RC Paul Makonda: Mbowe ameahirisha mikutano ya CHADEMA baada ya mwanaye kuambukizwa Corona

Hakuna tatizo.. ila shida ni MATAGA kusifia kana kwamba ni jambo moja la kishujaa na la kimkakati kitaifa, kumbe just person.
Ile ni picha tu, na MATAGA kusifia au kutosifia ni maoni yao. Yapo mengi yanayofanyika kimkakati na yana tija.
 
Daaah! mbona jina la mwanae Mbowe sijalisikia au bashite ana list yake.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mhe. Mbowe,

kaa kwa tahadhari kubwa kuanzia ofisini, kwenye gari Hadi nyumbani na familia yako.

Watu wabaya wameshaanza kujionesha kusema mtoto wako kaugua corona.

Wasije wakakumwagia upupu wa Corona kuthibitisha kauli zao.

MUHIMU:

WAZIRI WA AFYA AU WAZIRI MKUU AU RAIS WATHIBITISHE MTOTO WA MBOWE KUUGUA CORONA.
 
Mambo kama haya,ndiyo yanapelekea hata Mungu asisikie maombi yetu.
Viongozi wa kisiasa wanawapa waombaji wakati mgumu sana wa kulitubia taifa mbele za Mungu.
 
Mungu anajua kwanini kampa uongozi huyo dogo ila siye watanzania hatuelewi kabisa kwakua ni mipango ya Mungu basi tunaomba atakalo lifanyike maana hatumuelewi
Huu ndio upumbavu unaotufanya tuishi maisha ya dhiki kwa huu ulimwengu. Kutuaminisha hilo ulisemalo mthibitishe huyo mungu?!
 

Huo wote ni wivu tu baada ya kuona wananchi tuliguswa sana na kujitolea michango yetu kuwanusuru viongozi wa cdm na hukumu iliyokuwa imepangwa juu yao.sasa wanatafuta kila namna ya kuwadhoofisha kitu ambacho wameshashindwa miaka yote 4 waliyoshika dola..kiufupi ni kwamba wanatapatapa ni watu wa kupuuzwa tu hao
 
Majaliwa akimgusa Makonda atatimuliwa kama Mbwa koko siku hiyo hiyo , mguse mtafuta waganga na mpanga mauaji uone moto !
Ha ha haaa ! Kamanda, taarifa zako nawe...duh! Tukisema tupe ushahidi usiotiliwa shaka juu ya taarifa zako hizi; uko tayari!?
 
Dah Makonda kanyimwa akili aisee. Ungonjwa wa mtu ni siri kati ya daktari na muhusika

Kiongozi unasimama kwenye umma kisha unaropoka siri za mtu, siri za nchi ataweza kutunza kweli huyu zero brain

Sent using Jamii Forums mobile app
 
toka nchi hii ipate uhuru sidhani kama kumewahi kuwa na RC nonsense kama huyu. Nyimwa vyote ila pewa akili
 
KAMA ANAYETAKIWA KUTANGAZA HABARI ZA CORONA NI RAIS, WAZIRI MKUU, AU WAZIRI WA AFYA TU NA MAKONDA KATANGAZA HABARI ZA CORONA BASI MAKONDA ANA CHEO KIMOJAWAPO AU VYOTE VYA HAO WANAOPASWA KUTANGAZA HABARI ZA CORONA
 
Kama kweli Mbowe anaweza kuongoza na kufanya mikutano nchi nzima licha ya uwepo wa katazo serikali basi Mbowe na Chadema wana nguvu.

Vinginevyo sioni sababu ya RC kumover rate Mbowe.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mungu anajua kwanini kampa uongozi huyo dogo ila siye watanzania hatuelewi kabisa kwakua ni mipango ya Mungu basi tunaomba atakalo lifanyike maana hatumuelewi
sauti ya wengi ndio sauti ya Mungu, wengi hatumtaki, huyu kachaguliwa na magu wala usimsingizie Mungu.
 
Yani natamani ningesema ila basi tu ngoja kwanza nikae kimya.
 
Kwani Keegan hawezi kuugua corona?
Tunaweza kumuaga duniani kabisa akabaki hana tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…