RC Makonda: Watu wanafunga maduka, wanajifungia majumbani kisa Corona, mtakufa na njaa

RC Makonda: Watu wanafunga maduka, wanajifungia majumbani kisa Corona, mtakufa na njaa

Makonda jembe chapa kazi mzee, na kwa sitaili hii wavivu wote hawawei kukuelewa kabisa mbaba
 
Kipara mwenzangu leo ninakuunga mkono.
Kuwa dhamira huenda ni njema lakini kitendo cha kujitokeza hadhara na kutamka waziwazi kuwa watu wachape kazi hatufi na corona...mmh.
Jana tumeomba mkopo Us kwa ajili ya janga hili na leo tunatoa kauli tata kama hizi, hivi tunaelewekaje?
Hizi kauli tata za viongozi muda wowote dunia inaweza kututenga!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani nikifunga duka langu kuna mtu ananidai?kila mtu anachukua tahadhari kwa kiwango anachoona yeye na kulingana na Uchumi wake.
Mimi ni umaskini tu unanisumbua saa hizi ningekuwa kijijini familia yangu
 
Waanze kuwaambia pharmacies zianze ku stock paracetamol za kutosha hilo ndio la msingi; zitahitajika tu mbeleni.

Kutoka au kutokutoka ni choice ya mtu kwa sasa elimu ya kutosha imeshatolewa ulimwenguni jinsi ya kujikinga.
 
Mh. Paul weka akiba ya maneno.
Usitukane mamba kabla ya kuvuka mto, dude likishika kasi unaweza kuonekana kichekesho.
Utakosa mahali pa kuficha sura yako.

Unaweza kuhamasisha watu wakafanye shughuli za kujenga uchumi kwa maneno mengine mazuri bila kuidharau COVID-19
Nakutakia kazi njema mkuu wangu.
 
Kuna wakati hao tunaowaita wataalam na mabingwa waliobobea huwa wanafanya kazi kuwafurahisha wanaowalipa!

Zamani daktari bingwa wa Papa (Mkuu wa kanisa Katoliki la Roma) alitoa maelezo ya kitaalam kuhusu mzunguko wa damu katika mwili wa binadamu kuwa "damu ikitoka kwenye moyo inaenda kichwani ambapo ukutana na roho kisha kurudi kwenye mapafu" Aina hiyo ya wataalam bado wapo hadi karne hii!

Leo CNN wameonyesha kibibi cha miaka 90 kilichoambukizwa korona kimepona wakati "wataalam"$ walisema ni bora kuwanusuru vijana kwa raslimali chache zilizopo kuliko kupoteza kwa kuokoa wazee ambao hawawezi kupona! CCM tuwapuuze ila za kuambiwa changanya za Makonda!
 
Jamani kwanini Tanzania tunaendeela kudhalilika kiasi hiki? Na bado wapo wanaoshangilia kituko hiki
Ninashukuru hiyo clip ipo kwa kiswahili, dunia ingetuona viumbe wa dunia nyingine.
Majirani wana kila sababu ya kutusema! Awamu ya tano ina tufedhehesha sana
Ndugu yangu, we acha tu...washamba na limbukeni tumewasukumizia madaraka yanayowazidi kimo.
 
Yani nikifunga duka langu kuna mtu ananidai?kila mtu anachukua tahadhari kwa kiwango anachoona yeye na kulingana na Uchumi wake.
Mimi ni umaskini tu unanisumbua saa hizi ningekuwa kijijini familia yangu
Tena hawa watetezi wa uzembe wanasema, kitu muhimu ni kujilinda mwenyewe.
Well, mtu anajilinda kwa kufunga duka kisha anasumangwa kwanini amefunga duka.

Makonda alisema Mbowe anasambaza vidudu na alitakiwa awe katika karantini .
Watu wameamua kufanya isolation wenyewe hawakusbiri kuambiwa, imekuwa nongwa

Kilichonitisha ni kusikia Corona siyo Virus! halafu mtu huyo huyo anasema sababu ni kupeleka mikono puani na usoni. Sasa kama si virus hiyo mikono imebeba nini?

Waziri mkuu alisema taarifa zote zitolewe na wizara. Kuna mganga mkuu wa Wizara, naibu Waziri, Waziri na kisha Waziri mkuu. Hawa wote wanaonekana si lolote si chochote kwa amri ya RC.

Hivi nani atakayesema tena suala la utaalam ikiwa RC keshasema ''tokeni mkachape kazi''

Hivi Waziri mkuu na RC nani mkubwa kimamlaka, na kwanini RC wa mkoa mmoja anaweza kutoa kauli zinazoathiri nchi nzima?
 
macho_mdiliko,
Makundi ya vijiwe vya kahawa, bao na drafts yapo menngi sana. Yahani ukweli ni kwamba hali tuliyo nayo imetokana na ukweli kuwa, kuna watanzanaia wachache sana wenye mishe za kwenda nje.

Hii imetupa advantage kwenye viwango na kasi ya maambukizi kuwa hivi yalivyo. Ktk mktadha mwengine kutotoka nje ni kiashiria cha umaskini ulotopea!.
 
Tanzania kukaa ndani hakutawasaidia, hakuna uwezo wowote wa kuhandle hii virus cha kufanya bora mtoke tu nje wengi mpate mpone ili muwe immune,

tatizo ni kwa wale wenye immunity mbaya tu maana hii kitu itawaua ila nchi kama Tanzania ambayo imejaa vijana wengi watapona mapema, wengi watapata kamafua tu au homa wiki mbili then katapita.

Watakaokufa ni wachache compared to mkisema wote mkae ndani na mfunge ofisi, watakaokufa njaa ni wengi ka sisimizi
 
Kipindi ambacho viongozi wote wa dunia hii wanahaha na kutafuta wajifiche wapi ili kuepukana na dhahama hii ya covid19,ni Tanzania pekee tulie na kiongozi anaetoa taarifa tofauti na zile tulizozizoea kipindi hiki (za maambukizi yamefikia...,waliokufa ni....,mjifiche ndani msitoke,nk)

Huyu jamaa namfananisha na Colonel Muammar wa Libya alipojitokeza katikati ya mapambno na kushika kipaza sauti akipita mtaa kwa mtaa akiwaomba wana Libya wajitokeze kupambana.

Makonda mm namuona kama copy & paste ya jamaa maana nae hachoki kujitokeza (maeneo ya msongamano kama stendi na mtaa kwa mtaa kipindi hikihiki cha pandemic na kuwaasa watanzania wajitokeze kupambana)

[emoji870][emoji870][emoji870][emoji870]usichoke mheshimiwa, sisi hatuwasikilizi W.H.O,tunakusikiliza wewe[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli Tanzania wajinga ni weng, ila omba sana hili jambo liishie hapo na lisiwe na madhara makubwa zaid ya hapo kwan ,

kama ikiwa hivo, kutatokea mgogoro wa ndan yaan raia na viongoz walioshindwa kuhamasisha au waliopotosha,

pili jumuia za kimataifa zinaweza kutupuuza ili tukome vizur. Hata kama tumeamua kuupuuza iwe kimya bas si mbwembwe kama hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom