RC Morogoro awasweka rumande Wakuu wa Shule baada ya shule wanazozisimamia kufanya vibaya mtihani wa Taifa

RC Morogoro awasweka rumande Wakuu wa Shule baada ya shule wanazozisimamia kufanya vibaya mtihani wa Taifa

 
Hii inanikumbusha miaka 20 nyuma huko niliwahi kuchapwa shule ya msingi si kwa kufeli bali kusababisha shule isishike nafasi ya kwanza katika kata yetu, yaani sisi "tuliominiwa" hatukufanya vizuri na si kufeli basi tulichezea mboko hatari
 
Kwani wakaguzi wameona dosari za maandalio, mahudhurio n.k? Shuleni kuna chakula/uji, umbali kati ya shule na makazi, % ya wazazi kati ya wakulima na wafugaji, % ya madhehebu ya dini? Au Dereva akisababisha ajali Askari wote wa kituo wawekwe ndani, wakulima wasipovuna vizuri idala ya kilimo, umwagiliaji na ushirika wawekwe ndani.
 
Haya mambo Mimi huwa sikubaliani nayo kabisa dhidi ya unyanyasaji wa watumishi wa uma,basi tu,hapo kuna sababu nyingi dhidi ya ufaulu hafifu wa watoto ,utakuta mwalimu asilimia zake ni 0.008% huku wazazi na serikali wakichangia kwa asilimia 99%,miundo mbinu mibovu,je mwalimu ndo atumie mshahara wake kuboresha miundo mbinu,lishe duni pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ACHA BWANA HAJAWAWEKA NDANI ILA KAWAVUA MADARAKA YA WAKUU WA SHULE AMBAO SHULE ZAO ZIMESHIKA KUMI DUNI MIAKA MIWILI MFULULIZOOOO ILA ALIO WAWEKA NDANI NI WATENDAJI WA KATA KUSHINDWA KUWASILISHA MAPATO KUTOKANA NA POS WALIZO PEWA ZA KUKUSANYA USHURU
 
Walimu wanachangamoto nyingi hata chama cha walimu ni butu, wanasingiziwa mambo mengi ,walimu hawana motivation,hawajapandishwa dalaja muda umepita,Volume ya kazi imeongezeka kutokana na elimu bule,watoto wanaofundisha ni wengi dalasa moja mwalimu anashindwa kuwamudu.

Hakuna ajira ya walimu muda umepita .Mwanasiasa anayewaweka ndani anapalilia cheo chake chenye masilai makubwa kuliko ya mwalimu.
 
Very wrong!!
Mh Mkuu wa Mkoa (mwalimu).
Mwanzo mbaya.
 
Ukitazama kila pande ya nchi unakutana na ujinga, kuanzia viongozi mpaka vyombo vya habari, unaweza ukahitimisha kuna tabaka la juu linalofanya juhudi za makusudi za kuumea.

Angalia tofauti ya vipindi vinavyotengenezwa kwa fedha ya walipa kodi BBC na aina ya uwekezaji kwenye maudhui ya TBC.
Unamsikiliza katibu mkuu wa chama tena msomi huoni cha kupanua akili, bora umsikilize Greta, binti wa miaka 16 utatoka na kitu.
 
Back
Top Bottom