RC Makonda na Viongozi wa Dini Kwenye Matembezi ya Amani Arusha

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
"Tutalala mpaka chini kumuomba Mungu"

Waumini wa dini mbalimbali wa dini ya kikisto wameendelea kuomba dua kwaajili ya kuifungua Tanzania katika nyanja mbalimbali.

Waumini hao kila mmoja alikuwa ananena kwa lugha yake.

Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amefanya tukio kubwa na la aina yake mkoani humo la kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa dini na kufanya maombi ya pamoja kwaajili ya kuuombea mkoa huo pamoja na Taifa.

Maombi hayo yalianza kwa matembezi ya amani kutoka Round About ya Impala hadi mnara wa saa.
Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha Poul Makonda ameongoza mamia ya wananchi wa mkoa huo kuliombea taifa pamoja,tukio hili lililo simamiwa na Viongozi wa dini wa mkoa wa Arusha.

Soma Pia: RC Makonda na Viongozi wa Dini Kwenye Matembezi ya Amani Arusha


Maombi haya yanafanyika ikiwa leo tarehe 9 December. 2O24 siku ya miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika.

Your browser is not able to display this video.
 
Na ukimuona mtu anajifanya katili na asiyekuwa na hofu ya Mungu ujue huyo ni mwema?

Acha wivu na kukariri.

Mwovu atabaki kuwa mwovu na mtu mwema atabaki kuwa mwema bila kujali maigizo au mwonekano wa nje
Mtu mwema hana haja ya kujibaraguza.
 
Ila mwamba kila anachogusa huwa kina mwitikio mkubwa,ana kipaji cha kuwa kiongozi mwenye mamlaka na kukubaliwa na wananchi
Na ndiyo aliweza hata kumshawishi mtu mwingine kumuachia cheti na jina lake, ili alitumie maisha yake yote! Siyo jambo jepesi hata kidogo.
 
Sijui nani ametufunza au katika somo la Uchumi sijaona chapter au hata statement yoyote inayosema ili Uchumi ukue lazima muombe Mungu, sio kwamba napuuza uwepo wa Mungu wetu, la harsha, ni kwamba kama tunafanya mambo ambayo sio sawa, Uchumi kukua haihusiani na kukesha na kupiga makelele eti kumuomba Mungu, ni vitu viwili tofauti, nadhani hata Mungu wetu anatushangaa, maana watu wake wamekosa maarifa na Mwenyezi Mungu anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, usikute ndio kuangamia huku.

Uchumi haukui kwa kukesha kwa maombi au kunena kwa lugha za uongo uongo, naona kama tunakwenda njia tofauti..!!
 
Anaangaika sana ili aonekane ni mtu mwema,mnyenyekevu na mwenye huruma lakini moyoni mwake lazima atakuwa anateseka kwa maovu aliyoyafanya dhidi ya wengine,anajuta.
Sina uhakika kama una ushahidi wa hayo maovu unayo yaongelea hapa,

Ila kitendo cha kusema Anajuta ni dalili ya mtu kutambua makosa yake na kua mwema,mtu muovu hua hajuti bali huendeleza uovu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…