RC Mtanda: Lipeni fidia kwanza kabla ya kuchukua ardhi ya Mwananchi

RC Mtanda: Lipeni fidia kwanza kabla ya kuchukua ardhi ya Mwananchi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imetakiwa kuhakikisha inawalipa kwanza fidia wananchi kabla ya kuchukua maeneo yao kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mtanda amesema hayo katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata za Sangabuye, Bugogwa na Kayenze uliofanyika Mtaa wa Nyafula, Mei 12, 2026 kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao.

Pia soma:
~
Halmashauri ya Ilemela Kitengo cha Ardhi baadhi ya Maafisa wanazungusha Watu ilimradi tu 'ueleweke'
~ Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mwanza yachukua hatua kuboresha Huduma Za Ardhi Ilemela
~ RC Mtanda: Idara ya Ardhi Ilemela hakuna nidhamu, mikataba ya muda isitishwe

Ametoa pole na hongera kwa kuwa na moyo wa uvumilivu kwa wananchi wanaodai fidia tangu mwaka 2022 huku akitoa kipindi cha miezi mitatu kwa uongozi wa Manispaa ya Ilemela kuanzia mwezi Mei hadi Julai 2026 kuhakikisha wananchi wote waliopisha maeneo yao kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo wanalipwa fidia.

“Nitumie fursa hii kutoa pole kwa wananchi wote wale wanaohangaika na madai ya fidia kwa muda mrefu sasa madai yenu yote yatalipwa, nakuaelekeza mkurugenzi wa manispaa kwa kipindi cha miezi mitatau kuanzia mwezi Mei hadi Julai 2026 wananchi wote hao wanaodai fidia wawe wamelipwa na pia kuanzia sasa hakuna kuchukua eneo lolote kabla ya kulipa fidia” Alisema RC Mtanda.

Naye, Amiri Mohamed Mkalipa, mkuu wa wilaya ya Ilemela amemshukuru mkuu wa mkoa kwa kufanya mkutano huo na wananchi na kutatua changamoto zao hasa za migogoro ya ardhi na kuahidi kuwa maelekezo yote aliyotoa watayatekeleza kama alivyoagiza na anaamini kuwa changamoto zilizotolewa na wananchi zitaendelea kutatuliwa na kumalizwa kabisa.

Nao wananchi wa Sangabuye Bi.Agnes Buswelu Kakila kutoka mtaa wa Nyafula, Bw Jenerali Bahebe kutoka mtaa wa Igalagala na Renatus Boniphace Bujashi kutoka mtaa wa Ilekako wamemshukuru mkuu wa mkoa kwa kuja kuwasilikiza na kutatua kero zao zilizokuwa zinawasumbua kwa muda mrefu ikiwemo shida ya maji, umeme na barabara kwani kupitia yeye zimeweza kupatiwa ufumbuzi wa kudumu na wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kufanya kazi, kulinda Amani na kuiletea nchi maendeleo.
 
Back
Top Bottom