RC mpya wa Geita ashangaa stendi kuu ya Mkoa kuwa ya matope wakati kuna utajiri wa dhahabu

Kwa Mara ya kwanza Geita imepata kiongozi. SIJAMTAJA mtu
 
Ukanda huo madini yamekuwa yakichimbwa tangu 1940 wakati wa wakoloni wazungu na maendeleo bado wanayasikia redioni tu.
Airport zote Tanzania zinakarabatiwa na zote ni muhimu.

Kumbuka ukanda ule ardhi yake ni madini matupu hivyo ni suala la muda tu maendeleo kufika.
 
Ni vema wangeuendeleza mkoa mzima kuliko walivyobagua na kuwekeza chato tu
 
RC mpya wa mkoa wa Mara na wewe tembelea pale ilipo stendi uongee na wananchi, maana jamaa aliyeondoka sijui alikuwa anafanya kazi gani !.
 
Kiongozi wa wanyonge aliona bora kujenga stand ya ndege kwa kiwango cha lami (Chato International Airport) wilayani, akawaacha wanyonge hawana stand nzuri makao makuu ya mkoa.

Sawa mkuu wa mkoa Rose Senyamule kawaoneshe maendeleo wananchi wa mkoa wa Geita, wapate stand bora ya mabasi kwa sababu hiyo ndiyo level yao siyo uwanja wa ndege wa kimataifa ulioko Chato.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aishangea CCM yake ambayo hukusanya kodi zote za nchi hii!!
 
Mbona kile ki RC kilichokuwepo kilikuwa kinajitutumua sana kilishindwaje kuondoa hiyo aibu, huko si ndiko walinunua gari la DED la 400Mil?
 
Zile mbwembwe za musukuma kumbe stendi yake ni tope tupu kama Bukoba!!
Kwani Kibajaji kwake kuna nini cha maana. Hawa watu kelele nyingi bungeni wakijifanya wafia nchi/CCM kumbe hawana faida kabisa kwa wapiga kura wao. Hata Job naye ni mule mule, Kongwa ni shida tupu.

Akiwa Mwanza siku ya Mei Mosi, Job aliwasema wanamwanza waache kufunika nyumba zao kwa masufuria, akiwa na maana wasiezeke nyumba zao kwa bati zisizo na rangi. Kwake Kongwa na sehemu kubwa ya Mkoa wa Dodoma pamoja na huko kwa Kibajaji, nyumba zao zimefunikwa kwa matope/udongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hiyo pesa iliyowekwa hapo ikisubiri miaka 30 au 50 ijayo iweze kuleta hiyo maana, leo hii isingetumika kujenga madarasa, kutengeneza madawati, kusambaza vitabu mashuleni, kujenga mahospitali, kusambaza madawa mahospitalini nk? Au kote huko tumejitosheleza hadi tukazilaze pesa hizo hapo Chato zije ziwafaidishe wajukuu wetu miaka 50 ijayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…