RC Makonda: Idadi ya maambukizi imepungua Dar, kuna watu walinunua majeneza na kupiga picha ili kuzua taharuki

RC Makonda: Idadi ya maambukizi imepungua Dar, kuna watu walinunua majeneza na kupiga picha ili kuzua taharuki

Huyu jamaa anatakiwa hata makampuni ya mitandao imfungie, yaani inasema instagram @tweeter na facegear wanatumiwa na mabeberu kuiangusha serikali hii ya kidhalimu?

alafu na wao wanamuacha anakuwa na akaunti nao?
 
Da hivi hawa viongozi wanakwama wapi kutoa kauli kama izi why yatupwe dar na so mikoa mingine? Basi nafikili ulinzi dar sio imara kama mikoani kama ni kweli.

Maana kama watu wana nia ovu ya kuizalilisha serikali wanaweza fanya popote mikoani na kama ndo ivyo niwapongeze kamati za ulinzi zote kutoka mikoani maana hatujasikia ili huko tumelisikia huku jiji la kandoro
uwezo wake wa kufikiri uliishia hapo, akadhani anaweza kuleta hadithi za kitoto/kijinga zikakubalika kwenye jamii
 
Epidemiologist wamesema ivyo au ndo tunataka kutupa jiwe gizan tuone nani atapiga kelele.
Watu tunatafuta hela kumbe kuna bunch of people wananunua majeneza😁😁,,,,,,,,,,ila hii nchi waisraeli wenyew wakija watasalimu amri.


Too much sense will not kill me.

Hhahaa nimecheka mistari miwili ya mwisho..hii nchi nadhani hata mbinguni wataingia wachache wanaojitambua! Sijui tuna laana gani jamani
 
DAB angekuwa anapita humu JF nadhani akili yake ingekuwa tayari imeboreka, si kwa hizi za uso anazotupiwa
 
Hii nchi ngumu sana. Kweli watu wanunue majeneza kabisa kwa ajili ya kuigiza kuzika?
Yan jamaa, kweli nimeamin ukiwa na upeo mkubwa wa kufikiria ndo unapata matatizo mengi sana......... yan this is rubbish, Uharo kabsa cr mzima kusema
 
Hapo alipotoa hiyo kauli ya "...kununua majeneza na kwenda kuyachimbia makaburini" ndipo kaharibu kabisa.

Amefanya hata ambao wangeamini kauli ya kwanza ya kupungua kwa corona wasiamini tena. Anyway, kama yule mkubwa anaweza kuongea vile kwa nini tumshangae huyu, masikini ya Mungu hata shule haijui.
 
Yeye si ndiye aliyesema kwamba watu wanapukutika mpaka akaenda kununua dawa ya kuulia mende na kuwaagiza kikosi cha Fire keenda kuipulizia mitaani au?
 
Tumefikia huku kikubwa ni kujilinda mwenyewe
 
Kisa halijakufurahisha ndo linakuwa la kipuuzi...Nawe una tatizo vile vile
Uko nje ya key kabisaa!Mwendelezo ule ule wa siasa za majitaka kwenye mambo serious!Jiulize maswali mepesi kabla hujakurupuka kujibu!

1.Makonda ni mkuu wa mkoa,atueleze ni akina nani wamenunua majeneza na kwenda kuchimba mashimo ili kuzua taharuki?Atueleze pia Mashimo hayo yako wapi na majeneza yako wapi?Aeleze amewachukulia hatua gani za kisheria?

2.Huyu siku chache zilizopita alisema hali ya Corona Dar inatisha,baada ya hotuba ya Rais ya mwisho amekuja kivingine!Kama Maabara inachunguzwa na kwa maana hiyo hakuna vipimo vya Corona, amejuaje kama maambukizi yamepungua sana na hali ni shwari DSM?

Weka mihemko na mahaba pembeni na uiruhusu akili yako uliyojaaliwa na Allah ikuongoze!
 
Back
Top Bottom