The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Juma Zuberi Homera, ameagiza Jeshi la Polisi wilayani Mbarali kuwakamata wafugaji wote wanaodaiwa kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima na kuharibu mazao.
Dkt. Homera alitoa agizo hilo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Chimala, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Katika mkutano huo, baadhi ya wakulima walilalamikia vitendo vya wafugaji si tu kuchungia mifugo mashambani mwao, bali pia kuwacharaza bakora wanapojaribu kuzuia uharibifu wa mazao yao.
"Hawa si wa kuvumilia. OCD hakikisha unawakamata wote wanaolisha mifugo kwenye mazao ya watu. Hili haliwezi kuendelea huku wananchi wakiteseka na kupoteza chakula chao," alisisitiza Dkt. Homera kwa msisitizo.
Aidha, Dkt. Homera amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mbarali kufuatilia suala hilo kwa ukaribu na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa dhidi ya wahusika wote. Vilevile, ameagiza wakulima waliopoteza mazao yao warejeshewe chakula cha kutosha kwa kipindi cha mwaka mzima, gharama ambazo zinapaswa kubebwa na wafugaji waliolisababisha tatizo hilo
Chanzo Highlands FM