RC Makonda: Watu wanafunga maduka, wanajifungia majumbani kisa Corona, mtakufa na njaa

RC Makonda: Watu wanafunga maduka, wanajifungia majumbani kisa Corona, mtakufa na njaa

Graph,
Kwa taarifa yako: jana huko UK miongoni mwa wagonjwa waliofariki kuna watu 40 ambao walikuwa wazima kabisa. Yaani hawako kwenye risk group.

Unless kama unaniambie Tanzania itumie ursa ya huu ugonjwa kupunguza idadi ya raia wake.
 
Hajawahi kutoa tamko likaeleweka kwa watanzania. Sijui kalaaniwa na nani

In God we Trust
Mmawia hakuna laana yoyote. Ni woga wa sisi raia ndiyo unamfanya azidi kuonyesha ujinga wake.

Alianza kidogo kidogo na mambo ya kijinga akagundua hakuna kikwazo na sasa ameuvaa upumbavu.

Hachagui aongee nini kwani haoni sababu ya kuchagua. Nchi zinazojitambua mjinga kama huyu anaondolewa kama mbwa mwizi hata kama akiyemteua hapendi.
 
Hapa kuna mambo mawili.

1: Makonda aombe Mungu hili janga liishie hapa hapa i.e isitokee kama walivyotutabiria mabeberu kwamba ndani ya wiki mbili zijazo Afrika tutakufa kama inzi maana viongozi wamepuuza maelekezo ya wataalamu. Ugonjwa huu ukiishia hivo Makonda ataibuka mshindi na hadi wataalamu wa afya wataonekana si kitu bali Makonda coz atakua ndio kiongozi mwenye maono atakua ameweza kuendana na matamanio ya wananchi,wengi hawapendi kukaa ndani.

2: Kama ugonjwa ukiua watu wengi hapa kwetu kuliko Kenya, uganda na Rwanda Makonda atalaumiwa sana na watanzania na viongozi wote wa kimataifa. Na hoja zingine kumhusu yeye zitaibuka kama kuzuiliwa kwenda marekani kwani wengi watasema ni kiongozi asiyewatakia mema watu wake, anajiangalia yeye tu.

Tuombe Mungu iwe kama namba 1.
 
Ukiona mtu wa ngazi ya chini ktk nchi anaongea maneno yanakinzana na viongoz walio juu na hakuna anaye jibu basi juwa jambo moja tu anashida ya maadili.

The way mnamuona anaongea ndivyo the way siku moja hamtomuona akiongea tena wala tamani kuita mtu itakuwa siku ngumu kwake ambayo hakutegemea.

Kila zama na kitabu chake.
 
Hata Kama anabebwa Sasa amepitiliza, dunia inatushangaa
 

Attachments

  • 2358382_IMG_2115.mp4
    6.9 MB
Matts, Hivi kwa akili yako endapo JPM angekuwa anaongea lugha tofauti, hivi sasa huyo Makonda angekuwa anaongea huo ujinga?!

Anachoongea na Makonda na Mkubwa wake ni ujinga... na hilo halina mjadala!!!

Ni ujinga kwa sababu hakuna taifa hata moja ambalo lilibaki salama kwa kuwa na mawazo kama hayo... mojawapo ya taifa hilo ni Iran ambao waliamini wangelindwa na Mungu!!

Google mwenyewe "Shincheonji Church of Jesus + Lee Man-hee" ili uone huyo Lee ambavyo aliwajaza ujinga wafuasi wake, na kisha nini kiliwapata kiasi kwamba akalazimika kuomba msamaha kwa majanga ambayo aliwasababishia wafuasi wake!!

Kwa bahati mzuri, nchi za wenzetu hawapendi ujinga, na kwahiyo wakampeleka kotini!!!
 
Ushauri wa kamati ya kushughulikia janga la covid 19 imesema misongamano ipungue mjini na sii Rais wa nchi wala nani anaropoka kuhamasisha watu misongamano jamaa anakuja nakusema watu wakafanye kaz bila kumbuka jiji lake ndio kulikuwa na kitisho. Jaman hiz teuz hazitup viongoz bora ila bora viongoz
 
Mbona magufuli amekimbia jiji na kwenda kuji isolate chato? Mwambieni naye aache uvivu aje achape kazi.
 
Chige, lakini kwanini tusimshukuru na kumpongeza mtu anaejitokeza na kututia moyo/kutufariji kwenye kipindi hiki kigumu, kama kiongozi nadhani anatakiwa kusema anayoyasema[emoji40][emoji40][emoji40][emoji40]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
long live my love,
Hata kama janga halitaleta madhara zaidi bado kabisa Makonda ameonyesha upumbavu wa kiwango cha juu kuliko aliyofanya siku za nyuma na anatakiwa kuwajibishwa na kushtakiwa.

Hatuwezi kusifia mpumbavu anayedharau maelekezo ya wataalam na kucheza kamari mbaya sana.

Ukiambiwa hii ni sumu na ukiinywa lakini kwa bahati usife bado tu utabaki kuwa mpumbavu no matter the outcome.

Mwisho nataka kukumbusha kuwa sisi wananchi ndiyo tunatakiwa kuwajibisha viongozi wajinga kama hawa na siyo tutegemee adhabu anazopewa na nchi nyingine. Makonda ameshafanya ujinga mwingi hata sasa hakutakiwa kuwemo kwenye hiyo nafasi
 
Nimekumbuka ule usemi usemao
"Hata saa mbovu kuna wakati inasema ukweli"

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
 
Gazeti la Mwananchi online limeripoti maneno aliyoyatoa Makonda alipokuwa anatembelea sehemu za Ilala kukagua miradi. Kilichonishangaza ni kuwa huyu mkuu wa mkoa anavyotoa maneno ya kuropoka bila kuwa na scientific evidence.

Kila mara anatuambia Dar Es Salaam ipo salama wakati watu wanaugua na mmoja amefariki...Kuna habari ambazo zinaonekana kuwa za kweli kuhusu kufichwa kwa idadi ya wagonjwa waliopo sasa, Kuna idadi kubwa kuliko hiyo iliyotangazwa na huyo waziri.

Nchi hii hasa awamu hii inaficha habari nyingi sana ndiyo maana tumepata ban ya kufanya application ya D-visa lottery (Inaonekana bado hao viongozi uchwara hawajakoma).

Magufuli amekwenda Chato, hatujaambiwa kama amesharudi Dar (Kuna watu walio kwenye payroll ya CCM watauliza inanihusu/Inatuhusu nini kutaka kujua wapi alipo rais?) Sisi kama walipa kodi tunaolipa mshahara wa rais tunapaswa kujua rais yupo wapi na anafanya nini huko Chato badala ya kuwa Magogoni akishughulia matatizo ya watanzania!

Au atuambie kama amemwachia ofisi Makonda? Maana anazungumza Makonda mambo ya CORONA na hakuna anayemuuliza.

Haya yanayofichwa fichwa yataleta matatizo, Dunia nzima kuna tatizo....Mbona wengine hawafichi? Tunayo figures za nchi zetu na ongezeko la maambukizi linavyokwenda ni kitu cha wazi....Linafahamika.

Kuficha ficha itaigharimu nchi hii, wakati kwingine kumeisha mlipuko huku kwetu kutakuwa ndiyo kumeanza.

VIONGOZI KUWENI WAKWELI
 
Back
Top Bottom