RC Makonda: Idadi ya maambukizi imepungua Dar, kuna watu walinunua majeneza na kupiga picha ili kuzua taharuki

RC Makonda: Idadi ya maambukizi imepungua Dar, kuna watu walinunua majeneza na kupiga picha ili kuzua taharuki

Huyu kiongozi ni "ZERO ZERO ZERO KICHWANI" kabisaaa. Yani kichwa chake kimejaa "MATOPE". Akili zake hua anakua amezikalia. Yani ni punguwani kabisa hili jamaa.

Haya maradhi sio yakufanyia mzaha, ni hatari sana, yapaswa tuyachukulie "SERIOUS" sanaa.

Imefikia hatua nchi zote za jirani zinatuona kama mkaa wa moto. Tanzania tumekua kama vile "WAZALISHAJI/BREEDERS/INCUBATOR" ya COVID-19.
Halafu unajiuliza, idadi ya wagonjwa wanajua kweli hata waseme maambukizi yamepungua. Wehu wa kutisha huu. Duuh hatari.
 
Hii nchi ina katiba mbovu na mihimili iliyochakaa ndo maana jitu linazomoka na kuongea UTOPOLO tena katikati ya majanga na hakuna wa kubisha.
 
Majeneza yananunuliwa mtandaoni? Yale Yale ya Yule baba yake kuwa amefanya utafiti kakuta mapapai yana corona, hivi hawa watu shule walienda kweli?

Au kuna dhambi wamefanya inawatafuna? Maaana ujue mtu alietenda dhambi kubwa unamkuta anajiongelesha vitu vya kitoto kabisa na yeye anajisikia raha kuona yuko sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Dhambi dhidi ya TAL
 
Mambo mengine ndio hata yanamfanyaga MUNGU asijibu maombi kabisa. statement nyingine zinazotoka kwa viongozi zinakuwa machukizo kwa MUNGU. Imagine mdomo huohuo utumike kuhamasisha watu kufanya maombi dhidi ya Corona, tena mdomo huohuo utumike kuongea mambo ambayo deep down their hearts wanajua si ukweli. MUNGU huwa anatazama zaidi mioyo ya watu nakujua yupi anaomba kwa kumaanisha na yupi anaongea tu ili mradi aoekane anamtaja MUNGU. Kama waamini wa MUNGU tungelielewa hili, tungeacha kabisa kufanya maigizo ili tuonekane mbele ya watu bali tungefanya yale yanayomgusa MUNGU pale aitazamapo mioyo yetu. Biblia katika kitabu cha Mithali 15: 8 inasema “ sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA, bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake”
 
Point of correction;Mimi si mtu wa serikalini...,Simfuatilii hata huyo Kigogo....Huku nilipo hakuna shida ya sukari;ni 2,800/= per kg.
Sisi ni wabinafsi sana, ukiwa na kitu ulipo huwezi jali wenzako wanaohangaika kutafuta hicho kitu.
 
Ukiona mtu anaongea ujinga sn mbele yako wakati mwingine jichunguze uwelewa wako. Huenda huyo anaongea ujinga kutoka na upeo wako ulivyo
 
Video zinaonyesha watu wanalia na majeneza wewe unasema zimetengenezwa? Usiwafanye watu mazuzu.
 
Mkuu Mabeberu sio watu wazuri, Rais wa Madagascar aliambiwa atapewa doller miloon 20 ili aweke sumu kwenye dawa waliogundua ili iue waafrica
MMH na wewe nawe ukaamini ujinga huo bila ya kuhoji wala kujihoji? Nadhani wewe ni ndio mwenye TATIZO zaidi kuliko hata alokwambia.
 
Hao watu ni noma, wakanunua majeneza, wakanunua PPE wakavaa, wakachukua ambulance na yale ma-DFP, wakawapigia simu wanafamilia wa majeneza ili wakafanye maigizo, wakafika makaburini kufanya maigizo at the same time wakakataza watu kupiga picha.... Ova.
 
upo sahihi mkuu!. ila pia hali sio shwari kwa takwimu ipi pia!? nauliza tu kuondoa ujinga nna imani utanijibu kwa weledi bila hisia

Hatupimi watu wetu kujua nani mgonjwa na nani sio mgonjwa hivyo nchi yetu haina data yakuweza kusema kwa usahihi juu ya janga hili la corona na jinsi linaiyoathiri nchi yetu!!
 
Back
Top Bottom