RC Mtaka yupo sahihi. Ni kweli kabisa viongozi wetu hawana uchungu na elimu ya watoto wetu

RC Mtaka yupo sahihi. Ni kweli kabisa viongozi wetu hawana uchungu na elimu ya watoto wetu

elimu ni nzuri ndio maana imepewa masaa 9, masaa mengine wanafunzi wajifunze stadi za maisha......kwanza wakae makambi na wakeshe kwa ajira gani??.....maana elimu yetu practically haipo vizuri.....
Eti mkuu wa mkoa anashindisha watoto kwa makambi! Makambi pumbaf! Tangu wanaanza shule alikuwa wapi? Wanaingia mwaka wa mwisho wengine hawajui kusoma hata kuandika, anataka washinde kwa makambi.
 
Mtoto wa waziri atasomaje shule dalasa moja wanafunzi 630! Ukimwambia waziri hizi ndo shule zetu wala ahamini sababu ukweli nikuwa mambo ya Kayumba hawayajui kwahiyo matamko yake anaona sawa tu
 
Mtaka ni aina ya viongozi ambao hawataki makuu hasa endapo asilimia kubwa ya watu anao waongoza wana hali duni kimaisha, typical Nyerere style......unaona anavyosisitiza kwamba wao watoto wao wanasoma kule.....viongozi wasio na ubinafsi ndo wanahitajika kwa sasa kwani wanakuwa wanahisi shida za wananchi na wanakuwa tayari kuyachukua kama matatizo yao wenyewe....
Mtaka is so useless that we who know the stupidity in him, won't dare inviting him for any serious event, unless you are fond of theories.
 
Hivi kwanini aombe msamaha wakati yupo sahihi?
Kwanini watu hawataki kuambiwa ukweli?
ccm ni wanafiki kuliko hata shetani ambae ni mwasisi wa uongo.
 
Mtaka is so useless that we who know the stupidity in him, won't dare inviting him for any serious event, unless you are fond of theories.
Nyie mnaosomesha watoto Canada na kwenye International schools hamuwezi ku feel shida za wananchi, acheni Mtaka apige kazi yeye anapenda kutatua matatizo ya wananchi at the grassroots. Nyie endeleeni kukaa kwenye viyoyozi na kutoa matamko kwenye luninga......
 
Mtoto wa waziri atasomaje shule dalasa moja wanafunzi 630! Ukimwambia waziri hizi ndo shule zetu wala ahamini sababu ukweli nikuwa mambo ya Kayumba hawayajui kwahiyo matamko yake anaona sawa tu
Inaghafirisha sana ndio maana mtaka kaongea kwa hamaki kubwa

Unakuta waziri yupo ofisini anakula kiyoyozi hajui chochote kinachoendelea field akitoka humo anaingia kwenye V8 lake lenye full AC anajianzishia ziara uchwara na kujilipa posho na perdiem za kutosha kwa kisingizio cha kukagua miradi ya elimu

Akifika ziarani ana wahadaa wananchi kwamba serikali imeboresha mazingira ya wanafunzi kusomea na kujifunzia na kuajiri walimu wa kutosha na kwakuwa wananchi wengi vijijini hawana uelewa mtambuka wa mambo wanaamini maneno ya waziri huyo kwa kufikiri ana nia njema na elimu ya watoto wao kumbe behind anakuwa na lengo la kutafuta umaarufu wa kujijenga kisiasa ndio maana waziri anaweza kuropoka jambo lolote na wananchi wakampigia makofi lakini anapotokea mtu jasiri kama mtaka kukemea huo unafiki anapigwa mawe
 
Hili la watoto wa viongozi kutosoma shule za serekali niliwahi kumwambia Mwigulu Nchemba. Utetezi aliotoa ni bora angekaa kimya tu.
Watoto wa Mwigulu mwenyewe wapo feza schools ada 9.5M kwa mwaka.

Viongozi wa kiafrika wapo kwa ajili ya matumbo yao tu wala hakuna kingine.
 
Mtaka alikuwa na hoja nzuri ila hakuweza kutumia busara na kujua mipaka ya majukumu ya kazi yake. Waziri wa elimu anamaamuzi juu ya elimu kiujumla . Mtaka angependa kutengua hoja ya waziri wa elimu ni bora angejadiliananaye ili kuleta maelewano mazuri ya kiutendaji. Mtaka kwa kufanya ivi tusishangae kuna siku atakuja kumkemea hata Raisi wetu wa Jamhuri wa Muungano eti sababu anawatumikia wananchi. Mtaka ameonesha ni kiongozi mpenda kujikweza ili magazeti na vyombo vya habari vimtaje taje
 
elimu ni nzuri ndio maana imepewa masaa 9, masaa mengine wanafunzi wajifunze stadi za maisha......kwanza wakae makambi na wakeshe kwa ajira gani??.....maana elimu yetu practically haipo vizuri.....
Watoto Kassim Majaliwa ( Waziri mkuu ) wapo Feza wanasoma hadi saa sita usiku.

Pole wewe na ujinga wako.
 
Eti mkuu wa mkoa anashindisha watoto kwa makambi! Makambi pumbaf! Tangu wanaanza shule alikuwa wapi? Wanaingia mwaka wa mwisho wengine hawajui kusoma hata kuandika, anataka washinde kwa makambi.
Wewe mjinga sana hapo wenye makosa ni mawaziri TAMISEMI na ELIMU sio MTAKA.
 
Mtaka alikuwa na hoja nzuri ila hakuweza kutumia busara na kujua mipaka ya majukumu ya kazi yake. Waziri wa elimu anamaamuzi juu ya elimu kiujumla . Mtaka angependa kutengua hoja ya waziri wa elimu ni bora angejadiliananaye ili kuleta maelewano mazuri ya kiutendaji. Mtaka kwa kufanya ivi tusishangae kuna siku atakuja kumkemea hata Raisi wetu wa Jamhuri wa Muungano eti sababu anawatumikia wananchi. Mtaka ameonesha ni kiongozi mpenda kujikweza ili magazeti na vyombo vya habari vimtaje taje
Mkuu haya mambo yanauma sana watu hawajui tuu. Mtaka alighadhibika kwa hali ya kaya maskini watoto mazingira wanayowekewa na wanasiasa ambao watoto wao hawasomi hizo shule.
 
Mkuu haya mambo yanauma sana watu hawajui tuu. Mtaka alighadhibika kwa hali ya kaya maskini watoto mazingira wanayowekewa na wanasiasa ambao watoto wao hawasomi hizo shule.
Kwa hiyo ameleta ukombozi kwa makambi. Au anachochea waibe mitihani? Ni mkuu wa mkoa, awe na mipango ya kuboresha elimu mkoani kwake siyo kuja na makambi ya wanaofanya mitihani. Yaani wafundishwe maswali na majibu washinde, apewe sifa.

Ndo tatizo la kuwa na wanasiasa waliosoma sanaa. Rais sanaa, waziri mkuu sanaa, wakuu wa mikoa sanaa.
 
Mtaka alikuwa na hoja nzuri ila hakuweza kutumia busara na kujua mipaka ya majukumu ya kazi yake. Waziri wa elimu anamaamuzi juu ya elimu kiujumla . Mtaka angependa kutengua hoja ya waziri wa elimu ni bora angejadiliananaye ili kuleta maelewano mazuri ya kiutendaji. Mtaka kwa kufanya ivi tusishangae kuna siku atakuja kumkemea hata Raisi wetu wa Jamhuri wa Muungano eti sababu anawatumikia wananchi. Mtaka ameonesha ni kiongozi mpenda kujikweza ili magazeti na vyombo vya habari vimtaje taje
Uko sahihi!! Sera ya elimu iko chini ya Wizara na siyo mkuu wa mkoa. Hakuna mkoa wenye sera yake ya elimu. Huyu ni wale waliosifiwa, wao bila kujipima maana yake sasa najiamini ana ufahamu mkubwa wa kila kitu.

Unawezaje kuetegemea makambi yainue elimu mkoani kwako? Anachokifanya ni kulazimisha wafaulu mitihani hata kama kwa kukaririshwa majibu. Hata mkoa aliotoka hakuna mafanikio ya kimkoa.
 
mda mwingne huwa naanza kushawishika na wadai katiba japo siwaungi mkono (nitaeleza siku nyingne)

katiba ina contents nyingi zenye faida ukiachana na vipengele vya tume huru & serikali tatu vs mbili ambayo ndio main focus ya wadai katiba kuliko mengne.

kuna hili la mnyororo wa madaraka ya viongozi wa kitaifa linapaswa liwekwe sana na katiba ili lieleweke vzur

ijulikane wazi rc na waziri nan Boss kwa mwenzake na je wanaweza kuwajibishana?

mifano ni mingi:
Dc vs Das wanavimbiana hadharan
DED Vs DC, WAZIRI Vs NAIBU nk

mtaka anamvimbia ndalichako.mtaka naye anavimbiwa na ras ni vurugu.na hakuna wa kumfukuza mwenzake

huku chini nako mwalimu mkuu na mwalim wa kawaida ni ubabeubabe.
 
Omary nundu (now late) akiwa waziri ktk wizara moja aliwahi kugombana na athuman mfutakamba.

Katibu mkuu wa wizara nae anakwambia yeye ndio boss waziri yeye ni chawa tu wa rais

Pia ipo attitude ya mbunge mwenye jimbo kumdharau mbunge mteule
haya mambo yanaudhi

Huwa najiuliza ikitokea kawaziri fulan kakamvimbia pm majaliwa hadharan.
majaliwa atakuja na reaction gani.

maana kukafukuza hawezi kikatiba.
 
Mtaka alikuwa na hoja nzuri ila hakuweza kutumia busara na kujua mipaka ya majukumu ya kazi yake. Waziri wa elimu anamaamuzi juu ya elimu kiujumla . Mtaka angependa kutengua hoja ya waziri wa elimu ni bora angejadiliananaye ili kuleta maelewano mazuri ya kiutendaji. Mtaka kwa kufanya ivi tusishangae kuna siku atakuja kumkemea hata Raisi wetu wa Jamhuri wa Muungano eti sababu anawatumikia wananchi. Mtaka ameonesha ni kiongozi mpenda kujikweza ili magazeti na vyombo vya habari vimtaje taje
Ndomaana tunataka katiba mpya,unasema kukemea rais kwani hapa halicho hongea kuna uhongo gani na hata kama ni raisi kwani ukweli isisemwe!
 
Kwa kauli hiyo ya waziri kama mtu una uchungu na elimu unaweza kujikuta unatumia lugha ngumu kama aliyotumia Antony Mtaka kukemea uongo huo. Kwa sababu sisi wazazi tunaosemesha watoto wetu kwenye hizi shule za kata ndio tunajua adha wanazopata watoto wetu ikiwemo kukosa vipindi kwa sababu ya kutokuwa na walimu wa sayansi lakini waziri anatoka usingizini na kulipuka kwamba tatizo la walimu wa sayansi limekwisha. Hivi waziri kama huyu unaweza kusema ana uchungu kweli na elimu ya watoto wetu?
Tatizo lililopo ni viongozi wa juu kabisa wa nchi, uwezo wa ku unify education sysrem yetu wanao lakini kwakuwa wana maslahi binafsi juu ya hilo, wanakaa kimya, chukua mfano wa yule aliyefuta masomo kadhaa kwenye shule za sekondari, huwa najiuliza kama wao wangesoma kibaguzi kama wanavyofanya sasa, wangekuwa kwenye hizo nafasi?

Kinachotakiwa ni ku standardise elimu yetu, watoto wote wapate elimu inayofanana, kama mfumo wa kiingereza basi shule zote ziwe hivyo
 
Back
Top Bottom