#COVID19 RC Mghwira: Kifo cha Arthur Shoo ni udhihirisho kuwa Corona imerudi hivyo wananchi chukueni tahadhari!

#COVID19 RC Mghwira: Kifo cha Arthur Shoo ni udhihirisho kuwa Corona imerudi hivyo wananchi chukueni tahadhari!

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mh Anna Mghwira amesema kifo cha bwana Arther Shoo aliyekuwa Katibu mkuu wa KKKT dayosisi ya kaskazini ni ushahidi kuwa Corona imerudi tena.

RC Mghwira ambaye ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa katika ibada ya mazishi ya Shoo amesema kamati yake imetoka kutathmini hali ya maradhi haya katika mkoa na amewaomba wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote.

Naye askofu mkuu wa KKKT Dr Shoo amesema kuanzia mwezi January Kanisa limezika watu wengi hivyo amewaomba waumini kuchukua tahadhari tena na tena dhidi ya Corona kwa sababu ugonjwa huu upo na unaua.

Chanzo: Upendo tv

Maendeleo hayana vyama!
Msema chochote
 
Back
Top Bottom