Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ameagiza kusitishwa kwa mikataba ya muda ya watumishi wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela huku akiahidi kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi ili kuwahamisha watumishi waliokaa muda mrefu
Mtanda ameyasema hayo wakati akisikiliza kero za wananchi wa kata ya Sangabuye pamoja na kata Jirani zilizopo katika wilaya ya Ilemela ndipo ikaibuka migogoro mingi ya ardhi licha ya kuwepo kwa watumishi wengi katika Idara hiyo ndipo akaagiza watumishi wenye mikataba ya muda kusitishiwa mikataba hiyo mara moja
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa akawataka watumishi wenye ajira kuwajibika ipasavyo huku akiahidi kuzungumza na katibu mkuu wizara ya ardhi aweze kuwahamisha watumishi wenye ajira ambao wamekaa katika wilaya hiyo kwa muda mrefu.
Kama katamka hadharani ni Kiki tu, hao ajira za mkataba ardhi wana nguvu balaa, walishamtoa hadi waziri wa ardhi Angelina Mabula baada ya kuwasitishia mikataba yao kama anavyotaka kufanya Side.