RC Makonda: Watu wanafunga maduka, wanajifungia majumbani kisa Corona, mtakufa na njaa

RC Makonda: Watu wanafunga maduka, wanajifungia majumbani kisa Corona, mtakufa na njaa

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
8,926
Reaction score
17,880
"Tokeni kafanyeni kazi eti Watu wanafunga maduka, wanajifungia majumbani kisa Corona, mtakufa na njaa, ndio maana leo nawafuatilia wakandarasi, sasa nimkute mkandaraai hayupo site kisa corona, kuna wapuuzi huko wanasema Serikali inadanganya idadi imeongezeka, kwenu kuna Mtu amekufa na corona? kuna Mtu kwenu anaumwa corona?, hiyo idadi imetoka wapi?" - Paul Makonda, RC DSM

Good work our focused leader.

======

Wananchi wanaingia hasara kwa kukwepa majukumu yao huku mambo yakienda tofauti wanaanza kuilalamikia serikali ili iweze kupatia msaada.

Amesema hayo leo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaaam Mh Paul Makonda wakati akikagua mradi wa TARURA katika eneo la Kinondoni shamba ambapo kumekuwa na mgogoro baina ya TARURA na wananchi wa eneo hilo.

Pia amewataka wananchi kuacha kujifanya wajuaji wakati tatizo linapokuwa kubwa kwasababu wakati watu wanaingia katika eneo la mradi ambalo hawatakiwi kuvamia.

Vilevile amewataka wananchi kufanya kazi huku wakichukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona wasikae ndani watafute hela ili wasije wakafa na njaa.

“Tokeni ndani mkafanye kazi Corona isiwe kigezo cha kujifungia ndani tumepambana na magonjwa mengi ikiwemo kipindupindu na magonjwa mengine tufanye kazi huku tukichukua tahadhari’amesema Makonda.

Aidha Makonda amekukagua miradi ya barabara inayotekelezwa na TARURA katika wilaya ya Ilala na Kinondoni kujua maendeleo ya miradi hiyo.

“Barabara ni ahadi ya muda mrefu ya Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ijengwe kutoka makao makuu wa Bakwata hadi Biafra”amesema Makonda.

Hatahivyo amepokea taarifa ya mgogoro kutoka kwa wananchi wa eneo lile kwa kutaka kuvunjiwa nyumba zao bila kupata fidia na walio lipwa wapo na hawajipotiwa na barabara hiyo.

Aidha amewataka wananchi kuwa atatuma kamati yake ifanye ukaguzi na wataanza jumatatu ili walete majibu kamili ili mradi huo uende kwa haraka.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa mkoa wa Dar Makonda amewashangaa wananchi kujifungia ndani kisa Corona.

Makonda amesema watu watoke wakafanye kazi taratibu za kujikinga na corona ziko wazi, hivyo kujifungia ndani kisa Corona ni uzembe.

Amewashangaa wafanyabiara kufunga maduka kisa Corona.

Pia ameonya wanaosambaza habari kuwa kuna wagonjwa wengi ila wanafichwa, amehoji kwenye familia yako kuna mtu anaumwa corona ama amekufa na corona serikali imeficha.

NB. Kwa hizi kauli za viongozi ikitokea Corona ikatupiga sawasawa sidhani kama kuna Taifa litatia mguu kutusaidia.

Hata kama serikali ina msimamo wake kuhusu hili wangefanya kimya kimya, kutangaza hadharani hivi ni hatari kwa mstakabali wa Taifa letu.



 
Tanzania wananchi wanajifungia ndani lakin Serikal inawahamasisha watoke Nje wafanye kazi

Kwingineko Duniani Wananchi wanataka kutoka nje kuchapa kazi Serikal zao zinawazuia kwa hofu ya Corona

Maana yake Wananchi wa TZ ni waoga na wavivu wakati Serikal yao ni ya kijasiri na kichapa kazi

Kwingineko Serikal zao za kivivu na kioga wakati wanancho wao ni wachapakazi na majasiri



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda anatamani kuwa waziri wa afya kipindi hiki Cha corona ili apate Kuongolewa.
Kwangu mimi siamini mataifa mengine makubwa yenye wataalam si wajinga kiasi cha kuwaambia raia wake wajifungie. Hata kama kwa sababu moja au nyingine Tanzania haitaathirika sana na huu ugonjwa bado tu siwezi kusifu hatua zilizochokulia na nchi yetu kwa sababu wanafanya kamari mbaya sana. Siyo kwamba nataka wafanye lockdown kama nchi za Ulaya hapana. Kuna vitu wangeweza kufanya zaidi ili kuonyesha wanajali. Kuna mikusanyiko ambayo mpaka sasa inaendelea eg Bunge, Magulio, nk ambayo haina umuhimu na ni njia kuu ya kueneza hawa virus.
 
Back
Top Bottom