#COVID19 RC Mghwira: Kifo cha Arthur Shoo ni udhihirisho kuwa Corona imerudi hivyo wananchi chukueni tahadhari!

#COVID19 RC Mghwira: Kifo cha Arthur Shoo ni udhihirisho kuwa Corona imerudi hivyo wananchi chukueni tahadhari!

Huyo mkuu wa mkoa basi atakuwa mnafiki,maanake juzi wakati meya wa Moshi anawaamrisha wenzie wavue barakoa,kwa kisingizio kwamba Moshi hakuna Corona,sikusikia hamkaripie wala kumpa onyo.
 
Nasikiliza hapa Askofu shoo anashindilia nyundo kuwa sisi tusijione kuwa ni bora kuliko nchi zingine, pia anasema tusijitenge na mataifa mengine katika vita dhidi ya corona. Pa ameshauri kuwa tusifurahie vifo vya wenzetu
Amina,Mtumishi wa Mungu kwa kuwa Mkweli...
 
Huyo mkuu wa mkoa basi atakuwa mnafiki,maanake juzi wakati meya wa Moshi anawaamrisha wenzie wavue barakoa,kwa kisingizio kwamba Moshi hakuna Corona,sikusikia hamkaripie wala kumpa onyo.
Ilikuwa bado haijadhihirika bwashee!
 
Alipofariki Maalim alijua ni mikakati ya ACT Wazalendo kisiasa kuleta taharuki kama alivyowahi kusema bosi!
 
Mkuu,

Kitika uponyaji wa kiroho unatakiwa ukiri umepona kwa imani na kubadili mtindo wa kufikiri na maisha halafu matokeo ya uponyaji huo hujidhirisha unapokiri udhaifu uliokuzonga umetoweka ndipo uumbaji wa imani hiyo hutengeza matokeo chanya.

Lakini unapokuwa unaongozwa namna ya kuivaa imani kwa uponyaji kamilifu ukianza kuonesha wasiwasi na kudharau roho wa Mungu huaihirisha kusimamia uponyaji huo ambapo nguvu za giza hukuvaa kwa nguvu kubwa kiasi ambacho kujinasua itahitaji gharama kubwa sana.

Korona ni roho ya mauti iliyoruhusiwa kuvinjari katikati ya mifumo ya maisha ya wanadamu baada ya kuipa mgongo imani ya kiroho ambayo hata wanasayansi wanakiri kuna nguvu isiyo ya kawaida inayoendesha UHAI na mahusiano ya vitu na viumbe hai na mfu.

Jikinge, lakini usipoteze imani ya kiroho kufanikisha matamanio yako mema.
 
Back
Top Bottom