RC Paul Makonda: Mbowe ameahirisha mikutano ya CHADEMA baada ya mwanaye kuambukizwa Corona

RC Paul Makonda: Mbowe ameahirisha mikutano ya CHADEMA baada ya mwanaye kuambukizwa Corona

Huyo mtoto wa Mbowe wakati mwingine hata hajihusishi na siasa, anayo mipango yake mengine. Mfalme Suleiman aliomba hekima kwa Mungu ili aweze kuongoza jamii aliyopewa, baada ya kujiona yeye ni dhaifu. Tuwaombee viongozi wawe na hekima katika kunena na kutenda; wenye majivuno, Mungu aonyeshe uweza wake kwao.
 
Je ndiko tumefikia kwa wagonjwa was Korona kutajwa kwa majina?, Kwamba makonda ni mwenye dhamana yakutoa taarifa kuhusu wagonjwa??. Hakika nachelea kusema uteuzi was vijana wengi awamu hii umeonesha kiasi gani vijana hatuna uwezo wakuongoza kwa weledi, I hope next term turudishe wazee tu tujifunze toka kwao.
Usiseme wazee, sema watu wazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aisee!! hakika utawala wa awamu hii umefitinika
watu wanaungana kupambana ma hili dude sisi tunadharauliana kias hiki??
 
idawa,
Na ndiyo maana nimesema hapa, Tanzania ni nchi ambayo huwezi kuelewa Kwa haraka, Msomi ni yupi na mjinga ni Yupi,

Kwa hiyo mtu akipatwa na maradhi,Kwa mwingine inakuwa sherehe siyo?

Tunawatu wa ajabu kweli, hata kama Mbowe si wa upande wako, Kwa hiyo akiugua wewe unashangilia, majitu mengine utadhani yametokea sayari ya wapi ata hakijulikani

Mwenyezi Mungu irehemu Tz na watu wake
 
Hivi mtu anayechaguliwa kuwa mkuu wa mkoa Dar ndo anakua msemaji mkuu wa serikali au juzi rais sikumuelewa vizuri maana waziri mkuu na waziri wa wa afya wote nawafahamu msemaji Tu wa serikali nilikuwa simfahamu
 
Bashite ni zaidi PM hapa tz, angekuwa rc wa kawaida angeshatumbuliwa siku nyingi. Bashite analindwa na haya: Ni msukuma, ana uhusiano usiofaa na mamlaka za uteuzi, ni mjinga kama..... nk
 
Hivi hawa watu hawawezi kabisa kufanya mambo yao bila kuwa taja taja hawa wapinzani? Hii inamaanisha jambo moja kuu kwamba wanawaogopa sana tena sana pamoja nakujinasibu kuwa wanapendwa mana kama kiongozi anaweza kabisa kuelimisha watu kwakujikita moja kwa moja kwenye corona pasipo.

kuanza kuingiza hisia zakisiasa na lazima afamu hii corona hata yeye inaweza kumpata kwakushiriki mikusanyiko isiyo yalazima kama hii anahatarisha afya yake nawananchi pia na isitoshe anakiuka miongozo iliyotolewa na serikali na wizara ya afya yakutokusanyika!!!!ni aibu kubwa na ukumbuke huyu Mungu hadhihakiwi
 
Kuna Wakati, mtu hata kama akiwa ni sisiemu, akataliwe tu aambiwe hatakiwi kuwemo kwenye chama, na sababu iwe ni kwamba, anadharirisha wastarabu wengi walioko huko

Kwani huyo jamaa akikataliwa sisiemu itakufa? Mimi sina chama, ispokuwa ni mshabiki mzuri wa mtu mmojammoja.

Bashite hafai, huwezi furahia mabaya ya binadamu mwenzako
 
Hivi CCM naona sasa ebu tuwazungumzie kwa ukali kidogo.

Hivi Makonda na genge lako ni lini mtatofautisha siasa na kazi,

Ni lini Utatofautisha mzaha na hekima.

Ni lini tuwasubiri mkue ili tuwaamini?

Huu si wakati wa mzaha kwenye gonjwa hili.

RC Makonda nilikuwaga ninawaza waza pia kwamba huenda ukawa mkubwa baadaye.

SASA Nimethibitisha ni baaado sana. labda baada ya miaka 20 ndiyo kichwa kitatuli.

Ushauri kwa RC Makonda.

Sio WanaCCM tu wanaopigaga kura au kukuchafua au kukuharibia. acha na personal attach unapokuwa kiongozi kama wewe tena katika jambo la msingi namna hii.

Sasa kwa kauli yako wengi tunaanza kuelewa Corona ni kama maigizo tanzania.

Maana hata uptodate hatupati , watu wanachanganyika hatujui yupi mgonjwa yupi mzima, Mkoa gani unashida au La.

Jamani jamani jamani jamani CCM ninawaonja tena.

Nchi ya italia walifanya makosa haya haya tunayoyafanya mwisho wa siku wakajikuta nchi nzima imepata virusi vya corona. Chonde chonde acheni siasa kwenye corona.

Ninapinda kuwakumbusha kunawa mikono kwa maji yanayochuruzika kwa sabuni na hakikisha unanawa mara kwa mara na usshike pua au mdomo kwa mikondo.
 
Huyu ni dhahiri ana uwendawazimu wa aina fulani. Mwenye akili hawezi kusema hivyo.
 
kweli taifa hili kamwe halitakaa liishe vilaza! Hivi hata kama ni kweli je mamlaka ni yake kutangaza hili? Shame on him! sijui atakua lini!
 
CCM ni chama cha watu wavijijiniwasiokuwa na umeme wala maji.
Mkuu, ukisema hivyo, utakosa hoja ya kusema CCM haileti maendeleo, ukijisifia mahali unapoishi kwamba Ni pazuri unasifia maendeleo yaliyoletwa na CCM

Mponde huyo mmoja tu naye ni Bashite, hafai haswaa si kidogo
 
Back
Top Bottom