWADU anaitwa Chriss awape kile kipande wakaondoka naye wakati wanaondoka Ruge alikuja na Polisi akaingia lakini tayari walikuwa wameondoka ofisini wamechukua hicho kipande cha Video ya huyo mwanamke.

Hizo video zilichukuliwa kwa nguvu na Makonda na hao watu waliokuwa na Silaha inasemekana Makonda ana timu yake wanazisambaza kwa kasi na hatujui lengo lake ni nini.

Hata mkihitaji footage za Camera zipo jinsi tukio lilivyokuwa usiku wa jana.

ASANTENI SANA.
Mkuu mwaga hapa hapa jukwaani hizo footage tuone jinsi Bashite anavyotumia ubashite kulazamisha watu kuamini kuhusu vyeti.
 
Kwanza mwanaume kuzaa ni dalili ya lijali zaidi na si dhambi, cha Ajabu makonda hana hata mtoto wa kusingiziwa mpaka leo mkewe hazai wala yy hana mtoto ni Aibu jitu zima mpaka leo halina hata mimba za kupachika kwa Bahati mbaya kachepuka na kajala wakati mmewe akiwa jela lakini alishindwa kumpa mimba.
Kutopata mtoto sio aibu bali ni aibu kiongozi wa kiroho kuzaa nje ya ndoa
 
Hatimaye Mange amwanika SOUDY BROWN
mangekimambi_-20170319-0001.jpg
 
Na hili mh raisi wala hakumung'unya maneno, aljsema wazi kabisa akuna kilaza ataesalimika na zoezi ni endelevu. Mh. Rais kama ulivomtumbua kitwanga kwa ulevi wa pombe, huyu nae ni mlevi wa madaraka ni wakati wa kumtumbua sasa, hakuna namna tena!
Kitwanga alithibitika makonda akithibitika atatambuliwa tu lkn sio kwa pressure ya mbaya wake gwajima.
 
Mtoa Uzi akili zako unazijua mwenyewe ...sasa unawezaje kumuunhanisha Makonda na hili sakata LA huyu mama ??????...acha unafiki bana. Wewe ulikuwepo hapo clouds ambako alikutana nao ? Kama unaushahidi uweke sio kuja na porojo porojo zako .
 
Bishop Akiguswa Clouds Watafunga Kituo
Huyo Hana Mchezo Mchezo
Wakijichanganya
Watajiuwa Clouds
Mbwembwe ..... Hana lolote ...nchi hii inaongozwa na serikali ilopo madarakani yenye jeshi na vyombo vya dola na usalama ....hatupo tayari kuona usalama wa taifa ukiyumbishwa na porojo zenu.. Sana sana Gwajima ndie mpotezaji tuuu .
 
Sio lazima kuonyesha cheti kwa wananchi hakuna sheria inayomlazimisha zaidi ya utashi wa mtu kama mtu ana wasiwasi na uhalali na vyeti vya kiongozi aende mahakamani na ushahidi.

Huwezi ukathibitisha hana cheti kwa sab amekataa kuonyesha mahakama pekee yenye mamlaka hiyo.
Acha ubashite kwa sifa alizonazo ndugu yko angeita BBC na CNN kutangaza vyeti vyake
Lakini hana lolote yule ndo mana alikuwa analia makanisani na misikitini
Mwambie ndugu yko ma.vi anayoyatoa yanamchamfua JPM hata yy ananuka kwa sasa.
 
Acha ubashite kwa sifa alizonazo ndugu yko angeita BBC na CNN kutangaza vyeti vyake
Lakini hana lolote yule ndo mana alikuwa analia makanisani na misikitini
Mwambie ndugu yko ma.vi anayoyatoa yanamchamfua JPM hata yy ananuka kwa sasa.
Anuke au anukie haimzuii kuwa mkuu wa mkoa wala haimzuii jpm kuongoza
 
Kesho ntakaa.standby nisome watu wakivuliwa nguo
Yan wewe badala ujibu shutuma na kila uchao evidence zinatoka nzito
Unakuja na cheap accusations na zaid unaingia na kutishia watu ili wasambaze
Yan hapo umeudhihirishia umma kua yanayosemwa ni kweli
Sasa mmechokoza pasipochokozwa na zaid type za behaviour za mange sio kuingia kichwa kichwa kwa cheap acccusations kama unamrudishia kombora
Yatakayotoka kesho hakika watu mtatafutana
 
Wale waligundulika baada ya zoezi rasmi la kuhakiki vyeti kutangazwa nida walitembelea taasisi zote wengine waligundulika baada ya kuonekana watu wawili wenye jina moja wakipata mshahara kwahiyo walimsimamisha mmoja akijitokeza wanamhoji.

Serikali imefanya hivi kwa watumishi ambao wako kwenye sheria za utumishi wa umma tu ambao vyeo na madaraja yao yanapandishwa kulingana na elimu na taaluma zao. Zoezi hili halikuhusisha wateule wa rais na wanasiasa kwa sab elimu haitumiki kama kigezo cha kupata uteule kuchaguliwa n.k

Watu hao ni wakuu wa mikoa wakuu wa wilaya wabunge na madiwani ndio maana watu hao wana elimu tofauti katika cheo kimoja.

Hivyo makonda na wakuu wa mikoa wote uhakiki hauwahusu kwa mujibu wa zoezi lenyewe. Kwahiyo hakuna logic kwanini ahakikiwe makonda tu?

Pamoja na kwamba zoezi la uhakiki halifanywi kwa wakuu wa mikoa haiwapi ruhusa ya kufanya kosa la jinai kama la kughushi cheti na kuachwa hivi hivi kwahiyo kama kuna mtu mwenye ushahidi kuwa makonda amefoji cheti kwa kuwa ni kosa la jinai aende polisi necta au mahakamani na ushahidi ili mashitaka yafunguliwe ushahidi usikilizwe na maamuzi yafanyike. Kama kweli ikithibitika pasipo shaka makonda kafoji cheti afungwe tu kama wengine na kama ikiwa kinyume chake awe clean. Lkn kwa njia ya kudai cheti akilete mtandaoni au kwenye media ni utashi wake tu kukubali ama kukataa kwa sababu hakuna sheria inayomlazimisha kufanya hivyo wala kumzuia asifanye hivyo.
We unaongea tu, kwani ili vyombo vya usalama vichunguze jambo ni mpaka pawe na mlalamikaji? Humu mitandaoni wanaokamatwa kwa uchochezi ni nani anaeenda kufungua kesi? Tuhuma zingekuwa mbowe anawatoza ushuru machangudoa mdani ya casino lake" asinhechunguzwa!?
Wasiempanda ndo kawa rais wa wanasheria kazi wanayo!
 
Nyie ndo mabashite wengine, unatetea mpaka uozo.cjui kichwani umejaza nini?
Mimi ni mwanasheria ninaheshimu taaluma mtu yeyote ni innocent mpk mahakama iamue vinginevyo. Hakuna ushahidi wa convict makonda mpk upelekwe mahakamani na uthibitishwe kama utathibitishwa afungwe tu sina tatizo lolote lkn sio haki kumuhukumu kwa sababu yA maneno ya mgomvi wake.
 
We unaongea tu, kwani ili vyombo vya usalama vichunguze jambo ni mpaka pawe na mlalamikaji? Humu mitandaoni wanaokamatwa kwa uchochezi ni nani anaeenda kufungua kesi? Tuhuma zingekuwa mbowe anawatoza ushuru machangudoa mdani ya casino lake" asinhechunguzwa!?
Wasiempanda ndo kawa rais wa wanasheria kazi wanayo!
Inategemea ni jambo gani na tuhuma zimetoka wapi na ushahidi wake unapatikanaje.

Kwa mfano kwanza kabisa aliyetoa tuhuma ni victim wa vita vya madawa ya kulevya hiyo peke yake inatia mashaka.

Pili ushahidi kuupata ni ngumu bila kuletwa na watu wanaotuhumu.
 
Back
Top Bottom