RC Makonda: Watu wanafunga maduka, wanajifungia majumbani kisa Corona, mtakufa na njaa

RC Makonda: Watu wanafunga maduka, wanajifungia majumbani kisa Corona, mtakufa na njaa

Kesaboso,
Sema tahadhari" au "kufurahi"siyo "tahadhali" au "kufulahi". Ukisikia watu wanasema idadi siyo sahihi wanaelewa siyo wewe unayekaa huko ziwani kwenye mazizi ya ng'ombe. Wewe ndiyo ZEZETA hasa tena inawezekana la Kisukuma.

Tunataka ukweli ili wananchi waelezwe hali halisi tuweze kuchukua hatua, wala hatuhitaji sifa. Unapoeleza hali halisi unasaidia wananchi kujihami na kuchukua hatua kwa wakati.

Haya yanayotekea kwenye nchi zilizo na maambukizi zaidi ni kwamba hawakuchukua hatua madhubuti. Kwetu naona tunaelekea huko.
 
Yawezekana au isiwezekane kuwa yuko sahihi maana kwa kauli za namna hiyo bila kuwa na akiba ya maneno ni hatari zaidi kuliko imani aliyonayo kuhusu corona..kauli yake isije kufatiliwa na maadui kutimiza uovu wao katika taifa letu maana wanaweza kufanya juu chini ili huu ugonjwa uenee nchi nzima ikiwa ni jitihada za kutukomoa ili wapate kuaminika kweli kwamba ugonjwa huu ni hatari sana
Huu ugonjwa haupo ila unaweza letwa kwa makusudi kutimiza agenda zao.

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Siyo hivyo RC. Ugonjwa huu ukienea tutaisha. Ngoja tusubiri Wataalam wa Afya watuambie
 
Mkuu wa mkoa wa Dar Makonda amewashangaa wananchi kujifungia ndani kisa Corona.

Makonda amesema watu watoke wakafanye kazi taratibu za kujikinga na corona ziko wazi, hivyo kujifungia ndani kisa Corona ni uzembe.

Amewashangaa wafanyabiara kufunga maduka kisa Corona.

Pia ameonya wanaosambaza habari kuwa kuna wagonjwa wengi ila wanafichwa, amehoji kwenye familia yako kuna mtu anaumwa corona ama amekufa na corona serikali imeficha.

NB. Kwa hizi kauli za viongozi ikitokea Corona ikatupiga sawasawa sidhani kama kuna Taifa litatia mguu kutusaidia.

Hata kama serikali ina msimamo wake kuhusu hili wangefanya kimya kimya, kutangaza hadharani hivi ni hatari kwa mstakabali wa Taifa letu.



wanakosea aana kuongea waziwazi. sasa mfano itokee corona ipige kisawa sawa watasemaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha niwe mvivu siwezi kuamini maneno ya Kibwetere hata siku moja...hela zinatafutwa tuu hasara roho pesa makaratasi..
 
Naunga mkono kwa kile alichoongea RC wa Dar es salaam.
 
Ni nini chenye umuhimu kuliko uhai? Bunge shughuli zinaweza kusimama kwa muda ili kuokoa uhai. Je uhai ukipotea bunge litaurudisha?
mnajipa presha za bure tu!hakuna ugonjwa wenye scale ya kukutisha hivyo bhana,politics tu!🚶‍♂️🚶‍♂️
 
Graph,
Kwa taarifa yako: jana huko UK miongoni mwa wagonjwa waliofariki kuna watu 40 ambao walikuwa wazima kabisa. Yaani hawako kwenye risk group.

Unless kama unaniambie Tanzania itumie ursa ya huu ugonjwa kupunguza idadi ya raia wake.

Tatizo la virus kama hawa wanaweza mutate wakati wowote akageuka akawa virus mpya anayeua vibaya, ila tuseme ukweli Tanzania ikisema watu wasitoke nje watu watakula vipi? Watu wana njaa balaa.

Labda kila mtu aanze kutembea na mask na wabane kwelikweli mikutano hasa wadandia daladala maana wanagusana mno, na makanisani, sijaona watu wanasali kama watanzania dunia nzima. Kukaa ndani sio solution kabisa kwa nchi kama Tanzania watu watakufa njaa balaa, the maj
 
Tatizo la virus kama hawa wanaweza mutate wakati wowote akageuka akawa virus mpya anayeua vibaya, ila tuseme ukweli Tanzania ikisema watu wasitoke nje watu watakula vipi? Watu wana njaa balaa.

Labda kila mtu aanze kutembea na mask na wabane kwelikweli mikutano hasa wadandia daladala maana wanagusana mno, na makanisani, sijaona watu wanasali kama watanzania dunia nzima. Kukaa ndani sio solution kabisa kwa nchi kama Tanzania watu watakufa njaa balaa, the maj
Mimi sijapendekeza watu wakae ndani. Hoja yangu ni kuwa kuna mikusanyiko isiyo na ulazima bado inafanyika. Na viongozi wengine wajinga kama Makonda wanawafanya watu wasiwe makini kwa kuhimiza ujinga uliowajaa vichwani.
 
Mkuu kilichofanyika Italy ni Kama hiki kinachofanyika hapa kwetu.waliambiwa wajifungie ndani wakajifanya wao wanajua kupiga kazi,by the time wanajifungia ndani tayari kila familia Ina mwathirika then wakaanza kuambukizana ndani kwa ndani,Kama Tanzania haina Mungu wa pekee yake,Basi utaniambia kitakachotokea Makonda na Magufuli huko tuendako,tuombe uzima
Acha urongo/uongo. Muongo mkubwa kabisa. Lini Italy waliambiwa wajifungie ndani wakakataa?hivi mnatuona sisi wabongo ni viazi sana ee?
 
Acha urongo/uongo. Muongo mkubwa kabisa. Lini Italy waliambiwa wajifungie ndani wakakataa?hivi mnatuona sisi wabongo ni viazi sana ee?
Mkuu uwe unasoma unaelewe,kwani hapa kwetu Kuna mtu kaambiwa akae ndani?
 
Burundi wana wagonjwa wawili, na wao wanaficha?
Taarifa zako unaziokota wapi? Burundi ina wagonjwa 3. Burundi haikuwa na kipimo chochote cha kuthibitisha kirusi cha corona. Wamepewa vifaa hivi karibuni, na tayari wamethibitisha uwepo wa wagonjwa 3.
 
maradhi hayafichiki, wagonjwa wa corona wangekuwepo ingejulikana tu.tungeona hospitalini mrundikano wa wagonjwa, kama ni kulipuka, toka mgonjwa wa kwanza agundulike mpaka leo ungeshalipuka kitambo?
Fuatilia maambukizi na mlipuko ili ujue ni baada ya muda gani unategemea mlipuko.

CHINA: Maambukizi Dec - Mlipuko Febr
US & EUROPE: Maambukizi Jan - Mlipuko March
AFRIKA: Maambukizi March - mlipuko ??? (Expected May)
 
SASA WAMEFUNGA SHULE NA VYUO VYA NINI? HAPO NDIO WALITUOGOPESHA WANANCHI NA ANAPASWA KUJUA VYUO NA SHULE VIMEAJIRI WATU WENGI SANA YANI AJIRA RASMI NA ZISIZO RASMI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom