#COVID19 RC Mghwira: Kifo cha Arthur Shoo ni udhihirisho kuwa Corona imerudi hivyo wananchi chukueni tahadhari!

#COVID19 RC Mghwira: Kifo cha Arthur Shoo ni udhihirisho kuwa Corona imerudi hivyo wananchi chukueni tahadhari!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mh Anna Mghwira amesema kifo cha bwana Arthur Shoo aliyekuwa Katibu mkuu wa KKKT dayosisi ya kaskazini ni ushahidi kuwa Corona imerudi tena.

RC Mghwira ambaye ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa katika ibada ya mazishi ya Shoo amesema kamati yake imetoka kutathmini hali ya maradhi haya katika mkoa na amewaomba wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote.

Naye askofu mkuu wa KKKT Dr Shoo amesema kuanzia mwezi January Kanisa limezika watu wengi hivyo amewaomba waumini kuchukua tahadhari tena na tena dhidi ya Corona kwa sababu ugonjwa huu upo na unaua.

Chanzo: Upendo tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Nasikiliza hapa Askofu shoo anashindilia nyundo kuwa sisi tusijione kuwa ni bora kuliko nchi zingine, pia anasema tusijitenge na mataifa mengine katika vita dhidi ya corona
Amina bwashee!
 
Nasikiliza hapa Askofu shoo anashindilia nyundo kuwa sisi tusijione kuwa ni bora kuliko nchi zingine, pia anasema tusijitenge na mataifa mengine katika vita dhidi ya corona. Pa ameshauri kuwa tusifurahie vifo vya wenzetu
"....tusifurahie vifo vya wenzetu.." Askofu Shoo
 
Kwa nini kifo hiki na si vingine vilivyotangulia huyu mama ni mtu mzima naamini ana watoto akiwa kama mzazi ifike mahali aache tabia za akina Mwigulu na wenzie....Nyongo et al...ambao wamepoteza direction.
 
Nasikiliza hapa Askofu shoo anashindilia nyundo kuwa sisi tusijione kuwa ni bora kuliko nchi zingine, pia anasema tusijitenge na mataifa mengine katika vita dhidi ya corona. Pa ameshauri kuwa tusifurahie vifo vya wenzetu
Tuambine ukweli unafikiri hawa wanaopotosha kwamba hakuna Corona siku wakipata na kupoteza maisha watu hawatafurahi? La hasha hata Shoo anajua watu watafurahi ni kawaida.
 
Vingozi wetu waajabu sana huyu mama juzi kakataa kabisa Kilimanjaro hamna Corona leo iweje akiri kuna Corona? Mbona hajielewi?
Anajielewa Sana, sasa km uko ktk mazishi ya mtu ambaye imethibitika amekufa kwa korona utaongea nini zaidi ya kukiri.Kama Wenye msiba wanaongea korona,we Ni nani hata uwakataze. Au ujitoe fahamu useme hamna korona.
 
Back
Top Bottom