Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk Juma Homera amesema tayari amelielekeza Jeshi la Polisi kuongeza jitihada za kuwatafuta wahusika waliomshambulia kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mdude Nyagali, huku akiahidi Sh5 milioni kwa atakayesaidia kumpata kada huyo alipo akiwa hai au amekufa.
Hata hivyo, amesema pamoja na yeye kutojua tukio hilo, kwakuwa limetokea mkoani kwake akiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ameamua kulifanyia kazi kuhakikisha haki inapatikana, huku akilaani na kusikitishwa na tukio hilo.
Mdude anadaiwa kuvamiwa na kupigwa nyumbani kwake jijini Mbeya Mei 2, 2025 na watu waliojitambulisha kuwa polisi, lakini bado haijafahamika hali ya kada huyo na wapi alipo, hivyo kuibua sintofahamu kwa wafuasi wa chama hicho.
Akizungumza leo Jumatatu, Mei 5, 2025 baada ya viongozi wa Chadema mkoani humo na Kanda ya Nyasa kufika ofisini kwake kujua hatua zilizochukuliwa, Dk Homera amesema yupo pamoja na chama hicho kuhakikisha Mdude anapatikana.
Hata hivyo, amesema kufuatia matukio hayo, anatarajia kukutana na viongozi wa kimila kujadiliana namna ya kukabiliana na sintofahamu hiyo, huku akikiri kuwa hali hiyo inawatisha akitoa matumaini kwa wananchi kuwa mkoa huo utabaki kuwa wa amani.
Pia, Soma