Yaani nimpongeze mtu anayeniongoza kwenda kwenye janga?!!lakini kwanini tusimshukuru na kumpongeza mtu anaejitokeza na kututia moyo/kutufariji kwenye kipindi hiki kigumu,kama kiongozi nadhani anatakiwa kusema anayoyasema[emoji40][emoji40][emoji40][emoji40]
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kile kibri cha rais wa nchi kwamba hatutawazuia watalii kuingia nchini kingepokolewa na hao watalii hivi sasa tungekuwa kati hali gani?! Imekuwa bahati kwetu kwamba wenzetu duniani walizuia hizi international flights vinginevyo hivi sasa tungekuwa tunatafutana kama kweli hivi sasa tupo salama!!
Kama umeshawahi kuishi Zanzibar na Mafia, bila shaka utafahamu jinsi hivi visiwa vinavyopokea Waitaliano wengi kila mwaka!! Sasa ingekuwa bado wanamiminika Zanzibar na Mafia kwavile rais karuhusu, hivi sasa tungekuwa kwenye hali gani?
Au Marekani ambayo ni source kubwa ya utalii wetu... kama wangeendelea kuja hivi sasa tungekuwa katika hili gani?!
Nimesema si mara moja na hapa nitarudia: Angalia historia ya mataifayote yalioathirika sana... kuanzia China, Italy, Iran, Spain na hata US, hawa wote viongozi wao walileta mzaha kwenye coronavirus!!
Huyo Lee Man-hee niliyekupa mfano, mara tu baada ya sala ya Jumapili iliyotangulia, Korea ya Kusini walipofanya testinga, watu zaidi ya 400 walikutwa na COVID-19 na zaidi ya nusu walikuwa ni wafuasi wa Shincheonji Church of Jesus, na wiki 2 after first case, 60% ya waathirika wa COVID-19 Korea Kusini YOTE walikuwa ni wafuasi wa Shincheonji Church of Jesus.